Chadema waungwe mkono | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema waungwe mkono

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by jigoku, Nov 8, 2011.

 1. j

  jigoku JF-Expert Member

  #1
  Nov 8, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Yanayotokea Arusha yakiongozwa na CDM na kwingineko Tanzania nadhani kuna haja ya kutafakari kwa kina kisha tupate suluhu na kisha tufanye vitendo sasa.Ni miaka mingi sasa kumekuwa na vita dhidi ya haki inayokandamizwa na Vinara CCM kwa kuwa ndio wanaounda serikali na kwa kuwa ndio yenye wabunge wengi katika moja ya muhimili wa dola.Kumekuwa na ufisadi mwingi,dhuluma nyingi na uozo wa kila aina lakini hakuna suluhu.

  Leo yanayotokea Arusha yakiongozwa na CHADEMA ni dhahiri ni mapambano dhidi ya dhuluma,wizi,ufisadi wa kila aina,uonevu,ubakaji wa haki na ukandamizaji,nimekuwa nikiwaza sana mpambano kati ya CCM na CHADEMA unaondelea hapa nchini,na binafsi nadhani wanachokipigania CDM kwenye majukwaa,kule mjengoni Dodoma na sehemu zingine hata humu Jamnvini naona ya ukweli mkubwa na kama tutaendelea kuwa wazungumzaji tu bila vitendo hakika watanzania tulio wengi tutakuwa tumekwisha kwa ujumla wetu bila kujali huyu ni CUF,UDP,CCM wala CDM.
  Hiki kinanifanya nishawishike kukubali kuunga mkono CDM,nashawishika kuwaomba waTZ tuunge mkono harakati zinazoongozwa na CDM.
  1.MADINI
  Tanzania tuna madini mengi sana,moja ya migodi mikubwa ya DHAHABU ni
  *Tulawaka ulioko mkoa wa Kagera
  *Kahama mining(KMCL)
  *Geita Gold mine(GGM)
  *Buzwagi -ulioko katikakti ya mji wa kahama na mji mdogo wa Kagongwa.
  *Nyamongo (North Mara)
  *Resolute ulioko Nzega kwa bwana Kigwangala
  Hii hapo juu ni migodi mikibwa ya dhahabu Tanzania,Nauliza kwa wana JF hii yote inasaidia nini katika maendeleo ya taifa hili?kwa nini bakuli kila siku linatembezwa na mkuu wa kaya?kwa nini hakuna madawati,vifaa vya maabara,nyumba za walimu,hakuna vitabu na mengine mtaongezea,Hospital hakuna dawa wala vifaa vya kutosha...... lakini ngoja nikudokezee sehemu zingine kuliko jaa madini hayo ya dhahabu ili upate uwanja mpana wa kutafakari harakati za chadema na vita dhidi ya serikali ya ccm.
  Kuna migodi midogo midogo ya dhahabu ambayo ni:
  *Mpanda,Nyalugusu,London-Manyoni(Singida),Makongorosi -Chunya.Kolandoto-Shinyanga,Mwamanoni(sina uhakika na jina-nimelisahau jina la kijiji ila mgodi huu uko karibu na kijiiji cha Ukenyenge wilaya ya Kishapu),Isunga ngwanda Nzega,Nyang'wambe na Mikese na bwawa la Mindu yote iko Morogoro.Nachingwea na Igunga mabako hawajaanza kuchimba.N amingine mtaongezea, kama dhahabu ya Tanga
  Hivi migodi mikubwa na midogo inachangia nini kwenye pato la taifa,ina maana hakuna mchango wowote unaopatikana kutoka ktk utajiri huu,je hali ya matatizo ya taifa hili ikoje?je hakuna usiri wa jambo baya hapa ambalo linasababishwa na serikali ya CCM.lakini kama kuna tatizo ni kwa kiasi gani CCM na Serikali yake wameyashughulikia kwa vitendo.

  Jamani hapo juu ilikuwa ni Dhahabu hapa chini nazungumzia madini mengine.
  Almasi iliyoko Shinyanga huko Mwadui,Maganzo,Nyangw'ale(Kahama) na Mwabuku mkoani Mwanza

  Tanzanite-Huko Arusha ambako leo pamekuwa kitovu cha ukandamizaji.
  Je madini ya Gamestone kama Greenntomaline,Bluesphire,moonstone,Rubi ambayo yalisababisha mauaji yaliyotekekelezwa chini ya Zonmbe.
  Kuna Gamestone nyingi tu mkoa wa Tanga,Luangwa kule Lindi,Iringa,Morogoro lakini pia kuna Nikel iko Kabanga-Kibondo mkoani Kigoma,Kuna gas,kuna makaa ya mawe nk
  Ninachojiuliza hapa ni kwanini tusiwaunge mkono CDM kwa yale wanayoyapigania maana ni maslahi ya taifa,hata hili linalotokea Arusha leo chanzo chake kikuu si Lema kunyimwa dhamana bali chanzo kikubwa ni CCM kutokukubali kushindwa jimbo la Arusha ili waendelee kunyonya moja ya rasilimali nilizotaja hapo juu,leo wameapnic wameamua kuwa-remote polisi na mahakama kwa faida za kisiasa kwanini huwa wanakuwa wazito kushughulikia wala rushwa,mafisadi na wabadhilifu wengine?
  Nasema kuwaunga mkono chadema kwa vitendo kwa kuwa ukombozi wa Taifa hili si tu kudhibiti madini ni pamoja na kulinda haki za raia na kuwa na mfumo unaojali maslahi ya umma.kama kungekuwa na uwajibikaji na kwa wananchi wa nchi hii sidhani kama kungelikuwa na kelele,lakini ni kinyume kabisa,ufisadi wa kila aina na dhuluma za kila aina hatuwezi kuendelea kuvumilia,tuungane kuutokomeza ushetani huu,tena tuungane kwa vitendo hawa si wa kuwaomba ni kwa nguvu ya umma tu!
  Nawasilisha!
   
 2. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #2
  Nov 8, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu umesahau Liganga na Mchuchuma. Achilia mbali Mbuga za wanyama
   
 3. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #3
  Nov 8, 2011
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kwa hakika umenena maneno ambayo kila mtanzania mwenye kuitakia maendeleo atakuunga mkono,tuanze kuunga mkono kwa matendo sasa baada ya kuwa wazungumzaji sana kwa maandishi na maneno.
   
 4. the grate

  the grate JF-Expert Member

  #4
  Nov 8, 2011
  Joined: Sep 24, 2011
  Messages: 205
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pamoja sana mkubwa
   
Loading...