PreGE2025 CHADEMA yavunja rasmi kambi ya kumtafuta Mdude Nyagali aliyetoweka Mei 2, 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,437
Reaction score
5,235
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Mbeya Kusini magharibi mwa Tanzania kimetangaza kuvunja rasmi kambi iliyokuwa imewekwa kushinikiza kupatikana kwa kada wao, Mdude Nyagali aliyetoweka tangu Mei 02, 2025.

Mdude anadaiwa kuvamiwa na kupigwa nyumbani kwake mtaa wa Iwambi jijini Mbeya tangu Mei 2, 2025 hajapatikana huku Chadema ikitumia njia tofauti kumtafuta mwanaharakati huyo bila mafanikio.

Akizungumza leo Jumatano Mei 21, 2025 Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Mbeya, Masaga Kaloli amesema baada ya kupata vitisho ikiwamo kumwagiwa vitu vinavyodhaniwa kuwa ni sumu, wameona harakati za kumpigania Mdude zihamie nyumbani ili kuokoa maisha ya wengine.

Amesema zipo njia nyingi za kuendelea kupambania kila mwananchi na mfuasi wa chama hicho na Mbeya itaendelea kuwa mfano kupitia tukio la Mdude. Masaga pia aliiomba Serikali na vyombo vya dola kusaidia kupatikana kwa mwanaharakati huyo.

Pia, Soma

"Tumeona kuendelea kuwa hapa ilihali tunapitia vitisho vyenye nia ovu bora tutumie njia nyingine kudai haki ya Mtanzania huyu, hadi sasa tunaomba Serikali na mamlaka nyingine zisaidie kupatikana kwa Mdude, sisi tutatoa aina yoyote ya ushirikiano kwa yeyote" amekaririwa Masaga akizungumza na Gazeti la Mwananchi.
 
Je wajinga na wafata upepo mnataka muone mfano gani ili muwe mnaelewa mnapoambiwa acheni kudanganywa na wanasiasa wanawatumia kikinuka wataoumia ni ndugu zako tu
Fanya siasa bila kutukana watu matusi kila siku, wako watu wana uwezo wa kuvumilia matusi na wako hawana. Wewe unajuwa unamtukana mtu mwenye nguvu kuliko wewe lakini ukiamka wewe ni matusi tu kila siku ni kama unataka waje wakushike upate kick, iko siku wanakuchukuwa mazima halafu wa bongo tunajijuwa wiki 2 tunakusahahu.

Kweli unatoka nyumbani una watoto hujali wote hao unaenda kutukana viongozi hujui siku moja utapatwa na nini? Unaweza kufanya harakati na ukawa maarufu bila kutoa matusi ya nguoni. Baada ya mwezi tu hutasikia habari yoyote watu watarudi kwenye Wasafi Festival......na Singeli
 
Mdude alidhani ataondoka kama shujaa cha ajabu huko chadema nobody cares wako busy kumpraise Lissu. Kuna yule Soka nae ashasaaulika alikuwa anatembea na kifimbo anajikuta Nyerere awa watoto wanadanganywa sana uko wanaweka maisha yao rehani kijinga
 
Ushujaa utamsaidia nini kweli? unaacha family yako watu wanaokupenda eti shujaa wa nini? watu wenyewe unataka kuwapigia hawana habari.
 
Unatukana nini na huo ndio ukweli. Kwani yeye ndio wa kwanza kupotea? wangapi hata kuongelewa tu hawaongelewi vijana wadogo kama kina Soka. nani anaumia hivi sasa sio wazazi wake? wako wapi wanasiasa waliokuwa nyuma yenu. Hawana habari wao wana malengo yao pia.... kubali ukweli
Kwahiyo unashangilia watu kupotezwa na kupelekwa kusikojulikana badala ya kushauri mamlaka zizingatie utawala wa Sheria? Wakosaji wakamatwe na kupelekwa mahakamani na siyo kusikojulikana!
 
Fanya siasa bila kutukana watu matusi kila siku, wako watu wana uwezo wa kuvumilia matusi na wako hawana. Wewe unajuwa unamtukana mtu mwenye nguvu kuliko wewe lakini ukiamka wewe ni matusi tu kila siku ni kama unataka waje wakushike upate kick, iko siku wanakuchukuwa mazima halafu wa bongo tunajijuwa wiki 2 tunakusahahu.

Kweli unatoka nyumbani una watoto hujali wote hao unaenda kutukana viongozi hujui siku moja utapatwa na nini? Unaweza kufanya harakati na ukawa maarufu bila kutoa matusi ya nguoni. Baada ya mwezi tu hutasikia habari yoyote watu watarudi kwenye Wasafi Festival......na Singeli
wachungaji nao wanatukana fr kitima alitukana?
 
Mkuu hii point yako mimi Kila siku naihubiri huku lakini nimefurahi wewe kuona hiki kitu.

Katika nchi hii usipokuwa makini watu wanaweza kukufanya uwe na kiburi na ukafura kichwa huku wakionesha kuwa wako nyuma yako pale utakapokumbwa na changamoto lakini ukweli ni kwamba ukipata changamoto watu watapiga kelele siku mbili na siku ya tatu watakusahau na familia a yako hibaki taabuni.
 
Ushujaa utamsaidia nini kweli? unaacha family yako watu wanaokupenda eti shujaa wa nini? watu wenyewe unataka kuwapigia hawana habari.
we ni mmojawapo huna habari
 
Mdude alidhani ataondoka kama shujaa cha ajabu huko chadema nobody cares wako busy kumpraise Lissu. Kuna yule Soka nae ashasaaulika alikuwa anatembea na kifimbo anajikuta Nyerere awa watoto wanadanganywa sana uko wanaweka maisha yao rehani kijinga
Cdm wanataka ubunge na ruzuku tu
 
Unatukana nini na huo ndio ukweli. Kwani yeye ndio wa kwanza kupotea? wangapi hata kuongelewa tu hawaongelewi vijana wadogo kama kina Soka. nani anaumia hivi sasa sio wazazi wake? wako wapi wanasiasa waliokuwa nyuma yenu. Hawana habari wao wana malengo yao pia.... kubali ukweli
Kama siasi haikunufaishi kwa kiasi kikubwa bora uache, Leo hii lisu au Dr Slaa akikamatwa na kuwekwa ndani anapewa treatment Kama mfalme bila kujalisha ukubwa au udogo wa kosa alilofanya lakini mtu mwingine alifanya kasa linaloshabihiana na la la lissu anapewa adhabu Kali ikiwemo kupotezwa kabisa.

Viongozi kama akina lisu Wana brand kubwa ambayo inawafanya walinde na jumuiya za kimataifa, sasa nyoka wa mtaani eti amwiga lisu alifikiria atapata treatment zinazofanana😂😃.
 
Mdude alidhani ataondoka kama shujaa cha ajabu huko chadema nobody cares wako busy kumpraise Lissu. Kuna yule Soka nae ashasaaulika alikuwa anatembea na kifimbo anajikuta Nyerere awa watoto wanadanganywa sana uko wanaweka maisha yao rehani kijinga
Mkuu inasikitisha sana aise.

Dahhh!
 
Ewe mtanzania omba sana kwa bidii,
Maombi yako yana nguvu ya kubadilisha vitu vikubwa tu,usione kwamba maombi ni kazi ya watu fulani....noooooo
Ni wewe mwenyewe hapo,omba na familia yako pamoja,ukiwa kazini tamka neno juu ya Tanzania,ukiwa shuleni tamka neno juu ya Tanzania..
WAEFESO 3:20
✌️Zingatia neno kwa kadiri ya NGUVU itendayo kazi ndani yako
AMINA
 
Back
Top Bottom