CHADEMA yampuuza Nape

CHADEMA yampuuza Nape

Kihega

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2010
Posts
1,339
Reaction score
180
Wana JF.
Baada ya Katibu wa halmashauri (NEC) ya CCM Nape Nnauye kupatwa na malaria ya kupanda kichwani, CHADEMA kupitia kwa mkurugenzi wa mawasiliano na Habari Mh.John Mnyika wamesaidia kumpa tiba.

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimempuuza Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM, Nape Nnauye, kikisema kuwa madai yake yanalenga kuhamisha wananchi kwenye hoja.

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Habari wa CHADEMA, John Mnyika, amesema kuwa madai hayo ya Nape yanadhihirisha kile alichowahi kukisema bungeni kuwa nchi imefika hapa ilipo kutokana na upuuzi wa CCM.

Kauli ya CHADEMA inafuatia madai yaliyotolewa na Nape juzi mjini Kahama, mkoni Shinyanga juzi kwenye mkutano wa hadhara kuwa chama hicho kupitia kwa katibu mkuu wake kilipewa fedha na wafadhili nje ya nchi ili kuvuruga mchakato wa Katiba unaoendelea sasa.

Mnyika alisema kuwa ameshangazwa na madai hayo ya Nape ambayo aliyaita ya kipuuzi kutolewa mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.

"CCM kupitia Nape imetoa madai hayo kwa lengo la kuhamisha mjadala kutoka kwenye muswada mbovu wa sheria ya marekebisho ya Katiba uliopitishwa kwa nguvu bungeni," alisema.

Alisema kuwa Katibu wao Mkuu, Dk. Willibrod Slaa, hajawahi kupewa fedha zozote nje ya nchi kwa ajili ya kukodi helikopta ili kuvuruga mchakato wa Katiba kama alivyodai Nape.

Aliongeza kuwa katika tukio hilo kanuni za Bunge zilivunjwa na Naibu Spika, Job Ndugai, hivyo kuathiri hadhi na heshima ya Bunge kwa kuruhusu wabunge kushambuliwa, kudhalilishwa na kuhamishwa bungeni na watu wasiohusika.

Mnyika alihoji kuwa kwenye udhaifu kama huo wa kiti cha spika kwa maelekezo ya CCM inawezekanaje CHADEMA kuvuruga mchakato huo unaoendeshwa kimizengwe licha ya wao kuwa waasisi wa hoja ya Katiba mpya. "Madai ya CCM kupitia Nape ni ya kipuuzi na yanalenga kuwakatisha tamaa wananchi juu ya kazi inayofanywa na CHADEMA ya kuunganisha nguvu ya umma wa Watanzania dhidi ya udhaifu wa rais na uzembe wa Bunge linalohodhiwa na CCM katika mchakato wa Katiba mpya," alisema.

Aliongeza kuwa CCM inalenga kurudisha nyuma Watanzania kwenye uamuzi unaosubiliwa kwa hamu.
Mnyika aliongeza kuwa CCM ilikataa kuandika Katiba mpya mbali ya Watanzania kuidai kwa nyakati tofauti na kuzimwa mpaka CHADEMA iliposhinikiza kupitia wabunge wake kutoka bungeni.

Kwamba baada ya kuandaa maandamano ndipo rais akakubali mchakato wa Katiba mpya uanze.

"CCM haikuwa na sera ya kuanzisha mchakato wa Katiba mpya, haina uhalali wa kimaadili wa kuinyooshea kidole CHADEMA iliyokuwa na sera ya Katiba mpya kwa madai ya kutumwa na mataifa ya nje kukwamisha mchakato huo," alisema.

Mnyika alisema kuwa CCM imetoa msimamo na ufafanuzi wa maoni ya kupinga mazuri kwenye rasimu ya Katiba mpya. Kwamba inashangaza badala ya kuboresha mchakato wa kupata Katiba mpya yenyewe inataka kuuchakachua.

"Baada ya kushindwa kufanya hivyo kupitia mabaraza ya Katiba yaliyosimamiwa na Tume ya Marekebisho ya Katiba na mabaraza ya wazi yalioendeshwa na CHADEMA mengine kwa helikopta na mengine bila helikopta katika maeneo mbalimbali nchini, imeanza kuhadaa watu.

"Mbinu iliyobaki sasa kwao ni kuichakachua kwenye Bunge Maalumu la Katiba kwa kupenyeza watu wake kupitia kumpa rais mamlaka makubwa kwenye kuteua wajumbe 166 na pia kufanya uamuzi upite kwa wingi wa kura," alisema.

Source:Magazeti
 
Bunge maalum la katiba lichaguliwe na Rais halafu bado liitwe maalum, umaalum wake unatoka wapi sijui hawa watu wana balaa hawa! Tunadai KATIBA MPYA ili kuondoa haya mambo ya mtu mmoja kutuchagulia mwakilishi the way tunachaguliwa ma-RC na ma-DC, on the way, tutumie njia zile zile tunazozikataa halafu anasimama Nape aliyekosa aibu kusema CDM inaharibu mchakato.

Hivi makundi yakijichagulia wawakili CCM inaumwa wapi ikiwa kweli ina nia njema na hili zoezi?
 
Wamempuuza au wamekosa majibu ya tuhuma nzito zinazowakabili?
 
Kikwete aliwahi kusema huwa anapata hofu sana nepi anaposhika mic maana ni mropokaji na hajui ataropoka nini,huyu jamaa ni mpuuzi na anapaswa kupuuzwa hata mwenyekiti wake anamjua kuwa ni mpuuzi.
 
Tunaomba helikopta ianze kuwafuatilia Nape na Kinana kwa kuanzia Kahama ikiwa imewabeba Mnyika, Tundu Lisu na Heche ili uwongo wao kwa wananchi uwekwe wazi
 
Wamempuuza au wamekosa majibu ya tuhuma nzito zinazowakabili?

Mimi Nape ninamfahamu toka ngudu sec huwa nimropokaji tu na hawezi kujenga hoja.Aliingizwa kwenye siasa na baba yake mzee nape baada ya kukataa shule ili awe anapata hata fedha za kujikimu tu kwa hiyo nawaomba sana watanzania mumdharau na kumpuuza huyu nape.
 
Nape kwa kuropoka hajambo wakuu chadema kuruka na chopa ni ki2 cha ajabu?hawajaanza leo wala jana ndani ya chadema kuna watu Mungu kawajalia mf Ndesamburo huwa anatoa chopa kwa ajili ya shughuli za chama mfano mdogo kama huo Nape hawezi kuona
 
kwanza Nape angetujulisha,vp ule mkataba wa jengo la umoja wavijana aliokuwa anaupgia kelele je umerekebshwa?au alkuwa anataka ngazi yakupandia juu?na baada kufka alkokuwa anataka kufka kapga kimya.Nape weeeee kura bata kjana,kila mbuzi akula urefu wa kamba yake.jtaid 2015 na wwe utnge mjengon ukagonge meza.
 
ccm inaongoza kwa viongozi waropokaji hakuna asiyejua kama wao kuropoka ni kawaida
 
kwanza Nape angetujulisha,vp ule mkataba wa jengo la umoja wavijana aliokuwa anaupgia kelele je umerekebshwa?au alkuwa anataka ngazi yakupandia juu?na baada kufka alkokuwa anataka kufka kapga kimya.Nape weeeee kura bata kjana,kila mbuzi akula urefu wa kamba yake.jtaid 2015 na wwe utnge mjengon ukagonge meza.
 
Wamempuuza au wamekosa majibu ya tuhuma nzito zinazowakabili?

Ccm mnaendelea na sarakasi zenu. Nyie ndio mko madarakani. Vyombo vyao ulinzi na usalama viko chini yenu. Kama kuna ukweli, je sheria inasemaje kuhusu hili jambo. Kama sheria inaruhusu ccm nao watakuwa wanafanya hivyo hivyo. Kama sheria hairuhusu mahakama ziko wazi.

Acheni ngonjera zenu zisizokuwa na kichwa wala miguu.
 
Wamempuuza au wamekosa majibu ya tuhuma nzito zinazowakabili?

Nadhani wamejaribu kufanya tofauti na mahasimu wao kwa kupuuza hizo tuhuma kwani wangekuwa CCM najua kila kiongozi angeropoka kama sehemu ya kujaribu kuokoa chama.
 
Magamba kwa sasa wanafanya ile methali ya kibaya chajiuza,kizuri chajitembeza kuwa na maana zaidi.
 
Back
Top Bottom