CHADEMA wazidi kuigaragaza CCM Njombe

Joined
Sep 6, 2013
Posts
10
Reaction score
9
Hatimaye CHADEMA wameiangusha tena ccm Njombe mjini. nibaada ya kushinda kesi zote walizo shakiwa na ccm pamoja na OCD wa njombe.

Jana mahakama ya wilaya njombe imefuta kesi zote zilizokuwa zinawakabili viongozi wa CHADEMA NJOMBE.

Kesi hizo ni pamoja na ile iliyofunguliwa na Jar People (Deo Sanga) mbunge ambaye alilalamika kuwa chadema walifanya fujo kwenye mkutano wa ccm wakati wa uchaguzi mdogo wa udiwani mapema february 2014, na pia alilalamika ametishiwa kumwagiwa tindikali. na nyingine ni ile iliyofunguliwa na OCD dhidi ya Emmanuel Masonga akidai alitukanwa --------.

Mahakama iliamua kufuta kesi hizo zote baada ya upande wa mashtaka kushindwa kutoa ushahidi dhidi ya makosa hayo. hayo yalitokea baada ya wakili msomi wa utetezi kutoka makao makuu ya CHADEMA JOHN MALYA kutoa hoja mahakamani hapo. na wakili wa serikali kushindwa kutolea ufafanuzi wa kisheria.




 

Attachments

  • DSC_0079.JPG
    636.3 KB · Views: 2,907
  • DSC_0103.JPG
    591.4 KB · Views: 498
  • DSC_0105.JPG
    637.3 KB · Views: 2,751
hongereni sana na mungu azidi kuwafichua hawa mashetani wakijani
 
ninapoipendea cdm ni hapo tu , hata kesi ndogo lazima MAKAO MAKUU WALETE MTETEZI , ASANTENI SANA VIONGOZI WA CDM .
 
Jambo jema aibu yake ocd.
 
Nyuzi kama hizi huwezi kukuta mapepo ya Lumumba yakisogelea huwa wanahisi kuungua hasa

BACK TANGANYIKA
 
Bravo John Mallya (wakili msomi) kwa kuisimamia haki.Mungu atakulipa.
 
Hongereni sana makamanda. Kazi iliyo mbele yetu ni katiba mpya piga kelele serikali 3 ni lazima
 
Shetani hawezi kutenda wema ila Mungu.Bravo!
 
Nyuzi kama hizi huwezi kukuta mapepo ya Lumumba yakisogelea huwa wanahisi kuungua hasa

BACK TANGANYIKA

Mkuu hawawezi kutokea bado wna mapepo na ukitaka yawapande weka jina la Dk Slaa watakurupuka hao kama yale mapepo yaliuomfata yesu yakamwomba asiyaunguze.
 
inachekesha, chadema siku hizi wanashinda mahakamani ikija kwenye kapu la kura less than 10%. JITATHIMINI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…