CHADEMA yatangaza kiama cha CCM

CHADEMA yatangaza kiama cha CCM

sir.JAPHET

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2012
Posts
699
Reaction score
137
Jumanne, Januari 01, 2013 07:37 Na Benjamin Masese, Dar es Salaam

*Yamuonya Spika Makinda
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) itaondolewa madarakani na watumishi wa umma. Chama hicho kikuu cha upinzani kimesema kuwa, CCM itaondolewa madarakani iwapo haitapandisha mshahara wa kundi hilo kabla ya mwaka 2015.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi Chadema, John Mnyika, alisema nguzo pekee iliyobaki kwa CCM ni watumishi wa umma, ambao wanauwezo mkubwa wa kuiangusha.

Mnyika alisema ndani ya miaka miwili Chadema imefanikiwa kueneza sera na malengo yao na kufanikiwa kuungwa mkono kwa asilimia 90 ya Watanzania wasio watumishi wa umma.

Alisema kazi iliyobaki hivi sasa ni kukata nguzo hiyo iliyosalia ambayo ni watumishi wa umma na kuwataka walimu, madaktari na watumishi wengine wa idara zote za Serikali kuondoa hofu ya kupoteza ajira zao na kuungana na Chadema ili kuiondoa madarakani.

"Hatuingii Ikulu mwaka 2015 kwa fadhila wala hila za CCM, bali tunaingia kwa nguvu ya umma na ishara za nguvu ya umma zimejidhihirisha jinsi wananchi walivyounga mkono Vuguvugu la Mabadiliko (M4C).

"CCM itarajie nguvu kubwa mwaka unaoanza kesho (leo), baada ya ratiba ya kikao cha Kamati Kuu kukaa na kuweka mpango kazi, CCM isidhani inaweza kuisambaratisha Chadema kirahisi kama inavyofikiri.

"Kwanza wao wenyewe wameanza kutofautiana kauli, juzi Naibu Katibu Mkuu Bara, Mwigulu Nchemba amesema ifikapo 2016 Chadema itakuwa imekufa.

"Wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Uhusiano na Uratibu), Steven Wassira aliwahi kusema Chadema itakufa baada ya mwaka mmoja sasa hapo nani mkweli?

"Ni vema CCM ikaachana na propaganda za uchaguzi wa mwaka 2015 na badala yake iwatumikie wananchi kwa kupanua vyanzo vya mapato na kutumia rasilimali za nchi ili watumishi wa umma waweze kuongezewa mshahara wao vinginevyo watajutia.

"Hadi sasa asilimia 90 ya wananchi wasio na kazi wanaunga mkono M4C na mara zote wamekuwa wakiwalaumu watumishi wa umma kwa kuiunga mkono CCM kwa kuhofia kibarua chao. Sasa tunawaomba kuungana nasi ili kuiondoa CCM madarakani," alisema.

Mnyika alisema ameshangazwa na kitendo cha Nchemba kushindwa kutangaza majina ya wabunge sita wa Chadema walioomba kujiunga na CCM, kama alivyoahidi badala yake ameendeleza propaganda.

Alisema CCM inapaswa kuwaeleza Watanzania juu ya mpango wao wa kujivua gamba umefikia wapi na kwa nini imeshindwa kutatua migogoro inayowakabili wananchi huku miaka 50 ya uhuru ikiwa imepita.

Yamuonya Spika Makinda

Akizungumzia namna chama chake kilivyojipanga kwenda bungeni mwaka huu, Mnyika alisema wabunge wa Chadema wamejipanga kwenda na mfumo mpya wa kuwasilisha maoni, hotuba, maswali na uchangiaji bungeni.

Mnyika alitoa wito kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda kuongoza Bunge mwaka 2013 kwa kufanya marekebisho ya kanuni na kumtaka atambue kwamba anaongoza chombo cha juu.

"Huu ni wito kwa Spika Makinda anapaswa kubadilika mwaka huu, lazima atoe nafasi kwa wabunge wote kuishauri na kuisimamia Serikali, ili aweze kutenda haki lazima asimamie upande wa wananchi.

"Atambue maendeleo ya haraka ya nchi hayapatikani kwa mbunge mmoja mmoja kutoa fedha zake kwa wananchi wake bali wabunge wote kushirikiana na Serikali kuendeleza mipango ya maendeleo," alisema.

Tathmini ya mwaka 2012

Akitoa tathmini Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Katibu Mkuu, Victor Kimesera alisema mwaka 2012 ulioisha jana ulikuwa mwaka wa ubakaji wa demokrasia ulioambatana na matukio ya mauaji ya wananchi.

Kimesera alisema vitendo vilivyotokea mwaka 2012 kama mauaji ya raia wasio na hatia, bidhaa kupanda bei, umeme, nauli na vitu vingine ni matokeo ya Serikali kushindwa kutenda haki kwa Watanzania.

Aliwataka wananchi kutokata tamaa na maisha yao kwani Chadema bado ina matumaini y
a kuwakomboa hasa pale watakapoungana pamoja na katika kuiondoa CCM madarakani.
 
Tanzania hatuendelei kwa sababu wanasiasa - hasa wale waliopewa madaraka- wanatumia muda mwingi kubuni na kusimamia mambo ya hovyo kabisa. Kama Taifa, tumekubali kuwa na mfumo wa vyama vingi vya siasa, sasa iweje leo hii CCM wanatumia muda mwingi kuuwa vyama vya upinzani? Hivi huo ndio ushindani?

Kwa nini hawajifunzi toka nchi nyingine? Nchi za wenzetu, vyama vinashindana kwa sera, sisi hapa na akili za kuzimu tunashindana kwa 'mamluki' na kupandikiza migogoro. Hii ni aibu na inaonesha ni jinsi gani wanasiasa wetu wana akili za ujima! Ni dalili mojawapo ya kufilisika hoja.

Nitumie mfano wa team ya mpira wa miguu: Team ya Simba watataka kuishinda Yanga kwa kucheza uwanjani na sio kuleta hila ambazo zitaifanya Yanga ishindwe kucheza mechi, hivyo kuwapa Simba ushindi wa mezani.

Kama CCM wanajiamini wana sera nzuri, na utendaji wao unakubalika kwa wananchi sioni kwa nini watumie muda mwingi kuaanda mbinu za ushindi wa mezani? Kwanini wasiingie uwanjani tuone 'chenga' za kila team? Kuua upinzani tafsiri yake unahofia uwezo wako! Na linasikitisha kuna wanasiasa vijana wanaoendesha hizi siasa za uwoga!

Competition ni jambo zuri, CCM acheni woga!
 
Nasikia wafanyakazi wengi wanasema bado hawajalipwa na serikali mshahara wa desemba mwaka uliopita. Hii ni aibu. Ccm ni janga!
 
Selikali utumbo utumbo tu, hakuna cha maana inacho wafanyia watumishi wake, zaidi ya kuwakandamiza na mikodi ya ajabu ajabu isiyo na tijaaa
 
Hapa kazi kweli kweli, mimi mpaka sasa kiukweli kabisa ninaamini kwamba hawa wawili wote ni adui zetu, Administrators walio serikalini na watawala CCM wote wawili ni tatizo kubwa sana kwetu.

Naiomba CHADEMA iwe makini sana inapoanza kutafuta kuungwa mkono na kundi hili la wafanyakazi wa serikali sababu nalo ni chanda na pete na wanasiasa walio ccm katika kuikamua nchi yetu.

Kwa mfano, askari polisi.
Hawa ni wafanyakazi wanaolipwa mishahara midogo sana, ni wafanyakazi wanaoishi maisha magumu sana kutokana na kulazimishwa kukakaa kwenye makazi duni sana, wanafanya kazi katika mazingira magumu sana, na mara kadhaa wamekuwa wakiombwa kutokutumia nguvu kukabiliana na harakati za chadema kukomboa taifa letu kwa sababu zaidi ya wao ndugu zao ni sehemu ya watanzania watakaofaidika na ukombozi huu lakini wapi, askari polisi kwa sasa wanazidi kujipambanua kama wapinzani wa mabadiriko kuliko hata ccm wenyewe, sababu wako tayari kuua kwa ajiri ya kulinda vibarua vyao.

Taarifa za karibuni zinaonyesha kwamba jeshi la polisi ni moja ya taasisi za serikali yetu zinazoongoza kwa rushwa, askari polisi wote hata makuruta, ni sehemu ya jamii yetu inayobaka haki za watanzania kwa kukumbatia rushwa katika kila nyanja ya utekelezaji wa majukumu yao.

naomba chadema wawe makini sana katika kushirikiana na watu hawa.
Lakini nawatakia kila la kheri
 
Hili ni tamko madhubuti kabisa lililotolewa na kijana hodari asiyeyumba.
 
Tunataka mwaka huhu tuwamalize wote walioko ccm wasio nufaika wahamie chadema wabaki wale walio fisidi nchi ili mipango ya kuwanyonga ianze 2014 kwa haraka sana. Kwa m4c twaweza mungu ibariki chadema mungu wabariki viongoz wa CHA DE MA.
 
True. ccm ni janga lakini "the ground beneath their feet has shifted" they should brace for the worst.
 
Ndo maana nawakubali cdm, yaani wanatetea mpaka haki za wanyonge wa ccm, viva cdm
 
Tanzania hatuendelei kwa sababu wanasiasa - hasa wale waliopewa madaraka- wanatumia muda mwingi kubuni na kusimamia mambo ya hovyo kabisa. Kama Taifa, tumekubali kuwa na mfumo wa vyama vingi vya siasa, sasa iweje leo hii CCM wanatumia muda mwingi kuuwa vyama vya upinzani? Hivi huo ndio ushindani?

Kwa nini hawajifunzi toka nchi nyingine? Nchi za wenzetu, vyama vinashindana kwa sera, sisi hapa na akili za kuzimu tunashindana kwa 'mamluki' na kupandikiza migogoro. Hii ni aibu na inaonesha ni jinsi gani wanasiasa wetu wana akili za ujima! Ni dalili mojawapo ya kufilisika hoja.

Nitumie mfano wa team ya mpira wa miguu: Team ya Simba watataka kuishinda Yanga kwa kucheza uwanjani na sio kuleta hila ambazo zitaifanya Yanga ishindwe kucheza mechi, hivyo kuwapa Simba ushindi wa mezani.

Kama CCM wanajiamini wana sera nzuri, na utendaji wao unakubalika kwa wananchi sioni kwa nini watumie muda mwingi kuaanda mbinu za ushindi wa mezani? Kwanini wasiingie uwanjani tuone 'chenga' za kila team? Kuua upinzani tafsiri yake unahofia uwezo wako! Na linasikitisha kuna wanasiasa vijana wanaoendesha hizi siasa za uwoga!

Competition ni jambo zuri, CCM acheni woga!
Kaka hapo umenena na inaonekana unawajua vizuri hawa majamaam, kinachowala kwa sasa ni hofu na woga usio na maana na wameshaona wamechokwa ile mbaya. na c wabunifu wa kuleta mambo mapya yatakayowavuta watu ambao wamekosa imani nao badala yake wanatishia watu masuala ya vita oh sijui wapinzani wanavurugu yaani hawana pa kushika. Tuendelee kuwaelimisha na watanzania wenzetu waliombali ili nao waunganishe nguvu ili tuwapumnzishe hawa maveterani ambao kwa sasa wanatembea kila kona ya nchi kueleza walivyotekeleza ilani ya uchaguzi(matusi). kweli tuna kazi
 
Nakubalia na Mnyika 100% see the attachment mjionee wenyewe maisha ya watz tena wasomi alafu useme kuna serikali. Serikali gani imesahau hata elimu ambayo ndo nguzo muhimu katika nchi shame on CCm
 
Tunataka mwaka huhu tuwamalize wote walioko ccm wasio nufaika wahamie chadema wabaki wale walio fisidi nchi ili mipango ya kuwanyonga ianze 2014 kwa haraka sana. Kwa m4c twaweza mungu ibariki chadema mungu wabariki viongoz wa CHA DE MA.

Mmh....punguza mumkali! hata kama CCM wanafanya madudu, lakini CDM ikiingia mzdarakani 2015 lazima izingatie utawala wa sheria ili watakaohukumiwa wawe wliopatikana n'a hatia n'a mahakama zetu!!
 
Mtaji mwingine mkubwa wa ccm ni ujinga wa watanzania! Uchaguzi ukifika watahongwa tena kanga, chumvi na vitenge watasahau shida zao za nyuma na hivi wataichagua ccm tena!!!! CDM ihamasishe wananchi kuhusu huu mtaji pia!!!!
 
hivi ni kweli watumishi wa umm bado wako sissiem? mi naamini wengi wameshajitoa, wameacha tu mashati huko walishaondoka mda mrefu
 
Back
Top Bottom