CHADEMA wapokea msaada wa milioni 400

engmtolera

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
5,149
Reaction score
1,441
Chanzo; http://http://www.cloudsfm.co/profiles/blogs/chadema-wapokea-msaada-wa-milioni-400

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimepokea msaada wa fedha shilingi milioni 400 kutoka Chama cha Upinzani nchini Denmark cha Conservative People's Party (CPP), kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa kuwajengea uwezo vijana pamoja na Wanawake Viongozi wa chama hicho.

Akizungumza wakati wa kutiliana saini Mkataba wa utekelezaji wa Mradi huo, Katibu Mkuu wa CHADEMA, DK. WILBROAD SLAA amesema awamu ya kwanza ya utekelezaji wa Mradi wa kuwajengea uwezo Wanachama wake kupitia Baraza la Vijana la Chama hicho, (BAVICHA), pamoja na lile la Wanawake (BAWACHA), inatarajiwa kuanza Machi, mwaka huu.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Chama cha Conservative People's Party (CPP), ROLF AAGAARD, anaelezea lengo la chama hicho kutoa msaada huo.

Nae Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (CHADEMA), JOHN HECHE amesema msaada huo utawawezesha kutoa mafunzo kwa Viongozi wa Baraza hilo katika mikoa mbalimbali nchini.

Chama cha Conservative People's Party (CPP), kilianzishwa mwaka 1915 na kimekuwa madarakani kwa kipindi kirefu hadi kiliposhindwa katika Uchaguzi Mkuu uliopita nchini.

Chanzo; http://http://www.cloudsfm.co/profiles/blogs/chadema-wapokea-msaada-wa-milioni-400

http://http://www.cloudsfm.co/profiles/blogs/chadema-wapokea-msaada-wa-milioni-400
 
Matumizi yake yamewekwa bayana hapo juu,hilo ulilolitaja wewe ni lako na kumbuka wameingia mkataba,mkataba ambao watatakiwa kuweka wazi matumizi ya pesa hiyo na nadhani haiwezekani wakafanya kinyume na mkataba waliousaini.
 
matumizi yake yamewekwa bayana hapo juu,hilo ulilolitaja wewe ni lako na kumbuka wameingia mkataba,mkataba ambao watatakiwa kuweka wazi matumizi ya pesa hiyo na nadhani haiwezekani wakafanya kinyume na mkataba waliousaini.

acha umbumbu kijana, Sabodo ametoa msaada mara ngapi wakawekeana mkataba?
Umeona zilipoelekea?

Haya sabado alitoa millon 400 kujenga chuo cha kilelea viongozi na vijana wa CHADEMA pale kibaha ..fedha zilitolewa mwaka 2010 hicho chuo umekiona?
 
Matumizi yake yamewekwa bayana hapo juu,hilo ulilolitaja wewe ni lako na kumbuka wameingia mkataba,mkataba ambao watatakiwa kuweka wazi matumizi ya pesa hiyo na nadhani haiwezekani wakafanya kinyume na mkataba waliousaini.

Kukopeshana hakutakuwapo mana hata ruzuku ina mikataba ake as sheria na bado mko mnagawana kama kawa.
 
acha umbumbu kijana,sabodo ametoa msaada mara ngapi wakawekeana mkataba?
Umeona zilipoelekea?

Haya sabado alitoa millon 400 kujenga chuo cha kilelea viongozi na vijana wa chadema pale kibaha ..fedha zilitolewa mwaka 2010 hicho chuo umekiona?
Nakubaliana nawe kuwa mie ni mbumbu,ila umbumbu wangu ndio uliosababisha niseme kuwa ukisha ingia mkataba ni lazima ufanye jinsi mkataba unavyotaka,sasa hayo mengine kama yapo kinyume mimi si kiongozi na sina haja ya kuelewa hayo,dhamila yangu inatuma kuelewa kuwa unapoingia mkataba ni lazima ufuate masharti ya mkataba.sasa kama ni kinyume na hayo tuwaachie wenye vyama vyao
 
Acha upuuzi tuambie matumizi ya fedha zote mlizopewa (CCM) na sabodo kama sio kununua wapiga kura
 
Hizo pesa zitawafikia kweli wahusika.
 
Nenda Lumumba kachukue mshahara wako
 
Safari hii Slaa sijui atajikopesha shilingi ngapi!
 
Ingekuwa vizuri na vyama vingine viweke taarufa zao za misaada wazi kiasi na malengo yake ili wananchi tuweze kuwapima utekelezaji wao.
 
acha umbumbu kijana,sabodo ametoa msaada mara ngapi wakawekeana mkataba?
Umeona zilipoelekea?

Haya sabado alitoa millon 400 kujenga chuo cha kilelea viongozi na vijana wa chadema pale kibaha ..fedha zilitolewa mwaka 2010 hicho chuo umekiona?

wewe ndo mbumbu hujui unalolisema kama ushamba wewe namba moja tena lenye mbolea asili.funga domo lako linalonika ufisadi na una roho mbaya !!!!!!!!hilooooooooooooooo!!!!!!!!11
 
Matumizi yake yamewekwa bayana hapo juu,hilo ulilolitaja wewe ni lako na kumbuka wameingia mkataba,mkataba ambao watatakiwa kuweka wazi matumizi ya pesa hiyo na nadhani haiwezekani wakafanya kinyume na mkataba waliousaini.

umemjibu ya nini sasa huyu kuzi...ungemuacha tu...
 
Nilishtuka kweli nilivyoona Conservative party, nilifikiri ni kile cha Bwana Cameron mzee wa wali maftah a.k.a bwabwa a.k.a chakra!!! Lakini nilishawahi sikia kuwa kile pia ni chama hisani cha CDM hivi ni kweli eenh??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…