Na Rushyd Ahmed - London
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya UK, Jumamosi ikiyopita kilifanya uchaguzi wa viongozi wake wa kanda hiyo, ili kusimamia shughuli zote za Chama hicho nchini Uingereza.
Mkutano huo wa uchaguzi ambao ulifanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya RE, Hackney London na kusimamiwa na Mbunge wa Ubongo, Tanzania Mhe John Mnyika, ulimchagua Salim Amar Saad kuwa Mwenyekiti kanda hiyo.
Awali, kabla ya uchaguzi huo kufanyika wanachama na watu wengine waliyohudhuria walihitaji kupatiwa ufafanuzi wa maswali kadhaa kuhusu utaratibu uliyotumika katika kuwapata viongozi wapya wa kanda ya UK.
Baada ya vurugu ya maneno kuonekana kuwa na hoja za maana katika kutaka kujuwa uhalisia wa kamati ya muda iliyoratibu kupatikana kwa uongozi huo, Mnyika alitoa ufafanuzi wa kina kutuliza jazba ya wana-Chadema.
Mnyika alisema Katiba ya sasa ya Chadema, iko kimya kuhusu Chama hicho kuwa na uongozi au Tawi lake nje ya nchi, lakini alisema hakuna ubaya wa kufanya hivyo. Na alinukuu Katiba ya Chama hicho, jinsi inavyoeleza taratibu za uchaguzi.
Hoja hizo ziliibuka kutokana na kamati ya 'CHADEMA UK' ya muda kufanya upembuzi wa majina ya wanachama wa Chedema, waliyoomba nafasi mbali mbali za uongozi katika kanda ya Uingereza, kuchujwa na kubakishwa jina moja moja kwa kila nafasi, jambo ambalo lilionekana kuwa ni kosoro za kidemokrasia.
Akitoa mchanganuo wa malalamiko hayo Mnyika, aliweza kuwatuliza wana-Chadema na kuwataka wale wote waliyoomba nafasi za uongozi na majina yao kuenguliwa baada ya kuonekana kukosa sifa, wasimame. Hata hivyo, hakuna mtu aliyejitokeza.
Baada ya hatua hiyo, ndiyo ilipokubalika kwa watu wote walihudhuria mkutano huo kwamba uchaguzi huo uendelee na waliyoomba nafasi za uongozi kutakiwa kujieleza na kupigiwa kura.
Baadhi ya nafasi za uongozi wa 'Chadema UK' ziko wazi baada ya waliyojitokeza kuwania kukosa sifa zinazotakiwa. Moja ya nafasi zilizoachwa wazi ni pamoja na nafasi ya mwenyekiti wa 'Bavicha UK'.
Kwa mujibu wa vigezo vilivyopitishwa na Kamati ya kuratibu uongozi huo, chini ya mratibu wake wa muda Dk Allex Parino, juu ya nafasi hiyo, ilihitajika mtu huyo kukijua Chama hicho, mwenye uwezo wa kukisemea, kuratibu na kusimamia shughuli zake, pia uwezo wa kimenejimenti na kisiasa.
Sifa nyingine ni kuwa muunganishi asiye na 'undumi wa kuwili', mwenye nidhamu ya kichama na kazi, aliye tayari kujitolea na awe ni mwanachama wa Chadema na mwenye uwezo wa kufanya kazi.
Kutokana na vigezo hivyo, waombaji walioomba kuchaguliwa kwa nafasi hiyo walionekana kukosa vigezo, jambo ambalo uongozi mpya, utaitangaza tena nafasi hiyo, ili wanachama zaidi waweze kuiomba.
Katika taarifa iliyotolewa na mratibu wa muda wa kanda ya UK, Dk Parino hakukuwa na mwisho wa kupokea maombi ya waliyohitaji kuwania nafasi hiyo, lakini hadi jana waliotuma maombi hawakuwa na sifa.
Mkutano huo pia uliwachagua Goodluck Mboya kuwa Katibu wa CDM-UK, Matthew Allex Jutta Katibu Mwenenzi wa CDM-UK, Muweka Hazina CDM-UK ni Edwin Francis Kisenha na Mrs Petronella Mwakatuma ni Mwenyekiti wa Bawacha-UK.
Wengine waliyochaguliwa kwenye uongozi mpya wa Chadema-UK ni Miss Margaret Malekia anakuwa Katibu wa Bawacha-UK, na nafasi ya Katibu wa Bavicha-UK imechukuliwa na Bernard Charles Irondo.