Chadema wapinduana bunda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema wapinduana bunda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Salimia, Sep 28, 2011.

 1. S

  Salimia JF-Expert Member

  #1
  Sep 28, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 665
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] Wandugu hawa jamaa nadhani malaria inapanda kichwani, yaani ni wtu wa fujo fujo tu kila mahali! ndiyo matokeo ya kutumia mimea korofi Terrible.......


  Christopher Maregesi, Bunda
  MAPINDUZI ya uongozi yamefanyika ndani ya Chadema katika Jimbo la Bunda wilayani hapa, baada ya kundi moja kufanya uchaguzi wa viongozi wake watakaokiongoza kwa miaka mitano huku viongozi walioko madarakani wakiuelezea uchaguzi huo kuwa ni batili.

  Jana, katika mkutano wa chama hicho jimboni humo, wajumbe waliwachagua viongozi wapya kwa nafasi za Mwenyekiti, Makamu wake, Katibu mkuu na msaidizi wake pamoja na wajumbe wa kamati tendaji watakaokiongoza chama hicho kwa muda wa miaka mitano ijayo.

  Waliochaguliwa ni Jonathan Matiko kwa nafasi ya Mwenyekiti, Julius Wassira kwa nafasi ya katibu ambapo Samuel Alfred alichaguliwa kuwa mweka hazina wa chama hicho jimboni humo huku Davis Robert akichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa baraza la vijana la chama hicho (Bavicha) na Timothy Mburumatale akichaguliwa kuwa katibu mwenezi.

  Kwa mujibu wa msimamizi wa uchaguzi huo, Ferdinand Msilikale, wengine waliochaguliwa kushika nafasi mbalimbali za uongozi ni Godfrey Mkoba (mjumbe wa Bavicha jimboni), wajumbe wengine wa kamati tendaji ni Mohamed Tinga na Baby Mwasi huku Georges Miyawa, akichaguliwa kuwa mwenyekiti wa baraza la wazee la chama hicho jimboni humo.

  Wakati wajumbe hao wapatao 186 wakifanya uchaguzi huo, kwa upande wake uongozi uliko madarakani kupitia Katibu wake, Kaisiki Muyemba, ulisema kamwe hautambui mabadiliko hayo ya uongozi kwa vile mkutano huo uliitishwa na mwanachama wa chama hicho aliyesimamishwa uanachama tangu Mei mwaka huu kwa sababu mbalimbali.

  Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, Kasiki alisema Matiko aliyechaguliwa na wajumbe hao kuwa mwenyekiti alisimamishwa uanachama Mei mwaka huu na uongozi wa tawi lake la Miembeni la mjini hapa baada ya kumtuhumu kukihujumu chama wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

  “Huyo aliyeitisha mkutano huo na kisha kachaguliwa kuwa mwenyekiti siyo mwanachama wetu hai kwani alisimamishwa na uongozi wa tawi lake Mei mwaka huu kwa kosa la kukisaliti chama wakati wa uchaguzi uliopita.
  Hivyo sisi kama viongozi hatuyatambui mabadiliko hayo ya uongozi,” alisema Kasiki.

  Kulingana na katibu huyo mara baada kumsimamisha uanachama uongozi wa tawi lake ulitoa taarifa kwa uongozi wa wilaya ambapo kikao cha kamati tendaji kilichofanyika mapema mwezi huu kiliazimia kulipeleka suala hilo mbele ya mkutano mkuu wa jimbo utakaofanyika mapema mwezi ujao katika Kijiji cha Nyamuswa ili ulitolee uamuzi kama katiba inavyoelekeza.

  Hata hivyo, kama kile kinachoonekana kutambua hali halisi ya mambo ilivyo ndani ya chama hicho katika hotuba yake mara baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti Matiko alitoa rai kwa wanachama wa Chadema jimboni humo kutoruhusu majungu aliyosema yanaweza kukiua chama badala yake washikamane kwa pamoja katika kukiimarisha chama jimboni humo ili kijiwekee mazingira mazuri ya ushindi kwa chaguzi zijazo.

  Source: Mwananchi and Tanzania Daima

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #2
  Sep 28, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,401
  Likes Received: 736
  Trophy Points: 280
  Hawa jamaa hawaishi vituko....mmea korofi kazini...
   
 3. S

  Salimia JF-Expert Member

  #3
  Sep 28, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 665
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hawa jamaa mikosi mkuu. Tuwaweke kwenye maombi tu
   
 4. Dume la Mende

  Dume la Mende JF-Expert Member

  #4
  Sep 28, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 419
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  akuna kitu apo wakuu,,, nileteeni hao wakorofi niwashughulikie,, miye ndo dume la mende bana,, siogopi kinyesi
   
 5. Laface77

  Laface77 JF-Expert Member

  #5
  Sep 28, 2011
  Joined: Jul 9, 2008
  Messages: 1,293
  Likes Received: 1,436
  Trophy Points: 280
  Anayetumia mmea korofi ni ****** aka Vasco da Gama kwa kubadilishana maliasili za nchi na pea tano za suti na mwigulu aliyefumaniwa Igunga!Yakhe karibu twala ubwabwa
   
 6. Dume la Mende

  Dume la Mende JF-Expert Member

  #6
  Sep 28, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 419
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Unachekesha wewe,, yaaani unaweza kubishana hata na TV.. Huoni wenzio wanavyopinduana huko?? then wewe unabisha tu na kuingiza ishu ambazo hazipo. Grow up
   
 7. Malipesa

  Malipesa JF-Expert Member

  #7
  Sep 28, 2011
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 310
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Yani hapo ndo umeona kuna kitu cha ajabu saaaana. Kwani yale magamba vipi? siasa uchwara nazo je? yule aliyesigina amri ya sita ya mungu na mke wa kada mwenzake! kwa magamba kwao ni safi? kwa cdm noma!
   
 8. e

  ebrah JF-Expert Member

  #8
  Sep 28, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 397
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mi kwa mabadiliko ya uongozi sioni tatizo hadi uweke title ya kupinduana, kilichopo ni kwamba kuna hali ya kutoelewana na naamini viongozi husika wa wilaya na mkoa watashughulikia ajulikana mwenye mapungufu nani kati yao, uzuri chadema hakuna kubebana.mwenye makosa huwa anaambiwa makosa na taratibu za kikatiba zinafuata utaratibu wake!
   
 9. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #9
  Sep 28, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,401
  Likes Received: 736
  Trophy Points: 280
  Mwingine huyu hapa...
   
 10. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #10
  Sep 28, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  alert!! malware
   
 11. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #11
  Sep 28, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Endelea tu kula posho ili ulete upupu hapa!
   
 12. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #12
  Sep 28, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  huyo wassira mbona kama ndugu wa huyo mbunge wa BUNDA baba usingizi?
  tutajua tu hata madiwani wa Arusha ilikuwa hivi
  kuna kundi moja linatumika hapo lakini uzuri ni kwamba CC ya CHADEM ina meno
  kama kuna ubatili imekula kwao

  Dr slaa tunaomba kauli yako Tafadhali, au msemaji yeyote wa CHADEMA
  UKWELI NI UPI?
   
 13. KALYOVATIPI

  KALYOVATIPI JF-Expert Member

  #13
  Sep 28, 2011
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,419
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  chadema hamna kuvuana magamba ni kutoa jiwe na kuweka kokoto kikatiba ya chama
   
 14. Dume la Mende

  Dume la Mende JF-Expert Member

  #14
  Sep 28, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 419
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  unataka ukweli upi zaidi ya huo mkuu? absorb tu japo inauma
   
 15. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #15
  Sep 28, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Hawa CDM ipo siku watakuja kuuwana! Kwa uchu wa madaraka
   
Loading...