CHADEMA wapata pigo lingine Mwanza Madiwani wawili ushindi wao watenguliwa

Nsumba ntale tz

JF-Expert Member
Apr 19, 2016
713
762
Mahakama ya Mkoa wa Mwanza imetengua ushindi wa madiwani watatu wa Chadema Jijini Mwanza kufuatia ukiukwaji wa taratibu za kuhesabu kura uliofanywa na tume ya Uchaguzi mwishoni mwa mwaka Jana.

Kata mbili kati ya hizo ambayo ni kata ya Isamilo, na Kata ya Kitangiri marejeo ya Uchaguzi yatafanyika haraka iwezekanavyo Mara baada ya tarehe ya Uchaguzi kutangazwa na tume wakati kata ya Nyamanolo Diwani wa CCM ametangazwa kuwa mshindi Mara baada ya kuhujumiwa kwa kuibiwa kura.

Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu amesema kuwa Mahakama imefanya maamuzi ya kidemokrasia hivyo amewahakikishia ushindi wa kishindo wafuasi wa chama hicho kwenye kata zitakazorudiwa Uchaguzi.
 
Haya ndiyo yalitakiwa kufanyika na zanzibar mwenye mamlaka ya kutengua mshindi aliyetangazwa ni mahakama tu na sio vinginevyo
 
Naona Mwanza mahakama imeanza kufaanya kazi za chama kazeni buti ccm mbele kwa mbele.Mlishapewa pesa ya kufanyia kazi.Msiwaangushe waliotowa pesa.HAPA KAZI TU!!!!!!
 
Ubunge pia utenguliwe maana kura zote zilihesabiwa pamoja. Iweje kura za upande mmoja zionekane zilivurugwa wakati kura zilihesabiwa pamoja?
 
Yaani ccm sijui wanatupeleka wapi jamani? Huu ni wakati wa Tabu hakuna wa kubisha
 
hivi ZNZ hakuna walio lalamikia uchanguzi??????? au hakuna mahakama???? au JECHA ndiye aliyekuwa mgombea pekee wa majimbo yote ya uchaguzi na mlalamikaji!!!!!!!!!!!!!! Uchaguzi ulitenguliwa bila kesi na tarehe ya marudio ikapangwa. Only in this my mama land Tanzania!!!!!!!!!!!. Haki inaoyoonekana Mwanza sasa ingeonekana ZNZ demokrasia ingejidhihiri kwa uwazi zaidi na maswali yote hapo juu yangesadifiwa barabara
 
Ha ha haaaaaaaaa, na wananchi walivyokumbali Magufuli kwa utumbuaji majipu, wapinzani wategemee uchaguzi wowote wa marudio kuangukia pua.
 
Naona Mwanza mahakama imeanza kufaanya kazi za chama kazeni buti ccm mbele kwa mbele.Mlishapewa pesa ya kufanyia kazi.Msiwaangushe waliotowa pesa.HAPA KAZI TU!!!!!!
CCM imeteka mihimili ya mahakama na bunge, udongo mzuri wa kupanda mbegu ya udikteta
 
Yule wa CCM aliyeshindwa UDIWANI mahakama inampatia udiwani bila kurudia uchaguzi.

Wale wa UKAWA walioshinda UDIWANI mahakama inatengua ushindi wao inaamuru uchaguzi urudiwe.

nina doubt na hii taarifa because mahakama haina uwezo wa kisheria kumpatia mtu UDIWANI mahakamani zaidi ya kuamuru uchaguzi urudiwe.
 
Fedha zilizotolewa kwa muhimili wa mahakama waanza kufanya kazi,ipo siku uamuzi wa wananchi utaheshimiwa siyo zuruzunga za mahakama.
 
Haya ndiyo yalitakiwa kufanyika na zanzibar mwenye mamlaka ya kutengua mshindi aliyetangazwa ni mahakama tu na sio vinginevyo
Hao madiwani walilalamika mahakamani lakini Zanzibar rejea kama kuna mtu alilalamika mahakamani,rejea sheria na taratibu za uchaguzi wa nchi yako.
 
Back
Top Bottom