Kila uchao, CHADEMA wanalalama. Wanatupa shutuma kwachama tawala-CCM na vyombo vya dola. Shutuma za hujuma dhidi ya viongozi wa CHADEMA na harakati za kisiasa za kichama.
CHADEMA inadai kuwa viongozi wake wanapangiwa msururu wa mashtaka dhidi yao;mikutano yao inahujumiwa ili kuwatisha wananchi wasiendelee kuhudhuria;wanachama wa CHADEMA 'wananunuliwa' na kadhalika.CCM inakanusha kila itolewapo tuhuma dhidi yake na vyombo vya dola kama Polisi na Usalama wa Taifa.CHADEMA wanasisitiza,CCM wanapuuza.
Nini mwisho wa mambo haya? Nani mkweli?
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam.