CHADEMA yavunja rekodi Tunduma

CHADEMA yavunja rekodi Tunduma

The Conquerer

Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
79
Reaction score
94
Leo CHADEMA kimevunja rekodi katika mji mdogo wa Tunduma baada ya maelfu ya wakazi wa mji huo kuhudhuria kwa wingi mkutano wa hadhara uliohutubiwa na mbunge wa Musoma Mjini Mh. Vincent Nyerere akiwa na mwenyeji wake mbunge wa jimbo la Mbozi Magharibi Mh. David Silinde.

Katika mkutano huo, Mh.Nyerere alisema wakati umefika sasa wananchi kuchukua hatua na kukiondoa madarakani Chama cha Mapinduzi CCM kwa kuwa serikali yake ndiyo iliyowasababishia wananchi umasikini uliokithiri kwa kupora rasilimali za nchi na kuziuza kwa mabepari kwa bei chee kwa faida ya viongozi peke yake.

Mh. Nyerere amekemea tabia ya viongozi wa serikali kuwasomesha watoto wao nje ya nchi huku watoto wa masikini wakikosa huduma hiyo, na hivyo kujenga matabaka kati ya wenye elimu na wasio na elimu, matajiri na masikini jambo ambalo ni hatari kwa mustakabali wa amani ya taifa letu.

Aidha Mh. Vincent nyerere aliitaka serikali kuwajali wananchi bila kubagua kwa kuwa serikali ya sasa inawajali watu matajiri kuliko masikini. Hii ni kutokana na kuuwawa kikatili kwa mwanachama mmoja wa CHADEMA katika mji wa Tunduma tarehe 15/12/2012 na serikali haijachukua hatua yoyote.

Amemtaka mkuu wa polisi nchini inspekta Said Mwema kutuma jopo la wapelelezi ili kuwabaini wauwaji hao na kuchukua hatua kali kama alivyofanya kwa kifo cha aliyekuwa mkuu wa polisi mkoa wa Mwanza na wakubwa wengine.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Mbozi Magharibi, Mh. David Silinde alitumia mkutano huo kueleza mafanikio makubwa aliyoyapata kwa muda mfupi wa miaka miwili tangu ameingia madarakani. Ametaja miradi ya barabara, ujenzi wa madarasa ya shule, na miradi ya maji ambayo imefanikiwa chini ya uongozi wake akisaidiana na mh. Diwani wa tunduma nd. Frank Mwakajoka.

Tazama picha jinsi miamba miwili, mh. David Silinde (sauti ya simba) na mh. Vincent Nyerere mbunge wa Musoma Mjini walivyotingisha mji wa Tunduma.



SAM_0459.JPG
 

Attachments

  • SAM_0428.JPG
    SAM_0428.JPG
    1.1 MB · Views: 233
  • SAM_0435.JPG
    SAM_0435.JPG
    1.1 MB · Views: 250
  • SAM_0414.JPG
    SAM_0414.JPG
    85.9 KB · Views: 226
Kinachonifurahisha wananchi wamekuja wenyewe bila kusombwa wala ahadi ya pilau maana hakuna aliyevaa uniform hii inaonyesha wamekwenda kwa matakwa yao na mapenzi yao kwa wana Ukombozi.
 
Kama kawaida chadema hainunui watu kama ccm wananchi wanakubali,hii ni safari njema kwa watanzania kuelekea uchaguzi mkuu 2015
 
Leo chadema kimevunja rekodi katika mji mdogo wa tunduma baada ya maelfu ya wakazi wa mji huo kuhudhuria kwa wingi mkutano wa hadhara uliohutubiwa na mbunge wa musoma mjini mh. Vincent nyerere akiwa na mwenyeji wake mbunge wa jimbo la mbozi magharibi mh. David silinde. Katika mkutano huo, mh.nyerere alisema wakati umefika sasa wananchi kuchukua hatua na kukiondoa madarakani chama cha mapinduzi ccm kwa kuwa serikali yake ndiyo iliyowasababishia wananchi umasikini uliokithiri kwa kupora rasilimali za nchi na kuziuza kwa mabepari kwa bei chee kwa faida ya viongozi peke yake. Mh. Nyerere amekemea tabia ya viongozi wa serikali kuwasomesha watoto wao nje ya nchi huku watoto wa masikini wakikosa huduma hiyo, na hivyo kujenga matabaka kati ya wenye elimu na wasio na elimu, matajiri na masikini jambo ambalo ni hatari kwa mustakabali wa amani ya taifa letu. Aidha mh. Vincent nyerere aliitaka serikali kuwajali wananchi bila kubagua kwa kuwa serikali ya sasa inawajali watu matajiri kuliko masikini. Hii ni kutokana na kuuwawa kikatili kwa mwanachama mmoja wa chadema katika mji wa tunduma tarehe 15/12/2012 na serikali haijachukua hatua yoyote. Amemtaka mkuu wa polisi nchini inspekta said mwema kutuma jopo la wapelelezi ili kuwabaini wauwaji hao na kuchukua hatua kali kama alivyofanya kwa kifo cha aliyekuwa mkuu wa polisi mkoa wa mwanza na wakubwa wengine.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la mbozi magharibi, mh. David silinde alitumia mkutano huo kueleza mafanikio makubwa aliyoyapata kwa muda mfupi wa miaka miwili tangu ameingia madarakani. Ametaja miradi ya barabara, ujenzi wa madarasa ya shule, na miradi ya maji ambayo imefanikiwa chini ya uongozi wake akisaidiana na mh. Diwani wa tunduma nd. Frank mwakajoka.

Tazama picha jinsi miamba miwili, mh. David silinde (sauti ya simba) na mh. Vincent nyerere mbunge wa musoma mjini walivyotingisha mji wa tunduma.



View attachment 75655

Bado Nape atasema hajaiona hiyo nyomi.
 
Safi sana cdm...Mungu azidi kutupigania tufikie malengo.... nimesikia kwenye gari la matango la cdm jioni hii Mh.v nyerere atakuwepo Iringa pia mwenyewe taarifa zaidi anijuze pls.
 
Tanzanians are no longer tolerant of the acts of ccm, they need a change not only a change but a positive one that can make them out of impecunious lives, they do not want to be as imbecile as their top leader who thinks that the quantity of traffic in the country is an indicator of development as he thinks on bum. Viva chadema!
 
Na bado. Kesho mh. Vincent nyerere mbunge wa musoma mjini atatua iringa kuungana na mwenyeji wake mh.peter msigwa mbunge wa iringa mjini katika harakati za kuuelimisha umma juu ya haki zao na lengo la kushika madaraka ya nchi. Wana iringa jitokezeni kwa wingi. Mkutano ni saa nane mchana.
 
hii picha ya tatu, hichi ndicho kizazi kitakachoimaliza ccm
 
Lakini bila tume huru ya uchaguzi,bila katiba mpya,bila kujiandikisha kupiga kulinda haki zetu za kupiga kura ambazo ni hati/vitambulisho vya kupigia kura kwa kuishinda njaa kwa maana ya kutoviuza,bila kushinda ghiliba za chama cha majoka yanayoghilibu watu na kununua hati zao za kupigia kura,safari ya ukombozi itakuwa bado ni ndefu sana.
 
Mungu endelea kuwajaza pumzi makamanda hawa na hatimae ccm kife kifo cha kawaida
Leo CHADEMA kimevunja
rekodi katika mji mdogo wa Tunduma baada ya maelfu ya wakazi wa mji huo
kuhudhuria kwa wingi mkutano wa hadhara uliohutubiwa na mbunge wa
Musoma Mjini Mh. Vincent Nyerere akiwa na mwenyeji wake mbunge wa jimbo
la Mbozi Magharibi Mh. David Silinde.

Katika mkutano huo, Mh.Nyerere alisema wakati umefika sasa wananchi
kuchukua hatua na kukiondoa madarakani Chama cha Mapinduzi CCM kwa kuwa
serikali yake ndiyo iliyowasababishia wananchi umasikini uliokithiri kwa
kupora rasilimali za nchi na kuziuza kwa mabepari kwa bei chee kwa
faida ya viongozi peke yake.

Mh. Nyerere amekemea tabia ya viongozi wa serikali kuwasomesha watoto
wao nje ya nchi huku watoto wa masikini wakikosa huduma hiyo, na hivyo
kujenga matabaka kati ya wenye elimu na wasio na elimu, matajiri na
masikini jambo ambalo ni hatari kwa mustakabali wa amani ya taifa letu.

Aidha Mh. Vincent nyerere aliitaka serikali kuwajali wananchi bila
kubagua kwa kuwa serikali ya sasa inawajali watu matajiri kuliko
masikini. Hii ni kutokana na kuuwawa kikatili kwa mwanachama mmoja wa
CHADEMA katika mji wa Tunduma tarehe 15/12/2012 na serikali haijachukua
hatua yoyote.

Amemtaka mkuu wa polisi nchini inspekta Said Mwema kutuma jopo la
wapelelezi ili kuwabaini wauwaji hao na kuchukua hatua kali kama
alivyofanya kwa kifo cha aliyekuwa mkuu wa polisi mkoa wa Mwanza na
wakubwa wengine.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Mbozi Magharibi, Mh. David Silinde
alitumia mkutano huo kueleza mafanikio makubwa aliyoyapata kwa muda
mfupi wa miaka miwili tangu ameingia madarakani. Ametaja miradi ya
barabara, ujenzi wa madarasa ya shule, na miradi ya maji ambayo
imefanikiwa chini ya uongozi wake akisaidiana na mh. Diwani wa tunduma
nd. Frank Mwakajoka.

Tazama picha jinsi miamba miwili, mh. David Silinde (sauti ya simba) na
mh. Vincent Nyerere mbunge wa Musoma Mjini walivyotingisha mji wa
Tunduma.



View attachment 75655
 
Back
Top Bottom