Chadema wote na watanzania wazalendo wote popote mlipo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema wote na watanzania wazalendo wote popote mlipo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JATELO1, Jul 27, 2012.

 1. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #1
  Jul 27, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  WANA-JF;
  Nimelazika kuwaandikia hasa ndugu mwanachama au mshabiki wa CHADEMA na watanzania wazalendo wenye mapenzi mema na nchi yetu popote mlipo ili niwafahamishe yafuatayo;

  1. Hakuna binadamu mkamilifu. Katika siku za hivi karibuni Mh. Zitto Kabwe amekumbwa na mambo mengi ambayo kwa kiasi fulani yamesababisha wana-CHADEMA bila kujua kwamba ni njama za CCM za kutaka kuwaruga wao, nao wameingia mkenge na kuanza kushambulia viongozi wao hasa Zitto Kabwe. Narudia kusema kwamba kuhusu kilichotokea kigoma kati ya Zitto, Mwananchi, na Wabunge wengine haikuwa kitu kizuri na ndiyo maana sote tulilikemea. Hivyo, naamini Zitto kama kijana mwenzetu alisikia na atajirekebisha baada ya kuona kwamba kuna vitu anafanya ambavyo havijengi chama na badala yake anachangia kuchelewesha ukombozi wa Watanzania. Pamoja na hayo bado tuna imani kwamba Mh. Zitto ataweza kujifunza na kuendelea na ujenzi wa Taifa letu kupitia CHADEMA, kwani kuteleza siyo kuanguka. Hivyo nitoe wito kwa wazalendo wenzangu, TUACHE sasa kuendelea kufanya kazi ya NAPE na kitengo chake cha CCM cha Propaganda, ambacho kinafanya kazi ya kutakakuwagawa WANACHADEMA.

  2. Kama kumbukumbu zetu ziko sawa tunaweza kukumbuka kauli ya Wasira kwamba CHADEMA itakufa ndani ya mwaka moja. Je, mmewahi kupata muda na kufikiria ni namna gani chama kinaweza kufa? kama hamjafanya hivyo, basi nyinyi wenyewe wanachama mmeamua kuua chama chenu na sasa mnaona kwamba wabunge wa CCM kumsafisha Lowassa ni sahihi na hamuonekani kukemea na badala yake mmeendelea kushambuliana nyinyi kwa nyinyi na kusahau ile approach ya wakoloni ya Divide and Rule.

  3. Sawa, kuna wabunge wantuhumiwa kuomba rushwa TANESCO na wengi wao ni CCM, lkn sasa nyinyi bila kuchunguza na wala kuwa na uhakika mmeamua kufanya kazi ya kitengo cha Propaganda ya CCM bila kujua hilo. Hivi mnashindwa kujiuliza swali mmoja dogo tu kwamba mbona katika hizi mada za kuparuruana nyinyi kwa nyinyi wana-CHADEMA, watu kama kina Nape, Mwigulu (Burn Kurudi), na wote wanaolipwa na Nape kwa ajili ya kazi ya Propaganda hapa JF kama Zomba, Ritz, Mama Porojo, n.k, hawaonekani kuchangia chochote? Jibu ni rahisi tu, kwamba Wanachadema wanatimiza unabii wa Wasira wao kwa wao, bila hata ya kutafakari nini madhara ya hiki wanachofanya kwenye ujenzi na utengamano wa chama.

  4 Je hamjiulizi hata swali moja tu kwamba, iweje leo Mh. Zitto kuhisiwa tu kwenye hilo sakta la TANESCO wakati Mh. Sendeka na wenzake wametajwa moja kwa moja lkn hakuna anayewashambulia hao wengine na badala yake ni Zitto ndiyo anashambuliwa sana? Je mmechunguza ni lini hawa wanaoanzisha mada zinazohusu Zitto na CHADEMA wamejiunga hapa JF? ukiangalia na kufuatilia wengi wao wana ID mpya, hivyo hilo inawezekana ikawa ni strategy ya watu fulani kutimiza kile walichoelekezwa na kitengo cha propaganda cha CCM chini ya Nape.

  Mwisho naomba niseme kwamba, mimi ni kati ya watu wanaochukia ubadhirifu wowote na hata kauli za kiunafiki zenye malengo ya kuwadhoofisha watu katika ukombozi wao. Lkn pia naamini kwamba watu wana mapungufu, hivyo yawezekana Mh. Zitto naye ana mapungufu (ni kweli anayo), lkn wito wangu kwenu WANACHADEMA wote na WATANZANIA WAZALENDO WOTE popote mlipo, tusiingie kwenye mtego wa CCM wa divide and rule, na badala yake tuelekeze nguvu katika kujenga chama imara na kuwasidia viongozi wetu akiwemo Zitto ili tukakomboe nchi yetu kwa pamoja. Ukombozi wa Watanzania uko mkononi mwa CHADEMA, WANACHAMA WA CHADEMA, na WATANZANIA wazalendo wote. Na hili litawezekana tu iwapo hatutakuwa tayari kufanya kazi ya NAPE NA CCM. Nawaomba sana wazalendo wenzangu, tuamke sote na tuache kufanya kazi ya CCM, kwani CCM ilishajichokea lkn haiko tayari kuondoka madarakani.

  Nawasilisha wadau.
  TELO.
   
 2. a

  andrews JF-Expert Member

  #2
  Jul 27, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ​maelezo mazuri sana lakini kamati kuu ya chadema ni makini haiyumbishwi na michezo michafu ya ccm dhaifu
   
 3. Nyetk

  Nyetk JF-Expert Member

  #3
  Jul 27, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 1,624
  Likes Received: 819
  Trophy Points: 280
  Amekuahidi mgawo wa mihela ya mafisadi wa TANESCO, au?
   
 4. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #4
  Jul 27, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Mimi sihongeki lkn sipendi kuona propaganda za CCM zikitugawa sisi wazalendo.
   
 5. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #5
  Jul 27, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Ni vizuri lkn hata sisi tunawajibika kuwakemea hawa watu wanaotaka kutuvuruga.
   
 6. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #6
  Jul 27, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni zito mwenyewe,
  anazo platform nyingi sana za kulisemea jambo hili positively,
  lakini anachagua njia ya kumtuma Pasco kututhibitishia upuuzi tusioutaka kanakwamba yeye (zito) ni presidential material. Tunaunganisha dot ndugu yangu. Kale ka kijeba kenye domo chapati hakakunji kalianza wakati wa definition ya kambi ya upinzani bungeni, likatokea zengwe kwenye chama chake mbatia akakaweka kwenye kona (akachukua kadi)
  hatujakaa sawa kanabwatuka next presida lazima atoke kg, hapo hapo zito anajinasibu kiutovu wa nidhamu, tena kwa makusudi akijua kufanya hivyo kutaleta negative debate kwenye chama chake kuwa ana sifa za kuwa rais wa tz, sasa kama si zito wako katumwa na wasira hapo unataka kutushawishi nini! Kajipangeni, zitto si wa kumuamini tena kwenye historia ya tz. Anaweza kuwauzeni nyinyi kaka na dada zake kwa slesi ya mkate!!!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #7
  Jul 27, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  nafarijika anapotokea mzalendo kama wewe (kama ni kweli wewe siyo gamba na hapa uko kazini, ndiyo maana haujaelewa thread yangu) anayeumia kwa matendo ya Zitto, ungeelewa lengo la thread yangu wala usingeona tofauti yoyote kati yangu na hicho ulichokusudia kuiwasilisha (iwapo tu wewe siyo gamba na mchumia tumbo wa CCM). Mimi niliangalia madhara ya mijadala na thread nyingi zinazoanzishwa kama ***** hapa JF kwa jina la Zitto na CHADEMA, ndiyo maana nimependekeza mjadala wowote unaohusu Zitto unaletwa humu na watu maalumu na kwa kazi maalumu na wametumwa na kitengo cha Propaganda cha CCM chini ya Nape, ndiyo maaana nimewaomba wanachadema na watanzania wazalendo wayapuuzie ili umoja wetu uendelee na kamwe tusikubali kufanya kazi ya Nape na Wasira, bali tupige mbio kuelekea ukombozi wa nchi yetu.
   
 8. B

  Bob G JF Bronze Member

  #8
  Jul 28, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  ZZK anasemwa kwakuwa haikutegemewa ZZK ahusishwe na tuhuma za Rushwa, hawawezi kusemwa wabunge wa ccm ni kwa sababu % kubwa ya watu wa ccm wamehusishwa na Ruswha na Ufisadi wa kila namna haishangazi wala kuwashitua watu ndo kazi yao kupora,kuiba,Rushwa na si CDM
   
 9. GreenCity

  GreenCity JF-Expert Member

  #9
  Jul 28, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 4,662
  Likes Received: 2,115
  Trophy Points: 280
  Kweli mkuu umenigusa! Sitachangia tena thread zinazokuja kwa jina la CHADEMA NA ZITTO zilizo na elements za mtindo huu. Bali naanza kuwakumbusha wachangiaji kwamba kuna watu wametumwa kutucorrupt mind zetu. NAIPENDA CHADEMA.
   
 10. Uncle Rukus

  Uncle Rukus JF-Expert Member

  #10
  Jul 28, 2012
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 2,430
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Zitto hana mda wakujirekeisha maana anachokifanya ni sahihi, anafanya kazi aliyotumwa.
   
 11. SONGOKA

  SONGOKA JF-Expert Member

  #11
  Jul 28, 2012
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 1,710
  Likes Received: 877
  Trophy Points: 280
  Mkuu telo
  kama mwana chadema mwenzio nimefurahishwa na moyo wako wa kizalendo lakini nasikitika kuwa umeshinwa kutoa suluhu ya tatizo mbali ya maelekezo ya ujumla.kama nilivyo shade na red apo, ntajikita katika hayo mambo,lakini kabla ya yote nakuhakikishia mimi ni mwana chadema.

  1;Zito ana mapungufu: ni kweli kwamba kila mwanadamu ana mapungufu haijarishi haiba au karama aliyonayo lakini mapungufu ya zito ni ya makusudi na yanamalengo HASI katika chama kwa ujumla,kila zito anapoibuka na icho unachoita mapungufu husababisha matatizo makubwa sana kwa wanachama au chama chenyewe,ntatoa mifano michache
  Wakati tukiwa busy kwenye kampeni arumeru zito akatoa waraka kuwa anafaa kua raisi na atagombea,haukua muda muafaka kabisa, wakati wapinzani wakiishinikiza serikali kuachana na muswaada wa kununua mitumba na mambo ya kifisadi zito akaibuka kusapoti majenereta ya dowans(ile kampuni ya fisadi rostam)wakati chadema ikijenga chama na kusisitiza umoja zito aliibuka kutaka uenyekiti akiwa na kafulila,wakati muheshimiwa nasali anakanusha zito anakuja na tungo tata, SASA haya ni mapungufu au makusudi for any man with reasonable personality and state of mind same as zito we expect him to act in good faith and accountable to any action or statement soforth from him.

  2.Kujenga chama Imara: Chama imara kinajengwa kwa nidhamu na misingi yenye lengo moja,SASA hatuwezi kujenga chama imara kwa kunyamazia uozo wa kiongozi wetu ambaye anaonyesha marengo tofauti ETI kwa sababu tu NAPE atashangilia..HUU utaratibu ndo uliiiua CCM.Kuna bwana mmoja alitoka ulaya na degree kama nane ivi enzi za mwalimu,Nyerere kwa heshima kubwa akamuuliza huyu mtaaramu "tukupe kitengo gani kwa huu ujuzi wako ili uweze kuisaidia hii nchi" lakini kwa sababu alikua na uchu wa madaraka kama ZITO ,akasema anataka URAISI.Busara iliyotumika nina uhakika ushawai kuisikia, Sasa kiongozi gani asiyeeshimu misingi na taratibu za chama,hatujafika katika mchakato wa uraisi katika ngazi ya chama yeye anakurupuka tuu,tunakemea mafisadi yeye ana kula nao dinner, zito si chadema na wakati chama kinaanzishwa hakuwa chadema kwaiyo asifikiri bila yeye mambo hayawezekani

  Naomba kupingana na wewe na kuchukua nafasi hii kuuuomba uongozi wa juu wa chadema na wanachama wote kumchukulia zito hatua za kinidhamu kabla hajatuharibia harakati zetu za KUCHUKUA NCHI 2015.nahisi huu ndo mpango wake
  na kama wewe TELO ni zito zuberi kabwe basi jipange na jirekebishe haraka iwezekanavyo
   
 12. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #12
  Jul 28, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  uzalendo wako uko kwa zito na si kwa nchi hii, Zito mwacheni amtetee mhando maana si mara ya kwanza kwa Zito kuvuta kitu kikubwa kutoka kwa mafisadi,
   
 13. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #13
  Jul 28, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Good analysis.
   
 14. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #14
  Jul 28, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,744
  Likes Received: 12,822
  Trophy Points: 280
  Sisi tunamkemea zitto kwa sababu cdm ni chama safi hatuwezi kunyamaza eti kwa sababu ni mwanachama mwenzetu! Hii haikubaliki. Hatuwezi kunyamaza!

  Mbona yeye mwenyewe hata kukanusha ana kanusha kiwepesi wepesi tu.
   
 15. mcfm40

  mcfm40 JF-Expert Member

  #15
  Jul 28, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,142
  Likes Received: 1,779
  Trophy Points: 280
  Nashukuru Telo umeleta hili jambo. Yah, haya mambo wanamabadiliko wenzangu tuliyoanzisha ya kuisaidia CCM kazi ya kusambaratisha upinzani hasa Chadema sidhani kama ni jambo jema. Zito tunamuhitaji katika vita hivi vya mabadiliko. Tumkanye na atajirekebisha. Tatizo la Zitto ni kuamini kwamba yeye ni mtu muhimu kuliko wengine Chadema, na Chadema ipo ilipo kwa sababu yake. Ni kweli Zito amefanya kazi kubwa lakini anasahau kwamba vijana tunaipenda Chadema kama Chadema na siyo mtu binafsi. Na tunaipenda Chadema sio kwa sababu ni chadema bali kwa sababu wao ndio walau wanamwelekeo wa kuongoza mabadiliko. Tunaomba basi vijana kama anavosema Telo tuwe makini tusije tukajikwamisha wenyewe. Naamini Zito alishasemwa vya kutosha. Sasa tuachane na mambo ya kujibomoa wenyewe. Tujitajitahidi kumhimiza Dogo Zito awe kitu kimoja na wenzake. Km akiendelea kuwa arogant nadhani atajimaliza tu mwenyewe kisiasa. Na kazi ya kuibana CCM na serikali yake na iendelee. Amen!


   
Loading...