Chadema yadai CCM imeanza kucheza rafu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema yadai CCM imeanza kucheza rafu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MziziMkavu, May 22, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).



  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimekishutumu Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa kimeanza mkakati wa kununua shahada za kupigia kura za vijana wanaoonekana kushabikia vyama vya upinzani katika mikoa yote nchini.
  Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu wa chama hicho, Tundu Lissu, alisema jana kuwa viongozi na makada wa chama hicho kuanzia ngazi za mashina na matawi wamekuwa wakikusanya taarifa za wananchi waliojiandikisha karika daftari la kudumu la wapiga kura.
  Alidai kuwa katika kutekeleza mkakati huo, makada hao wa CCM wanashirikiana na maofisa watendaji wa kata na vijiji ambao katika uchaguzi mkuu watakuwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi.
  Alisema Chadema imepata ushahidi unaoonyesha kuwa sensa ya wapiga kura inayofanywa na CCM ni maandalizi ya kuharibu uchaguzi wa mwaka huu kwa kutoa rushwa kwa wapiga kura wenye mwelekeo wa kuviunga mkono vyama vya upinzani.
  Lissu alisema Jumamosi iliyopita, wanachama wa Chadema wa kijiji cha Nkhoiree, kata ya Ihanja Jimbo jipya la Singida Magharibi kulimkamata kada mmoja wa CCM akiwa katika zoezi la kuchukua taarifa za wapiga kura.
  Alisema katika purukushani za kumkamata, kada huyo alifanikiwa kukimbia na kutoroka, lakini wanachama na wafuasi wa Chadema walifanikiwa kukamata nyaraka alizokuwa nazo.
  Alisema nyaraka alizokamatwa nazo ni muhtasari wa kikao cha CCM kata ya Ihanja ambayo inawataja pia Mwenyekiti wa kata na Katibu wa kata hiyo ya Ihanja.
  Lissu alisema ajenda namba 5 ya muhtasari huo inahusu maazimio ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa inayoelekeza makatibu wote wa matawi yote ya CCM wafanye sensa ya wapiga kura wote wa vyama vya upinzani kujua wako wangapi hasa vijana wa rika la kati ili kupata idadi yao Tanzania nzima.
  Hata hivyo, Mkurugenzi wa Kitengo cha Propaganda cha CCM, Tambwe Hizza, alipoulizwa alisema hizo ni taarifa za uongo kwani CCM inachofanya ni kuhakiki wanachama wake na si kuhangaika na wapinzani.
  Alisema zoezi hilo ni la kawaida na limekuwa likifanyika miaka mingi iliyopita hivyo hakuna kitu kipya.
  Alisema wanachofanya sasa ni kuhakikisha kila mwanachama wa chama hicho amejiandikisha katika daftari la wapiga kura.
  “Tunahakikisha kila mwanachama wetu anajiandikisha katika daftari la wapiga kura ili siku ya uchaguzi apige kura na ambaye hatafanya hivyo hataruhusiwa kupiga kura za maoni ndani ya chama,” alisema Tambwe.



  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #2
  May 22, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kabisa hawa jamaa wameanza kazi hii muda mrefi kidogo.Hivi Upinzani hatuna cha kufanya zaidi ya kutoa haya matamko?naomba wanaJF tunajadili the best way ya kukabiliana na hili janga,tufanyeje ili hawa wapuuzi wasindelee na huu wizi na ufirauni wanaoufanya.Tuje na mbinu mbadala sio hizi za kulialia kwenye matamko.hawa jamaa ni viziwi wasio na mkalimani wa lugha ya alama au hearing aids hivyo tutakuwa tunapoteza muda tu kwa kutoa haya matamko.
   
 3. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,124
  Trophy Points: 280
  Tundu Lissu ni mwanasheria aliyebobea,je mazingira hayo hayatoshi ku-sue waliofanya hivyo? Huyu mke mdogo wa Makamba nae anachekesha...kwamba mwana CCM hawezi kushiriki kura ya maoni ndani ya chama chake kama hujajiandikisha kwenye DKWK? Kama ni kuhakiki wanachama wake, si matawi yaitishe wanachama wake na kuwaambie waje na vitambulisho vya kupigia kura? Yeye kama alivyo boyfriend wake Makamba,ni kukanusha hata kwa kitu kilicho na ushahidi!! Wito kwa vijana wanaofuatwa kurubuniwa...watakapofuatwa wawalengesha kwa viongozi wa CUF au CHADEMA walio karibu nao.
  I hate these guys!!!!
   
 4. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #4
  May 22, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Kuwafungulia mashtaka ni wazo zuri lakini kumbuka jinsi kesi zinavyochukua muda mrefu hapa kwetu Tanzania..Huku kesi zinaendela wengine wataendelea kufanya maasi yao.
   
 5. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #5
  May 22, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kulalamika si suluhisho la matatizo,kama wao wananunua na nyie toeni mapesa hata kwangu njooni mchukue!Sasa kelele za nini?Mimi yangu nauza kwa Tshs.20,000,000/-mkiwa tayari leteni mafweza!
   
 6. Lighondi

  Lighondi JF-Expert Member

  #6
  May 22, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 585
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mimi ninatoka discount kidogo. Sina bei sana kama Pengo, Elfu 17 tu naachia mzigo. Heeeee, mnashangaa nini Ndio mtaji pekee niliobakia nao sasa nifanyeje na uchaguzi ndio huu. Nikichemsha hapa hadi 2015!!!!!!!!!!!!!!!!
   
Loading...