Chadema wavutana mkutanoni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema wavutana mkutanoni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by jamadari, Apr 28, 2010.

 1. jamadari

  jamadari JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2010
  Joined: Feb 13, 2010
  Messages: 295
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  VUTA nikuvute kati ya viongozi waandamizi wa Chadema wilayani Same mkoani Kilimanjaro iliibuka juzi wakati walipolumbana hadharani wakigombea kubaki kwenye kikao cha ushauri cha wilaya hiyo huku kila mmoja akidai kuwa na barua ya mwaliko. Mgogoro huo ulianza wakati katibu wa kikao hicho ambae pia ni mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Juma Idd alipotaka kujua viongozi wa siasa waliofika kwwenye kikao hicho na baadaye kubaini kuwa Chadema iliwakilishwa na watu watatu badala ya wawili. Kutokana na hali hiyo, mkurugenzi huyo aliwataka kukubaliana ili wabaki viongozi wawili ambao wangewakilisha chama. Katibu wa chama hicho kutoka Same Magharibi, Mudy Munandi alidai kuwa yeye ndie anaekaimu nafasi ya katibu wa wilaya baada ya aliyekuwepo kusimamishwa uongozi na viongozi wa chama ngazi ya mkoa. Munandi alisema katibu wa wilaya wa chama hicho, Muhando Mdingi alisimamishwa uongozi na tangu Februari 17 mwaka huu kwa tuhuma za kukihujumu chama na hivyo hakustahili kuhudhuria kikao hicho wala kufanya kazi yoyote inayohusu chama. Akionyesha barua iliyoandikwa na katibu wa mkoa wa Chadema, Basil Lema yenye namba CDM/KIL/2010/37 iliyomtaka Mdingi kutojihusisha na shughuli zozote za kichama kwani lengo lake sio kujenga bali ni kukihujumu chama. Kutokana na malumbano hayo, mkurugenzi huyo aliingilia kati na kusema kuwa chama hicho kilipaswa kutoa taarifa ya maandishi kwa uongozi wa wilaya kama wamefanya mabadiliko ya uongozi ili wilaya iweze kujua viongozi wapya. “Jamani vyama vya siasa mkifanya mabadiliko ya uongozi mnapaswa kunijulisha kama msimamizi wa uchaguzi wa wilaya... mpaka sasa sijapata taarifa ya mabadiko hivyo namtambua Mdingi kama katibu wa wilaya wa Chadema. Sasa nyie nendeni mkajipange upya muandike barua mtoe nakala kwangu ili niweze kujua mabadiliko hayo,” alisema. Alisema taarifa aliyonayo ni kuwa mwenyekiti wa chama hicho ni mgonjwa na atawakilishwa na mwenyekiti wa Same Mangharibi, John Ngowi na kuwa katibu atakuwa Mdingi hivyo Mudy Munandy anapaswa kuondoka katika kikao hicho. http://www.mwananchi.co.tz/habari/5-habari-za-siasa/1067-chadema-wavutana-mkutanoni
   
 2. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #2
  Apr 28, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Mmh
   
Loading...