figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,485
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimelaani vitendo vya kusababisha vurugu na kuandaa matukio ya udhalilishaji kwa viongozi wa CHADEMA yanayofaywa na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akiongea na Wanahabari mapema asubuhi Kaimu Katibu Mkuu, Salum Mwalimu alisema kitendo kilichotokea jana katika Halmashauri ya Kilombero kwenye uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo ambapo Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali alizalilishwa mbele ya wananchi baada ya aliyekuwa mwenyekiti wa kikao hicho Azimina Mbilinyi kutoa amri Mbunge huyo atolewe nje.
Mbilinyi alitoa amri kwa polisi waliokuwemo ndani ya ukumbi huo kwamba wamtoe nje Mbunge huyo kwa kile alichokidai kuwa hakupaswa kuwepo kushiriki upigaji kura huku akidai kwamba amepokea maelekezo hayo kwa Waziri George Simbachawene.
Kitendo hicho alichofanyiwa Lijualikali ni cha udhalilishaji kwani njia waliyotumia kumtoa nje ilikuwa ni ya mabavu.
“Naamini kwamba matukio yanayofanywa katika Halmashauri ambazo UKAWA tumeshinda yanapangwa na CCM kwa kushirikiana na Serikali yake kwani ni matukio ya uzalilishaji na kwa nini yafanyike kwenye maeneo ambayo sisi tumeshinda na si maeneo ambayo wao wameshinda?”. Amesema Mwalim.
Mwalim amesema, Halmashauri ya Kilombero inaongozwa na UKAWA kutokana na kuwa na Madiwani na wabunge wengi kuliko CCM, ambambapo uchaguzi huo sasa unagailishwa kwa mara ya tatu, huku CCM wakiwa na madiwani pamoja na wabunge viti maalumu 18 huku UKAWA wakiwana na 20.
“Pamoja na ushindi wa UKAWA kuonekana wazi wazi lakini bado CCM wanaleta figisufigisu ya kuleta hata wabunge wanje ili mradi tu washinde."
Hawataweza kutushinda hata kwanini maana hata sisi tukipeleka wabunge toka nje bado tutawapita. Na hiyo ni ishara ya kutuogopa”.
Amesema Mwalim
Hata hivyo, Mwalim amesema, kutokana na kitendo alichofanyiwa Mbunge wa Kilombelo jana wanaitaka serikali kulichukulia uzito suala hilo na kuhakikisha Mkurugenzi huyo aliyetoa amri kwa polisi kutumia mabavu kumtoa nje Mbunge hyo achukuliwe hatua za kinidhamu.
Pia, wamemtaka Mkurugenzi huyo ambaye alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho kuonyesha barua aliyotumiwa na Waziri Simbachawene ya kutoa amri ya kumtoa nje Mbunge huyo.
Mbali na hilo, pia ametoa rai kwa serikali kufuata misingi bora ya uongozi haswa katika kusimamia masuala yanayowahusu wananchi hususani suala la Meya wa Jiji ambalo bado halijafanyika.