Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Ni dhahiri kwamba Uchaguzi Mkuu wa 2015 umemalizika. Kumalizika kwa uchaguzi Mkuu wa 2015 kunatoa fursa kwa vyama vya siasa kujipanga kwa ajili ya uchaguzi ujao.
Mpaka sasa, ni chama cha Mapinduzi pekee ndicho hakina ombwe la Uongozi. Labda wanafuatia ACT. Ila kwa CHADEMA na CUF wao wana shughuli pevu ya kujaza mapengo yaliyoachwa wazi kutokana na viongozi wake wakuu kuachia ngazi baada ya kubakwa kwa mfumo wa kumpata mgombea Urais kupitia UKAWA.
Hata hivyo, CHADEMA wana kazi kubwa mbili mbele yao. Kwanza kumpata Katibu Mkuu ili kujaza nafasi iliyoachwa wazi baada ya Dk Slaa kujiuzulu mwishoni mwa mwezi Julai 2015. Kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA, nafasi hiyo ilipaswa kujazwa ndani ya siku tisini. Hata hivyo mpaka sasa, nafasi hiyo ipo wazi na taarifa zilizopo ni kwamba CHADEMA wamekosa mtu mwenye sifa za kukaribia sifa za Dr Slaa. Kutokana na kukosa mtu ndani ya CHADEMA, chama hicho kikawa na wazo la kumteua Frederick Sumaye kushika nafasi hiyo. Hata hivyo, mapendekezo hayo yanakataliwa na baadhi ya Mahafidhina.
Kazi ya pili ni ya kumpata Mgombea Urais. Ni dhahiri kwamba Edward Lowasa hatakuwa mgombea Urais wa CHADEMA kwa mwaka 2020. Kwani mpaka sasa, imedhihiri kuwa mwanasiasa huyo ameshapoteza mvuto na mwelekeo. Ndani ya CHADEMA mpaka sasa hakuna figure hata moja ya kuivusha CHADEMA 2020. Jicho lao limeangaza tena kwa Sumaye. Hata hivyo, bado hali ni tete kwani Sumaye hana umaarufu wa kumzidi Lowasa. Hivyo kama Lowasa alipigwa kirahisi na Magufuli, sijui kwa Sumaye hali itakuwaje.
Pupa, ulafi na tamaa ya Mbowe ndiyo imewafikisha hapa CHADEMA.