MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,982
VIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo na Chama cha Demokrasia na Mendeleo (CHADEMA), nusura wakutane uso kwa uso nyumbani kwa Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere, walipokwenda kuzuru kaburi lake kwenye Kijiji cha Mwitongo, Wilaya ya Butiama, mkoani Mara.
Msafara wa Naibu Katibu Mkuu CHADEMA Bara, Bw. John Mnyika, ndio ulioanza kuwasili kujijini hapo na baada ya kuzuru kaburi, waliondoka na baada ya muda mfupi ukawasili msafara wa ACT ukiongozwa na Kiongozi wa chama hicho, Bw. Zitto Kabwe.
Msafara wa ACT, ulifika kijijini hapo baada ya chama hicho kumaliza ziara ya kukitangaza, kukitambulisha chama na viongozi wake kwenye mikoa mbalimbali nchini.
Akizungumza mara baada ya kuwapokea viongozi wa ACT-Wazalendo, Mzee wa Ukoo wa Burito ambaye pia Mwenyekiti wa Wazee wa Butiama, Jack Nyamwaga, aliwaambia muda mfupi uliopita walikuwepo viongozi wa CHADEMA.
"Baada ya viongozi hao kufika hapa Mwitongo, walisema kuna viongozi wanakuja lakini tusiwape ushirikiano wakidai kama ni suala la kupinga ufisadi, CHADEMA wamelipigia kelele ili kumuenzi Mwalimu Nyerere.
"Kimsingi kila mtu anaruhusiwa kufika hapa Mwitongo katika kaburi la Mwalimu na sisi kama wanafamilia, tunampokea kila mtu lakini si kazi yetu kusema nani aje, nani asije," alisema.
Aliongeza kuwa, viongozi wengi wamekuwa wakimuenzi Mwalimu Nyerere kwa maneno si kwa vitendo...ACT mmeanza vizuri na mtamaliza vizuri, nawatakia kila la heri kama kweli mtamuenzi Mwalimu kwa vitendo," alisema Mzee Nyamwaga.
Kwa upande wake, Bw. Kabwe alisema wao watamuenzi Mwalimu kwa vitendo ndio maana wameweka msingi huo katika sera ya chama chao.
Alisema lengo la kumalizia ziara hiyo kwenye kaburi la Mwalimu Nyerere ni kutokana na kuuenzi mchango wake kwa Taifa na Watanzania ndio maana walianzia ziara yao mkoani Ruvuma ambapo ilikuwa ni kitovu cha vita ya maji maji.
"Tumefika hapa na viongozi wenzangu wa ACT kwa sababu ya kutambua mchango wa Mwalimu kwa Taifa...chama chetu kitayaenzi mambo yote ambayo Mwalimu alikuwa akiyataka na kuyapigania kwa vitendo na Katiba yetu inatamka hivyo," alisema Bw. Kabwe.
Chanzo:Gazeti la Majira.

===============================================
Andrew Nyerere ambaye Mtoto wa Hayati baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, akibadilishana kofia na kuteta jambo na Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe.
Andrew Nyerere alimpa Kofia ya CCM na Zitto Kabwe akampa kofia ya Chama cha ACT-Wazalendo na kuvaa wakati viongozi wa chama hicho walipofanya ziara kijijini Mwitongo Wilayani Butiama
Ujumbe wa ACT-Wazalendo wakiangalia Mawaziri wa Baraza la Mawaziri la mwisho la Mwalimu Nyerere. walipotembelea Makumbusho ya Baba wa Taifa Butiama jana
Zitto Kabwe akimuonyesha Afande Sele picha ya Deng Xiaoping ambaye ni ‘baba wa mabadiliko ya kiuchumi ya China'. Hii ni baada ya kumjadili wakati wakiwa kwenye ziara kabla ya kufika Butiama.