CHADEMA walihubiri mabadiliko wasiyoyajua?

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,999
Habari wana JF!

Kadiri siku zinavyosonga nimelewa kuwa Chadema walihubiri mabadiliko wasiyoyajuwa na kwa sasa kasi ya upumbavu inatamalaki kwa hali ya juu.

Tulihitaji serikali itakayoleta nidhamu kwa watumishi wa umma na ikibidi kuwachukulia hatua inapobidi.... Nimeshangaa eti Mtumishi asiyechukuwa mhahara miaka 3 wamemwita shujaa na mzalendo eti ni msomi sana na hamna badala...dah.

Hamna nchi duniani mtu anaweza akagomea mshahara halafu muajiri akamuacha... eti anaishi kwa posho, eti mmewe ni tajiri... upumbavu. Niwakumbushe tu kama huridhiki na mshahara unapaswa kuondoka mara moja.

Eti, kulikuwa na "negotiations" inaendelea kati yake na JK miaka mitatu, bodi imeshindwa kuidhinisha maamuzi ya raisi?... Nani ana ushahidi wa mazungumzo?

Eti, Raisi amepotoshwa?..anakurupuka! Hivi kuna mtu ana taarifa za watumishi au usalama kuliko Rais?.. Maana'ke wengi wanaosema hivyo ni watu hopeless kama kina Kibonde na magenge yao.

Hivi kwa sababu amewajibisha viongozi wengi kwa ubadhirifu kwa hiyo ikitokea mwingine kaleta hasara asiwajibishwe?.. Upumbavu huu, ni idadi gani ikifika utumbuaji usimame?...Hivi Chadema hamkumbuki ninyi mlisema hii nchi inatakiwa isafishwe kila idara?... Hivi karibuni walikamatwa majangili huko Maswa na mahakama kuwaadhibu... eti, hao wanaonewa?

Hivi ikitokea ripoti ya CAG inaripoti ubadhirifu kwenye idara zote serikalini na hasara kubwa imepatikana je ni dhambi kuwaondoa?... Wakiachwa, CCM ni ile ile!!!! Raisi akichukuwa hatua ohhh! angefanya uchunguzi, amekurupuka!.. Hivi kuna uchunguzi gani zaidi ya CAG?..

CAG ametoa ripoti ya kuwa vyama 21 havijakaguliwa, Chadema wameibuka.... huyu CAG katumwa na serikali kudhalilisha chama, Ujuha huu!

Ukawa... wananchi wanashuhudia jinsi huu upumbavu unavyotamalaki hamtabaki salama.

Nawasilisha.
 
Mleta mada una mihemko na una stress,tulia jenga hoja!Papara ya nin?
Kumbe nidhamu inarejeshwa kwa watumishi wa umma tu,sio kwa wanasiasa!
 
ukawa wanahaha wanatafuta sympathy Kwa wanao adhibiwa(either Kwa ufisadi au uzembe kazini) wakiamin wataungana nao kukuza chama!Chadema ungeni mkono juhudi za JPM otherwise mnapoteza watanzania wanawaona mnavo wafanya vipofu, mafisadi sasa ndo sehemu ya chadema! plz cdm back on your track
 
Kuntu!
 
ni nafasi za kisiasa,sasa hujaelewa kipi?mbona mzembe hivyo?
Dah...mbona vitu vya msingi huelewi?...ngoja nikufundishe,ndio maana siku wanateuliwa walijaza fomu za maadili ya viongozi wa umma...na hiyo ni lazima hata kwa wakurugenzi na mameneja wa mashirika ya umma!!!
 
CHADEMA wasipotoa maoni yao kwenye kila kinachofanywa na serikali ya CCM wanahisi kwamba wanaweza kupotea mapema kisiasa, hivyo ni lazima wawakumbushe watu kwamba na wao bado wapo. Tatizo linakuja kwenye jinsi ambavyo wanawakilisha mawazo yao ambayo yanapaswa kuwa mbadala na bora kuliko yale ya CCM. Lakini CCM inayoitwa chama kikongwe, mwakani inafikisha miaka 40, CHADEMA mwakani inafikisha miaka 25, hivi ni vyama vichanga sana, vinahitaji kukua kadri miaka inavyozidi kwenda.
 
kuna tofauti kati ya watumishi wa umma na viongozi wa umma.Mbona watumishi waliofanya madudu awamu iliyopita wametumbuliwa na magufuli ila viongozi waliofanya madudu awamu iliyopita wamepewa second chance na bado wanaboronga hawatumbuliwi.mfano ni yule waziri aliyetoboa siri ya ziara ya kushtukiza ya Mh Majaliwa ikasababisha maandalizi ya upesi upesi ya kujaribu kuziibua meter toka kuzimu ikashindikana,hebu nieleze huyo hakustahili kuwa jipu?Mbona kapeta?wanaoshughulikiwa ni watumishi wa umma,ila viongozi wanapeta.
 
Yap kweli,pia wamejitwika mzigo ambao wanashindwa kushambulia,wamebaki kujitetea....wanatumia "vinjago"..vya adui kumtisha!
 
kuna tofauti kati ya watumishi wa umma na viongozi wa umma.Mbona watumishi waliofanya madudu awamu iliyopita wametumbuliwa na magufuli ila viongozi waliofanya madudu awamu iliyopita wamepewa second chance na bado wanaboronga hawatumbuliwi.mfano ni yule waziri aliyetoboa siri ya ziara ya kushtukiza ya Mh Majaliwa ikasababisha maandalizi ya upesi upesi ya kujaribu kuziibua meter toka kuzimu ikashindikana,hebu nieleze huyo hakustahili kuwa jipu?Mbona kapeta?wanaoshughulikiwa ni watumishi wa umma,ila viongozi wanapeta.
Kichwa kama chako ndio kinafanya hadi kina mbowe,lema,msigwa kuwa wanasiasa...bure kabisa!
 
Habari wana JF!

Kadiri siku zinavyosonga nimelewa kuwa Chadema walihubiri mabadiliko wasiyoyajuwa na kwa sasa kasi ya upumbavu inatamalaki kwa hali ya juu.

Tulihitaji serikali itakayoleta nidhamu kwa watumishi wa umma na ikibidi kuwachukulia hatua inapobidi.... Nimeshangaa eti Mtumishi asiyechukuwa mhahara miaka 3 wamemwita shujaa na mzalendo eti ni msomi sana na hamna badala...dah.

Hamna nchi duniani mtu anaweza akagomea mshahara halafu muajiri akamuacha... eti anaishi kwa posho, eti mmewe ni tajiri... upumbavu. Niwakumbushe tu kama huridhiki na mshahara unapaswa kuondoka mara moja.

Eti, kulikuwa na "negotiations" inaendelea kati yake na JK miaka mitatu, bodi imeshindwa kuidhinisha maamuzi ya raisi?... Nani ana ushahidi wa mazungumzo?

Eti, Raisi amepotoshwa?..anakurupuka! Hivi kuna mtu ana taarifa za watumishi au usalama kuliko Rais?.. Maana'ke wengi wanaosema hivyo ni watu hopeless kama kina Kibonde na magenge yao.

Hivi kwa sababu amewajibisha viongozi wengi kwa ubadhirifu kwa hiyo ikitokea mwingine kaleta hasara asiwajibishwe?.. Upumbavu huu, ni idadi gani ikifika utumbuaji usimame?...Hivi Chadema hamkumbuki ninyi mlisema hii nchi inatakiwa isafishwe kila idara?... Hivi karibuni walikamatwa majangili huko Maswa na mahakama kuwaadhibu... eti, hao wanaonewa?

Hivi ikitokea ripoti ya CAG inaripoti ubadhirifu kwenye idara zote serikalini na hasara kubwa imepatikana je ni dhambi kuwaondoa?... Wakiachwa, CCM ni ile ile!!!! Raisi akichukuwa hatua ohhh! angefanya uchunguzi, amekurupuka!.. Hivi kuna uchunguzi gani zaidi ya CAG?..

CAG ametoa ripoti ya kuwa vyama 21 havijakaguliwa, Chadema wameibuka.... huyu CAG katumwa na serikali kudhalilisha chama, Ujuha huu!

Ukawa... wananchi wanashuhudia jinsi huu upumbavu unavyotamalaki hamtabaki salama.

Nawasilisha.
UKAWA/ CHADEMA hawaeleweki wanataka nini!?!?!?!?!?!
 
Back
Top Bottom