CHADEMA yailiza CCM Igunga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yailiza CCM Igunga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Karikenye, Aug 22, 2012.

 1. Karikenye

  Karikenye JF-Expert Member

  #1
  Aug 22, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  CHADEMA yailiza CCM Igunga

  • Rais Mkapa, Dk. Magufuli, Wasira wamponza Kafumu

  na Ramadhani Siwayombe na Irene Mark


  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimepata pigo jingine baada ya Mahakama Kuu ya Kanda ya Tabora kumvua ubunge, Dk. Peter Kafumu, aliyekuwa Mbunge wa Igunga.Kafumu ambaye anakuwa mbunge wa kwanza kukaa muda mfupi madarakani, alivuliwa ubunge jana baada ya mahakama kuthibitisha masipo shaka kwamba taratibu za uchaguzi mdogo uliomwingiza madarakani zilikiukwa.

  Mlalamikaji katika kesi hiyo alikuwa Joseph Kashindye ambaye alikuwa mgombea wa kiti hicho kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).Kashinde alifungua kesi dhidi ya Kafumu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo hilo.
  Akisoma hukumu ya kesi hiyo katika Mahakama ya Wilaya mjini Nzega jana, Jaji wa Mahakama Kuu, Marry Shangali alitaja vipengele sita alivyotumia kutengua matokeo ya ubunge wa Dk. Kafumu.

  Vipengele hivyo ni pamoja na matukio yaliyojitokeza wakati wa kampeni za uchaguzi huo ambapo ni kutolewa kwa ahadi ya kutojengwa daraja kama hatachaguliwa Kafumu.Jaji Shangali alisema ahadi hiyo ilikiuka mwenendo wa kampeni za uchaguzi.Aidha, Jaji Shangali alisema pia kitendo kilichofanywa na upande wa walalamikiwa cha kwenda kutembelea hospitali na kutoa misaada mbalimbali kilikiuka taratibu na hivyo kuathiri zoezi zima la uchaguzi huo.

  Kipengele kingine alichokitaja kukiuka taratibu za uchaguzi ni pamoja na kitendo cha ugawaji mahindi ya msaada siku chache kabla ya upigaji kura katika jimbo hilo la Igunga na hivyo kuwafanya wananchi kupiga kura kutokana na ushawishi wa misaada hiyo.
  Pia kupanda katika majukwaa ya kampeni kwa Mbunge wa Jimbo la Tabora Mjini, Ismail Aden Rage (CCM) akiwa amening'iniza silaha kiunoni nako kuliathiri mwenendo mzima wa uchaguzi huo.

  Kutokana na sababu hizo na maelezo mbalimbali ya upande wa mashahidi wa pande zote mbili, mahakama imeridhia na kuamua kutengua matokeo ya ubunge wa jimbo hilo na kuwataka washtakiwa kulipa gharama zote za kesi hiyo.CHADEMA katika kesi hiyo iliwakilishwa na mwanasheria Profesa Abdallah Safari.Wakati wa utetezi wake, Profesa Safari aliwasilisha hoja 15 za kupinga ushindi wa Dk. Kafumu ikiwemo ya Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli kufanya mkutano wa kampeni katika Kata ya Igulubi wilayani Igunga akitumia madaraka yake kuahidi ujenzi wa Daraja la Mbutu kama wananchi hao watampigia kura Dk. Kafumu.

  Pia Safari alidai kuwa waziri huyo aliwatisha wananchi wa kata hiyo kwamba wasipoichagua CCM daraja hilo halitajengwa na kwamba pia watashughulikiwa.

  Profesa Safari alidai Baraza la Waislamu (BAKWATA) Wilaya ya Igunga liliwakataza waumini wasiipigie kura CHADEMA na kwamba naye Rais mstaafu, Benjamini Mkapa alitoa ahadi ya kugawa mahindi kwa wananchi wa Igunga siku moja kabla uchaguzi ili waichague CCM.Hukumu hiyo iliamsha shangwe na nderemo kutoka kwa mashabiki wa CHADEMA ambao walifurika mahakamani hapo kusikiliza hukumu hiyo.

  Akitoa maoni yake kuhusiana na kuanguka kwake, Dk Kafumu alisema jaji hakuwasikiliza vizuri na alionesha kushangazwa na jinsi alivyokubaliana na hoja za CHADEMA alizodai kuwa zilikuwa za kusadikika.

  "Sijapenda sana jambo lilivyotokea huku… wakati wa kampeni tulikuwa tunanadi sera na Ilani ya CCM. Nakubali kwamba kwa sasa mimi sio mbunge, nitaendelea kuwa mtaalamu wa madini kama ilivyokuwa, usiniulize sijaridhika na siwezi kusema sasa hivi, nitachukua hatua gani kiulize Chama Cha Mapinduzi," alisema Dk. Kafumu.Hata hivyo alisema hajaridhika na uamuzi huo kwani alishawahi kulalamika kwamba hana imani na jaji tangu mapema kwa sababu alikuwa anaegemea upande mmoja na suala la rufaa alitaka kiulizwe chama chake.

  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alipoulizwa msimamo wa chama kuhusu hukumu hiyo, alikuwa mbogo na kusema hana taarifa rasmi za CCM kupoteza ubunge katika jimbo hilo. "Nimesema hivi, taarifa ikishafika tutazungumzia, chama kina mtandao wa kupokea taarifa zake, kama wewe hujanielewa Watanzania wamenielewa, usinilazimishe kusema," alifoka Nape.

  Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa alisema kuwa chama chao kimeweka historia nyingine katika siasa za Tanzania.Alisema CHADEMA imekuwa ikiwaonya CCM kuacha kutumia mawaziri kutoa ahadi kama za kugawa mahindi na mambo mengine kwani kufanya hivyo ni kinyume na kanuni za uchaguzi.Alitamba kuwa CHADEMA ina uhakika wa kutwaa jimbo hilo kwani mara ya kwanza CCM walitumia hila kama hizo zilizowaangusha mahakamani.

  Katika uchaguzi mdogo uliofanyika katika jimbo hilo, Dk. Kafumu alishinda kwa kupata kura 26,000 dhidi ya mgombea wa CHADEMA aliyepata kura 23,000.
   
 2. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #2
  Aug 22, 2012
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Huyu Jaji aliteuliwa kutokana na weledi bila shaka yoyote, anafanya kazi kutokana na uelewa na maamuzi yake ni huru, natamani ndiye angekuwa Jaji katika kesi ya kupinga uchaguzi jimbo la segerea na Arusha mjini. Nakuombea afya njema Jaji Maria.
   
 3. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #3
  Aug 22, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,142
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  iseje kuwa kwa kuwa tumeshinda kesi!!!!!!!!!!!!
   
 4. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #4
  Aug 22, 2012
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  La! Watu wengi wanadhani kushinda kesi ndio kutendewa haki, hata kushindwa kesi ni kutendewa haki pia ili mradi haki ionekane kweli imetendeka. Ili uchaguzi uwe batili au kwenda kinyume cha sheria ni lazima uwe batili kisheria. Uchaguzi unatakiwa uwe huru na wa haki. Suala la kutumia rasilimali za serikali kufanyia kampeni za kisiasa ni batili kisheria, rejea Kesi ya Joseph Sinde Warioba vs Stephen Wasira. Nadhani utakumbuka kwamba serikali ilihamishia kazi zake Igunga wakati wa kampeni, na kwamba mawaziri wanaoheshimika katika serikali walitumika kukampeni, hiyo ni kinyume na taratibu za uchaguzi. Pia baadhi ya mashahidi wa utetezi walikubali kwa namna moja au nyingine kuhusika na vitendo vinavyokiuka maadili ya uchaguzi mfano, Rage. Mashahidi muhimu kama Mh. Mkapa n a Mh. Magufuli hawakutokea mahakamani kuisaidia mahakama. On my opinion judgement was fair and justy.
   
 5. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #5
  Aug 22, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,351
  Trophy Points: 280
  Hiyo kesi ilikaa vibaya sana kwa upande wa CCM.Jaji makini hawezi lazimisha. Hata wakikata rufaa na kupika matokeo ,bado wapo upande unaolaumiwa na kutoaminika na wananchi.Wananchi kwa sasa hawana sana imani na vitu vya CCM.Siku hizi ni rahisi kusikia hata mwanachama wa CCM akisema "bwana CCM in wataalamu wa,FITNA ,lazima ccm tushinde ".Ni ishara kuwa wanaamini kuwa CCM ina utaalamu wa fitna.Kama ni kumpatia Kafumu ubunge wacheki viti Maalum kama mh Rais hajamaliza slot yake.
   
 6. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #6
  Aug 22, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  safi sana
   
 7. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #7
  Aug 22, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  hii ndo maana ya mtu kuwa mwana taaluma na msomi yoyote hayumbishwi na siasa za kipumbavu
   
 8. PROFESA KYANDO

  PROFESA KYANDO Member

  #8
  Aug 22, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 81
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]CM yapoteza jimbo jingine [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Tuesday, 21 August 2012 20:46 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  [​IMG] Dk Dalaly Peter Kafumu

  MAHAKAMA YATENGUA MATOKEO YA MBUNGE WAKE IGUNGA, CHADEMA WAIBUKA KIDEDEA
  Mustapha Kapalata na Hastin Liyumba, Nzega
  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimepata pigo baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, kutengua matokeo ya ubunge Jimbo la Igunga yaliyompa ushindi mgombea wake, Dk Dalaly Peter Kafumu.Dk Kafumu aliibuka mshindi katika uchaguzi mdogo uliofanyika Oktoba 2, mwaka jana kuziba nafasi ya Rostam Aziz ambaye alijiuzulu kwa madai kwamba anaachana na siasa chafu ndani ya CCM.Uchaguzi huo ulikuwa wa ushindani mkubwa kati ya Dk Kafumu na aliyekuwa mgombea wa Chadema, Joseph Kashindye ambaye hakuridhishwa na mwenendo wa uchaguzi huo, hivyo kuamua kupinga matokeo hayo mahakamani. Kesi hiyo ilifunguliwa Machi 26, mwaka huu.

  Akitoa hukumu hiyo, Jaji Mary Nsimbo Shangali alisema Mahakama ilipokea malalamiko 15 ambayo yaliridhiwa na pande zote mbili, lakini baadaye yakaongezwa madai mengine mawili hivyo kufikia 17.
  "Madai yaliyopokewa na Mahakama ni 17 na kati yake imethibitisha madai saba," alisema Jaji Shangali katika hukumu hiyo.

  Mbali na Dk Kafumu, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya uchaguzi walikuwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Igunga aliyetangaza matokeo hayo.
  Dk Kafumu akizungumza na Radio One jana alisema tangu awali, hakuwa na imani na jaji aliyesikiliza kesi hiyo. Alisema hana mpango wa kukata rufaa, bali anawaachia viongozi wa CCM kufanya hilo.
  Alisema baada ya ubunge wake kutenguliwa, anaendelea na shughuli zake za madini kwa kuwa ni mtaalamu wa sekta hiyo... "Ndugu mwandishi karibu Singida, mimi narudi kuendelea na shughuli zangu za madini."
  Sababu za kutengua matokeo
  Alisema hoja zilizothibitishwa na Mahakama na ambazo zimetumika kutengua matokeo hayo ni pamoja madai kwamba Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli alitumia nafasi yake ya uwaziri kutoa ahadi ya ujenzi wa Daraja la Mbutu ambalo lilikuwa ni moja ya kero kubwa kwa wananchi wa Jimbo la Igunga.

  Dk Magufuli akiwa katika moja ya kampeni za uchaguzi huo, alitumia nafasi ya uwaziri kwa kuwatisha wapigakura wa jimbo hilo kwa kusema kama hawatamchagua mgombea wa CCM, watawekwa ndani.

  Jaji Shangali aliendelea kueleza kuwa Mbunge wa Tabora Mjini, Ismail Aden Rage alitangaza kuwa mgombea wa Chadema alikuwa amejitoa katika uchaguzi huo, jambo ambalo Mahakama imeridhishwa na ushahidi uliokuwa ukitolewa.

  Jaji Shangali alitaja hoja nyingine iliyotumika kufuta matokeo hayo kuwa ni kauli ya Imamu Swaleh Mohamed wa Msikiti wa Ijumaa Igunga, kuwatangazia waumini wa msikiti huo kuwa wasikichague Chadema, kwa kuwa baadhi ya viongozi wake wamemdhalilisha Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatuma Kimario.Alisema hoja nyingine ni Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama kudai kuwa Chadema kilileta makomandoo katika uchaguzi huo na kupanga kuuvuruga.

  Hoja nyingine ambayo Jaji Shangali aliikubali ni ugawaji wa mahindi ya kuwawezesha wakazi wa Igunga kukabiliana na njaa wakati wa uchaguzi huo kwamba ulitumiwa vibaya na baadhi ya wanasiasa kuwashawishi wananchi wawapigie kura.

  Jaji huyo alihoji iwapo wakazi wa Jimbo la Igunga walikuwa na njaa sana wakati wa uchaguzi huo kiasi cha viongozi wa Serikali kuona kuwa ulikuwa wakati mwafaka wa kugawa mahindi hayo.
  Kuhusu hoja ya upande wa utetezi kwamba mgombea wa Chadema, Kashindye alipaswa kupeleka malalamiko hayo Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), alisema siyo ya msingi yanayoweza kumzuia mlalamikaji kupeleka malalamiko hayo katika Mahakama Kuu na hakuna kifungu chochote kinachomzuia mlalamikaji kufanya hivyo.

  Kutokana na hali hiyo, Jaji Shangali alisema kuanzia sasa Jimbo la Igunga lipo wazi na kwamba: "Milango iko wazi kwa walalamikiwa kukata rufaa ikiwa hawajaridhika na uamuzi."

  Hali ya usalama katika mahakama hiyo ilikuwa imeimarishwa, huku wafuasi wa Chadema wakiwa wengi zaidi na wakionekana kuwa na furaha hasa baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo.

  Dk Slaa, Nape wazungumza
  Baada ya hukumu hiyo, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema: "Mahakama imedhihirisha yale ambayo tumekuwa tukisema kila wakati kwamba CCM inatumia mabavu."

  Alisema anashukuru Mahakama kwa kutoa haki na kukubaliana na Chadema kuwa CCM iligawa vyakula kwa wananchi ili kuwashawishi wawapigie kura.

  Pia alisema kwamba imeudhihirishia umma kauli kwamba CCM kinatumia vibaya rasilimali za nchi katika mambo ya siasa akitoa mfano wa mawaziri kuwalazimisha watu wawachague wagombea wao.
  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema alikuwa hana taarifa kuhusu hukumu ya kesi hiyo.
  Hata alipopata taarifa kuhusu matokeo hayo, alisema atakuwa tayari kuyazungumzia pindi akiyapata kutoka katika mfumo wa chama chao."Siwezi kuzungumzia matokeo ya hukumu unayoniambia wewe. Nitakuwa tayari pindi nitakapoyapata rasmi kutoka kule Igunga (CCM)," alisema Nape.

  Uchaguzi
  Oktoba 3 mwaka jana Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Igunga, Magayane Protas alimtangaza Dk Kafumu kushinda ubunge kwa kura 26,484 akifuatiwa na Kashindye ambaye alipata kura 23,260, huku Leopold Mahona wa CUF akipata kura 2,104.

  Ushindi huo wa CCM ulihitimisha mojawapo ya michuano mikali ya kisiasa nchini ambayo Chadema, CUF na CCM vilionekana kufukuzana vikali. Dk Kafumu kabla ya nafasi yake hiyo alikuwa Kamishna wa Madini katika Wizara ya Nishati na Madini.

  Ushindi wa CCM katika jimbo hilo ulikuwa ni pigo kubwa kwa Chadema kwani ulikifanya chama hicho kushindwa kuibuka na ushindi hata katika mazingira ambayo kilitarajiwa au kuonekana kukubalika zaidi. Chaguzi nyingine ambazo Chadema kilidhaniwa kushinda ni zile za Babati, Busanda na Biharamulo ambako kote CCM kilitetea viti vyake.
  Nyongeza na Leon Bahati.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 9. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #9
  Aug 22, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Pigo Takatifu. Washindwe kabisa.
   
 10. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #10
  Aug 22, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,694
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Hii kesi ilikuwa open and close, hakuna cha kujadili hapa.
   
 11. masatujr1985

  masatujr1985 JF-Expert Member

  #11
  Aug 22, 2012
  Joined: Oct 27, 2011
  Messages: 1,933
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  We shall see more
   
Loading...