Chadema wamnyemelea mbunge CUF; Lema amshangaa Membe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema wamnyemelea mbunge CUF; Lema amshangaa Membe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jun 7, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Wednesday, 06 June 2012 21:15[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  Geofrey Nyang'oro

  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jana kilizindua vuguvugu la mabadiliko (M4C) katika Mkoa wa Lindi huku kikimtaka Mbunge wa Jimbo la Lindi Mjini (CUF), Salum Barwani kujiunga na chama hicho.
  Katika siku hiyo ya kwanza, Chadema kilimnasa aliyekuwa meneja wa kampeni wa mbunge huyo, Abdallah Madebe.


  Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema mbunge huyo kwa sasa na wabunge wenzake wa CUF wamekuwa hawana sauti ya kutetea wananchi ndani ya Bunge kwa kuwa uongozi wa juu wa chama hicho umeungana na CCM.


  Mbowe alimkaribisha mbunge huyo baada ya wananchi wa Kata ya Nng'apa, kusema Barwani amefuatilia baadhi ya malalamiko yao ya muda mrefu lakini, juhudi zake zinakwamishwa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi na madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi.


  Malalamiko mengine ya wananchi hao yalikuwa mfumuko wa bei, kukosa huduma za afya na wanafunzi kutozwa Sh20,000 kwa ajili ya ulinzi wa shule za Serikali.


  Mkazi wa Kata ya Ng'apa, Rashid Issa alimweleza Mbowe katika mkutano huo kuwa hajui hatima ya maisha yao kutokana na mfumuko wa bei unaojitokeza kila wakati huku wakiendelea kutozwa kodi katika vivuko vya mazao na fedha hizo kuishia mikononi mwa wajanja.

  Akijibu hoja hizo, Mbowe alisema maisha magumu kwa Watanzania ni matokeo ya sera mbovu za Serikali ya CCM katika kusimamia uchumi wa nchi.

  Akimzungumzia Barwani, Mbowe alisema katika mazingira ya sasa ya CUF, mbunge huyo hatakuwa na uwezo wa kuwasaidia wananchi kwa sababu viongozi wa juu wa chama hicho, akiwamo Mwenyekiti, Profesa Ibrahim Lipumba na Katibu Mkuu, Seif Sharif Hamad ndiyo wanaofanya uamuzi na ‘wamekiunganisha' chama hicho na CCM.


  "Sina ugomvi na Barwani, ni mbunge na tunafanya naye kazi vizuri, tatizo ni misimamo ya viongozi wake wakuu. Hawa ni tatizo kwake. Ninamshauri ajitathmini na huku kwetu mlango uko wazi, anaweza kuusukuma na kuingia kwa ajili ya kuwatetea wana Lindi," alisema Mbowe.

  Mbowe aliwataka wakazi wa Lindi kutowavumilia viongozi wazembe ambao hawawezi kuwaelezea kodi zao zimetumika vipi, wakati wao wanashindwa kupata huduma za msingi.

  Slaa na polisi
  Akizungumza katika mkutano uliofanyika katika Uwanja wa Ilulu mjini hapa, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa aliwataka polisi wasipate tabu ya kurekodi mikutano yao, bali fedha wanazonunulia kanda za kurekodia wazitumie kuboresha maisha yao.

  Dk Slaa alidai kwamba katika mikutano ya Chadema, askari wamekuwa wakijaa kwa wingi kwa lengo la kusikiliza yanayozungumzwa ili wawafikishie mabosi wao.

  "Ninyi askari mnanishangaza sana ufisadi umejaa kila sehemu, badala ya kushughulika nao ninyi mnakuja kurekodi ili mseme tunachochea vurugu..." alisema Dk Slaa.Alisema atakachoweza kuwasaidia askari ni kuhakikisha kuwa mishahara yao inaongezwa baada ya mwezi wa saba.

  Lema amshangaa Membe
  Kwa upande wake, aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alisema Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Bernard Membe amepoteza sifa ya kufikiria kuwa kiongozi wa nchi kutokana na kushindwa kuusaidia Mkoa wa Lindi kuondokana na umaskini.

  Alisema kama Membe angekuwa kiongozi makini, angetumia fursa yake ya kusafiri nje kila wakati kutangaza vivutio vya Mkoa wa Lindi na kuufanya uwe mji wa kitalii kama mikoa mingine inayosifika kwa utalii Tanzania.

  Mnyika awashtukia wabunge CCM
  Mbunge wa Ubungo, John Mnyika alisema kama Rais Jakaya Kikwete asipopeleka bajeti yenye kupunguza mfumuko wa bei katika Bunge lijalo, Chadema itahamasisha nguvu ya umma kumshinikiza afanye hivyo.
  Alisema kauli inayotolewa na wabunge wa CCM kuwa wataigomea Bajeti ijayo ni ya kujikosha mbele ya jamii kwa kuwa wanajua wazi kuwa hilo haliwezekani kulingana na katiba waliyonayo.

  "Hawa wanasema wataipinga Bajeti wakati wana hamu ya kupokea posho za bungeni mbona wanajidanganya kwa kuwa wakifanya hivyo Rais atavunja Bunge na kwa hofu ya matendo yao, wengi wanajua hawataweza kurudi hivyo hizo ni propaganda tu," alisema Mnyika.

  Sugu na ajira za vijana
  Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) alisema wakati anaelekea Mtwara akiwa ndani ya ndege alijua mikoa hiyo ya kusini ni ya kupigiwa mfano kutokana na aina ya watu aliokuwa nao katika ndege, kwamba hata vijana wa Mkoa wa Lindi watakuwa wananufaika na rasilimali za mkoa huo.

  "Nilipotua nikawauliza kama vijana mnanufaika na gesi inayopatikana katika mikoa yenu? Cha ajabu mnaniambia kuwa mnachopata ni vifaa vya kukingia kifua tu."
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Hadi Lindi.... Mmm Mama Salma yuko wapi? Oh Anasubiri 2012 au 2013 kugombea U-NEC?

  Barwani wa CUF ni Msafi anafaa CHADEMA sio CHENGE
   
 3. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #3
  Jun 7, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ccm plus cuf is equal to sisiemu bii
   
 4. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #4
  Jun 7, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,277
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  Who Unleashed The Dragon???

  CCM Mtajuta kumpokonya Lema majukumu na kumwacha Huru, atawabomoa kinoma
   
 5. m

  mechard Rwizile JF-Expert Member

  #5
  Jun 7, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 937
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 80
  Kwa sasa kila mbunge makini katika CCM,CUF na NCCR mageuzi anatakiwa kujiandaa na kuwaandaa wanachama wake kisaikolojia kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA ) ili katika uchaguzi wa mwaka 2015 waweze kuchaguliwa. Na chama hicho kushinda uchaguzi kwa kuiangusha CCM. Inabidi wote tufanye hivyo ili kuanza hatua ya ukombozi.

  CCM ikianguka tutakuwa kumetoa funzo moja kubwa sana; kwamba chama chochote kitakachokuwa kimechaguliwa kiwe makini kutekeleza ahadi zake,vinginevyo kitapigwa chini katika uchaguzi unaofuata.

  Katika chaguzi zilizotangulia hasa kuanzia mwaka 1995, CCM kimekuwa kiomba huruma ya wapiga kura kwa madai kuwa kitajirekebisha, baada ya kuonewa huruma na kuchaguliwa kinageuka na kuanza kusema sera zetu zinakubalika na wapinga kura wana imani nacho.

  Sasa wakati umefika wa ndama kurejea kwa mama yake. Mheshimiwa Baruan upo hapo! Mheshimiwa Kafulila upo? Mheshimiwa Mkosamali unasikia, Mheshimiwa Mwakyembe unasikia? Tafakari na chukua hatua.
   
 6. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #6
  Jun 7, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Peoples..........
   
 7. t

  tara Senior Member

  #7
  Jun 7, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 190
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Imenikumbusha ishu ya Kagawa na Sir Alex furguson.........
   
 8. m

  mwigo Member

  #8
  Jun 7, 2012
  Joined: May 8, 2012
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  slaa amepopolewa alipo anza kumzushia MTATIRO huko nanyumbu, nasasa mmeishiwa kabisa na sera za kuzungumza, kilicho baki ni CUF CUF CUF, HMNA JIPYA NYIE CUF KIBOKO YENU, kila kitu mna kazi ya kuiga tu.
   
 9. S

  Shembago JF-Expert Member

  #9
  Jun 7, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 332
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kazi bado inaendelea hitimisho kuchukua Nchi 2015
   
 10. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #10
  Jun 7, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,841
  Trophy Points: 280
  gamba at work for his daily bread
   
 11. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #11
  Jun 7, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  nawaonea huruma mawaziri na bajeti zao za mwaka huu...maana akina zitto lazima walianzishe huko bungeni
   
 12. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #12
  Jun 7, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Mbona sijaona mahali Dr (PhD) Slaa amezungumza habari ya cuf!? Ngoja nitafute miwani!
   
 13. m

  mwigo Member

  #13
  Jun 7, 2012
  Joined: May 8, 2012
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ULIZA UAMBIWE kila koner issue ni CUF badala wazungumzie matatizo ya watu wa kusini. hata yeye atakueleza. na operasion yao imeishia leo baada ya wakati mgumuuuuuuuuuuuu
   
 14. m

  mwigo Member

  #14
  Jun 7, 2012
  Joined: May 8, 2012
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  inakula kwenu hiyo maana baadaya kukosa mtu wa kuwapa mambo ya kuongea mmemukosa sasa mnabaki kukashifu vyama vya wenzenu tu, hamadi ndio alikuwa anawapa mambo ya kuhusu ufisadi sasa kafukuzwa hamna jipya tuone kama mtatoa, mtaishia hivo hivo tuuuuuuuuuu. hata penye ukweli mnapinga haoooooooooooooo
   
 15. Mr. Bigman

  Mr. Bigman JF-Expert Member

  #15
  Jun 7, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,853
  Likes Received: 629
  Trophy Points: 280
  Barwani aje Cdm,Lindi Municipal itapaa
   
 16. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #16
  Jun 7, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,841
  Trophy Points: 280
  maneno yako kama ya kwenye kanga za mipasho zinazouzwa pale mataa wa kongo...
  CHADEMA NI CHAMA MAKINI sana..na sa izi tumevamia KUSINI sasa nyie na SPOUSESwenu CUF inabidi mfe pamoja si au mtatumia ile kauli yenu ya "KUTOTENGANA MPAKA KIFO KIWATENGANISHE??"
   
 17. Mr. Bigman

  Mr. Bigman JF-Expert Member

  #17
  Jun 7, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,853
  Likes Received: 629
  Trophy Points: 280
  Hii huja wakati magamba na jamaa zao yanapopata moto!
   
 18. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #18
  Jun 7, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  Kama barca vile
   
 19. N

  Noboka JF-Expert Member

  #19
  Jun 7, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 1,144
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  “Nilipotua nikawauliza kama vijana mnanufaika na gesi inayopatikana katika mikoa yenu? Cha ajabu mnaniambia kuwa mnachopata ni vifaa vya kukingia kifua tu.”
  Sugu anakufanya ufikiri hasa, nakumbuka hata lile suala la Twiga alivyomuuliza Maige awaeleze aliwezaje kumuingiza Twiga na ulefu wote kwenye ndege!
  Kwa watu wa kusini huu ni wakati wao kukombolewa, kila la kheri kwao!
   
Loading...