Simiyu Yetu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2013
- 18,949
- 4,638
TOFAUTI YA CHADEMA YA KINA ZITO KABWE , KITILA MKUMBO,SAMSONI MWIGAMBA, Dr SLAA NA SAID ARFI VS CHADEMA YA KINA GODBLES LEMA, SUGU, PROF JAY, LOWASA, NA MBOWE.
1. Chadema ya kina Zito na Dr Slaa adui yao mkubwa alikuwa ni mtu fisadi. Chadema ndio waanzilishi wa kutaja watu mafisadi hadharani. Kupitia waraka wao wa "List of Shame" waliwataja mafisadi papa wa Tanzania na Lowassa akiwa mmoja wao.
Chadema hii ya kina Lowassa hawataki mafisadi watajwe hadharani. Chadema hii ina huruma sana kwa mafisadi wanataka waandikiwe barua za siri kuelezwa kuwa wao ni mafisadi. Lowassa hadi leo hajawahi kuwashtaki kina Slaa kwa kuwa walimtaja hadharani kwa hiyo Tanzania ilithibitisha kuwa yeye ni fisadi.
Kitendo hiki cha chadema hii chini ya mbowe na Lowassa kutokutaka Magufuli kutumbua majipu hadharani kinanikumbusha Nadharia ya Inductive resoning ( To Draw conclusion from particular to general) Lowassa ni fisadi, Lowassa yupo chadema, hivyo chadema wote ni mafisadi na hawataki wengine waguswe.
2. Chadema ya kina Zito ilipigania maendeleo yaonekane jimboni. Slaa alikuwa akizunguka nchi mzima kuamsha wananchi kupata elimu ya Uraia.
Chadema ya sasa ya kina Mbowe wanakwenda Dodoma badala ya kujadili bajeti za maendeleo ya wananchi wao wanalilia waonekane kwenye Runinga. Kuna uhusiano gani kati ya bajeti ya maendeleo na runinga??
Watanzania wanataka maendeleo yaonekane majimboni si kuona waliolala na kufanya vurugu bungeni.
3. Chadema ya kina zito walijua kabisa sheria hutafsiriwa Mahakani na si bungeni. Ndio maana hata yeye aliposhindwana na chadema alikwenda mahakani.
Juzi Mbowe anataka tafsiri za sheria zijadiliwe bungeni.
Mh Chenge juzi kawakumbusha kuwa kazi ya Bunge ni kutunga sheria na si kujadili sheria kusikia hivyo Akaamua kutoka njee.
Ule waraka wa mabadiliko walioandika kitila, samson na Zito walisema maneno haya " ni kwa bahati tu Ccm inawapa chadema matukio ya kuongelea ila kama hayapo hayo matukio chadema haina cha kuongelea" kwa tafsiri rahisi chama hiki kinategemea matukio ili kujiendesha.
Kinachonifurahisha ni kila jipu linalotumbuliwa vilio vya maumivu vinatokea huko chadema. Tafsir yake ni kuwa mzizi wa haya majipu upo huko chadema hahaaaa. Tunaoelewa tunajua ccm inachokifanya kila likibinywa tu utasikia kilio kikitokea ufipani.