CHADEMA yaja na mbinu mpya

CHADEMA yaja na mbinu mpya

mtendaji wa kijiji

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2012
Posts
533
Reaction score
115
Katika harakati za kujenga CHAMA Kuanzia ngazi ya msingi, Kijana Godson Mbaga amekuja na mbinu mpya ya kuhamasisha michezo kwa vijana jimbo la Same magharibi. Zoezi hilo linaendelea kufanyika ambako jana tarehe 27/10/13 Godson Mbaga alipata wasaa wa kuzindua timu ya mpira na kuhutubia halaiki katika kijiji chaGonjanza kata ya suji.

Mbali na uzinduzi huo alipokea wanachama wapya ambao walikula kiapo na kukabidhi kadi 20 Za CCM. Aidha katika hotuba yake alilazimika kuwapa nafasi wazee walioonekana kuwa na hamasa ya kutaka kuongea. katika maelezo yake mzee Emanuel Nziacharo miaka 80 akiwakilisha wazee wengine alisema "tumechoshwa na mbunge aliyepo sasa (David Mathayo) ambaye amekua akirubuni wazee kwa kuwapa sukari kg 2 na miche ya sabuni, akishindwa kutatua kero za muda mrefu ambazo zitatufanya tumkumbuke hata akiachia kiti, alisema hivi sasa kunashida kubwa ya maji, ndoo imefikia sh 500 lakini kwa dharau zake anakuja kugawa sukari hivi itatusaidia nini??? (alihoji mzeeemanuel)"

Hivyo basi wazee kwa sauti moja walimtaka Godson Mbaga Kuto kukata tamaa katika kuwapigania wana same magharibi na wamemuahidi kumpa ushirikiano 100% kwani wanasema hajawahi kujitokeza kijana mwingine wa aina yake.

Aidha katika harakati zake alipofika makanya alisikitishwa na alichokifanya Mbunge wa ccm David Mathayo Kugawa tende na sukari huku akishindwa kugundua matatizo ya msingi ya wananchi alisema "Huyu mgawa tende mwoneeni huruma amesha choka na anaonyesha dhahiri kuwa kejeli"

Kijana Godson Mbaga amekua akijitolea kwa dhati kuzunguka kwa miguu, baiskeli hata bodaboda kuhakikisha kwamba anafika kila kijiji na kitongoji Same magharibi Hii imewafurahisha sana wazee wa same magharibi na kumuona kama Mkombozi wao 2015. Godson amewaahidi wana same kua ata pambana kwa namna yoyote ile kuhakikisha kuwa dharau na kejeli za CCM Zinakwisha 2015 atakapo pata nafasi ya ubunge endepo CHAMA kitampa ridhaa.

Katika ratiba ya leo 28/10/13 Kijana Godson atakuwa NKWINI na SAWENI
29/10/13 ATAKUWA RUVU na tarehe 30/10/13 atakuwa mbakweni, tarehe 1/11/2013


kwa mawasiliano +255752225501
 

Attachments

  • DSC00564.JPG
    DSC00564.JPG
    49.6 KB · Views: 329
  • DSC00598.JPG
    DSC00598.JPG
    50.7 KB · Views: 367
  • DSC00612.JPG
    DSC00612.JPG
    47.6 KB · Views: 296
  • DSC00610.JPG
    DSC00610.JPG
    48.7 KB · Views: 301
Hongera kwa kutoa elimu ya uraia siyo kitoa kitu cha kumsaidia mtu kwa muda badala kusaidia jamii kuondokana na umasikini uliotanda hasa vijijini.
 
Hongera kwa kuwafundisha watu kuvua samaki sio kuwapa samaki ubarikiwe
 
I salute u Kamanda Mbaga...Mungu akubariki na aendelee kukupa moyo wa namna hiyo,Mana Geografia y kule kwetu na Mguu,Baisekeli kaz kweli kweli aluta Kontinyua kka!!!Kaza NGUMI mkuu
 
Wananchi wakikataa sukari kilo mbili na miche ya sabuni aaah David mathayo kwisha habari yake,kamanda kanyaga kwa saana.
 
Back
Top Bottom