CHADEMA yaigaragaza CCM uchaguzi wa mwenyekiti wa kijiji Moshi

Malata Junior

JF-Expert Member
Nov 29, 2011
3,104
2,549
Ile kauli maarufu ya Lumumba 'kazi ya Magufuli itaua vyama vya upinzani' ilishindwa kujidhihirisha katika kijiji cha Sambarai jimbo la Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro baada ya mgombea wa CHADEMA kumgaragaza vibaya mgombea wa CCM katika uchaguzi mdogo wa mwenyekiti wa kijiji uliofanyika wiki mbili zilizopita.

Uchaguzi huo ulifanyika baada ya mahakama kutengua ushindi alioupata mgombea wa CHADEMA mwaka 2014 na kuamuru uchaguzi urudiwe kufuatia kesi ya kupinga matokeo iliyofunguliwa na mgombea wa CCM.

Katika uchaguzi huo wa marudio mgombea wa CHADEMA alishinda kwa tofauti ya kura 3000 licha ya mgombea na makada wa CCM kutumia jina la Magufuli kuomba kura.
 
Hongera sana chadema kwa ushindi wa kishindo . Nasikia mmemgalagaza vibaya sana na bado.
 
Hongera sana, na bado huku kwetu mbeya tutaendelea kuwagalagaza tu mpaka washike adabu
 
Mkuu unategemea Chadema watashindwa Moshi wakati ni uwanja wa nyumbani.
Haahaaa ukweli mchungu tu magufuli hawezi itingisha chadema hata mara moja, kwa lipi hasa? Kutumbua majipu aliyoyapaka mafuta mkubwa wake? Hata kidogo, UKAWA wamemiliki Dar nako ni kwa wachaga, mmeishiwa kweli nyie.
 
Back
Top Bottom