Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 137,304
- 271,567
Taarifa ya Chama hicho iliyosambazwa kote Duniani hii hapa.
===================
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Job Yustino Ndugai, kilichotokea tarehe 6 Agosti 2025 jijini Dodoma.
Soma Pia: Job Ndugai, aliyewahi kuwa Spika wa Bunge afariki Dunia
Mhe. Ndugai aliwahi kulitumikia Taifa akiwa Mbunge wa Jimbo la Kongwa, Naibu Spika, na baadaye Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Alikuwa sehemu ya uongozi wa Bunge katika kipindi cha mabadiliko ya kisiasa na mijadala muhimu ya kitaifa.
Chadema tunatoa pole za dhati kwa familia ya Marehemu, wananchi wa Jimbo la Kongwa, marafiki na wote walioguswa na msiba huu.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe. Amina.