Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Dar es Salaam. Chadema imesema kitendo cha waziri kuagiza mafuta bila ya kushindanisha zabuni na kusababisha bei katika soko la ndani isishuke kadri inavyotakiwa, kina harufu ya ufisadi na hivyo kumtaka Rais John Magufuli kutumbua majipu ya waliohusika katika sakata hilo.
George Simbachawene, akiwa Waziri wa Nishati na Madini wa Serikali ya Awamu ya Nne, aliagiza mafuta hayo kwa ajili ya miezi ya Septemba, Oktoba na Novemba kwa maelezo kuwa sheria inamruhusu kufanya hivyo anapokuwa na sababu.
Waziri Simbachawene alisema Februari 19 mwaka huu kuwa, alichukua uamuzi huo kwa kuwa nchi ilikuwa inaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu na kulikuwa na wasiwasi wa hali ya usalama.
Uamuzi wa Simbachawene, ambaye sasa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), ulisababisha mafuta hayo kununuliwa kwa Sh40 bilioni, ambayo ni mara mbili ya bei ambayo ingetumika kama zabuni zingeshindanishwa.
Wakati anachukua uamuzi huo, tayari kulikuwa na zabuni mezani zilizokuwa zikisubiri kushindanishwa, lakini kitendo cha kuzingatia utaratibu huo kilisababisha mtu aliyepewa kazi hiyo kuweka bei ya juu ambayo imesababisha mafuta kutoshuka kwa kiwango kinachotakiwa.
Jana, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika alisema kuna harufu ya ufisadi katika suala hilo.
“Uamuzi wa waziri kupuuza ushauri wa Ewura ambayo ni mamlaka ya udhibiti, unaonyesha ipo haja ya uchunguzi juu ya nini kilimsukuma kuchukua uamuzi huu,” alisema Mnyika, ambaye ni Waziri wa Nishati na Madini wa Kambi ya Upinzani bungeni.
“Mara nyingi vigogo wa Serikali hupiga dili (hufanya mpango wa fedha) kwa kisingizio cha Uchaguzi Mkuu. Pili, Rais Magufuli atueleze atalitumbua vipi hili jipu kwa sababu bei ya mafuta ipo juu wakati katika soko la dunia imeshuka na hii inatokana na athari katika mfumo wa uagizaji wa mafuta.”
Alisema jambo hilo ni lazima lichunguzwe na wahusika kuchukuliwa hatua kwa maelezo kuwa kama ungefanyika ushindani, ni wazi kuwa bei ya mafuta ingekuwa chini na kuwa nafuu kwa wananchi.
“Lazima tuhakikishe kuwa hakukuwa na mianya ya rushwa kwa sababu wakati mwingine wanapochagua kampuni moja na kuacha kampuni nyingi huwa kunakuwa na mazingira ya ufisadi,” alidai Mnyika.
Alisema iwapo suala hilo halitachunguzwa, Chadema italivalia njuga na kuliibua katika mkutano ujao wa Bunge la Bajeti utakaoanza Aprili 19.
Akizungumza na Mwananchi Februari 19, Simbachawene alisema alichukua uamuzi huo kwa nia njema kwa ajili ya usalama wa nchi.
“Kama kwenye uchaguzi kungetokea uhaba wa mafuta na watu wakaingia barabarani (kuandamana), mimi ningekuwa sina la kusema,” alisema Simbachawene.
Juzi, Ewura ilitangaza kushuka kwa bei ya bidhaa za petroli kwa asilimia 1.70, ikiwa ni mara ya nne mfululizo kwa viwango vya nishati hiyo kushuka tangu Desemba mwaka jana.
Lakini bado bei hiyo haijashuka kufikia Sh1,652 kama ilivyokuwa Machi mwaka jana wakati bei ya mafuta ghafi duniani ilipokuwa dola 47.70 za Marekani kwa pipa, sawa na Sh87,434 (dola 1 ilikuwa sawa na Sh1,833 mwaka 2015).
Hadi jana, bei ya mafula katika soko la dunia ilikuwa dola 36.40 za Marekani kwa pipa kwa mujibu wa marketwatch.com. Bei hiyo ni sawa na na Sh78,951.6 kwa kuwa hivi sasa dola moja ni sawa na Sh2,169.
Mwananchi ilipata habari kuwa bila ya Waziri kuagiza mafuta hayo, bei za mafuta nchini zingeshuka zaidi ya kiwango cha sasa, iwapo zabuni ya kuagiza mafuta kwa kipindi hicho ingefanyika kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za ununuzi wa mafuta kwa pamoja (BPS).
Wakati huo, Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Ewura, Titus Kaguo alilieleza gazeti hili kuwa mafuta hayo yalikuwa kwenye tenda hizo namba 37, 38 na 39 za Septemba, Oktoba na Novemba, ambazo hazikushindanishwa.