Hali ya CHADEMA yaanza kuteteleka kata ya Mbezi baada ya mapandikizi ya CCM na ACT ndani ya CDM kuanza kubungua taratibu. Mamluki hao wakiongozwa na Makweta kufurukuta hadi kupata uenyekiti chama wa mtaa Makabe.
Nafasi ya mwenyekiti ameipata baada ya kuendesha na kupiga majungu yaliyomlazimisha mwenyekiti aliyekuwepo kujiuzulu ndugu Munuo.
Makweta na kundi lake wamefanikiwa kuuweka mfukoni uongozi wa chadema Kata ya Mbezi Luis na Jimbo la Ubungo. Uongozi wote wa Chadema Jimbo na kata kwa sasa wanacheza ngoma inayopigwa na Makweta.
Kwa sasa, katiba imekuwa ikivunjwa wazi wazi ili mradi Makweta na mamluki wenzake wafanikishe malengo yao. Lengo mojawapo,ni kuhakikisha wanapandikiza watu wao kwenye ngazi za juu za chama katka kata ya Mbezi Luis. Hadi sasa wamelazimisha uchaguzi ndani ya chama urudiwe kwa kujaza nafasi zote. Wamelazimisha kufanya uchaguzi wa kujaza nafasi za wazi ngazi ya tawi na kuwaondoa hata viongozi waliopo na waliochaguliwa mwaka jana.
Jambo lisiloeleweka ni pale ambapo viongozi wa kata na jimbo wanaendesha chaguzi zilizoamriwa na Makweta; huku wakijua dhahiri kwamba baadhi ya nafasi zinazoitiwa uchaguzi zina viongozi wanaozishikilia tangu uchaguzi uliopita.