- Source #1
- View Source #1
Wakuu kuna hii Taarifa nimekutana nayo inaeleza kuwa Chadema wamemfukuza mbowe kutokana na kile wanachokiita kwenda kinyume na maazimio ya No refoms No election. Je ni kweli?
- Tunachokijua
- Freeman Mbowe alikuwa ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuanzia mwaka 2004 hadi 2025 ambapo alishindwa uchaguzi na Mwenyekiti wa sasa Tundu Lissu.
Madai
Ipo barua inayosambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo Facebook Julai 21, 2025 ikiwa na nembo ya Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ikieleza kuwa kamati kuu ya chama hicho inatangaza rasmi kufukuta uanachama Bw. Freeman Mbowe.
Uhalisia wa madai hayo
JamiiCheck imefuatilia na kujiridhsisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli.
Kupitia utafutaji wa maneno muhimu JamiiCheck imejiridhisha kuwa taarifa hiyo haijachapishwa wala kutolewa na chanzo chochote cha kuaminika.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii hawajachapisha wala kutoa taarifa hiyo kwa Umma kama inavyooenaka, hivyo taarifa hiyo ni ya kughushi.
Aidha barua hiyo imetumia aina tofauti ya mwandiko (Fonts) jambo linaloendelea kudhihirisha kuwa taarifa hiyo ni ya kughushi na haijatolewa na CHADEMA.
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA-Bara, John Heche amefanya mahojiano na Upendo TV ambapo pamoja na mambo mengine Heche aliulizwa kuhusiana na uwepo wa Freeman katika chama hicho ambapo alijibu kuwa Freeman Mbowe bado ni mwanachama na mjumbe wa kamati kuu wa chama hicho.
“Ni mjumbe wa kamati kuu ya chama kama alivyo mzee Mtei. Kwa mtu yeyote ambaye amefikia nafasi ya mwenyekiti wa Taifa wa chama chetu atakuwa mjumbe wa kamati kuu ya chama maisha yake yote” - John Heche, Makamu Mwenyekiti CHADEMA