CHADEMA wajifunze kwa CUF

CHADEMA wajifunze kwa CUF

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,578
MIAKA kadhaa iliyopita Chama cha Wananchi (CUF) kilikuwa na sera au kaulimbiu za ‘ngangari’ na ‘jino kwa jino’.
Nakumbuka Uchaguzi Mkuu wa 2000 hadi 2005 sera hiyo ilikuwa katika kilele chake. Ukienda katika mikutano viongozi waliwasalimu wanachama kwa: ‘CUF’ ngangariii’ ‘vijana ngangariiii’, ‘akina mama ngangariii’. Wafuasi nao walijibu: ‘ngangariiii’.
Ukiacha salamu hizo, kulikuwa na nyimbo na vidokezo vilivyobeba ujumbe wa jino kwa jino uliotumika kuhamasisha wanachama, wafuasi na wapenzi wa chama hicho katika mikutano, maandamano na shughuli nyingine za kichama.
Kwa mujibu wa Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mawasiliano na Umma wa CUF, Abdul Kambaya, ngangari neno ambalo maana yake ni ukakamavu au kwa lugha ya vijana ‘kukomaa katika jambo fulani’; na ‘jino kwa jino’ msemo ambao unahimiza kulipa ubaya kwa ubaya (kisasi); ni kaulimbiu zilizoanzishwa kwa nia nzuri.
Akielezea maana ya kaulimbiu hizo, Kambaya anasema ‘ngangari’ na ‘jino kwa jino’ zilikuwa ni kaulimbiu zilizohimiza ukakamavu katika kudai haki, na kwamba ni wapinzani wao CCM na vyombo vya habari vilivyopotosha tafsiri ya kaulimbiu hizo.
Tafsiri mbaya anayoizungumzia Kambaya ni ile taswira iliyojengeka katika jamii juu ya CUF ya miaka ile ambapo baadhi ya wananchi walikichukulia (baadhi hadi sasa) kuwa ni chama cha kigaidi kinachoendeleza siasa za visasi, fujo, vurugu, matusi, ubabe na uvunjifu wa amani.
CCM ilitumia vema kaulimbiu hizo tata za CUF zilijojenga taswira mbaya mbele ya jamii kujinufaisha kisiasa kwa kukishambulia chama hicho kila walipopata nafasi. CCM walihakikisha wanaaminisha na kuimarisha taswira ya CUF kama chama cha kigaidi kwa kutumia kila aina ya hoja. Hata rangi nyekundu katika bendera ya CUF ilitajwa kuwa ni ushahidi kuwa ni chama kinachokusudia kumwaga damu.
Januari 27, 2001 taswira ya CUF kama chama cha kigaidi iliimarika zaidi baada ya kuendesha maandamano yaliyopigwa marufuku na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 30 (kwa mujibu wa takwimu za CUF), hususan kule Pemba huku wengine kadhaa wakikamatwa na kushitakiwa.
Lengo la maandamano yale ilikuwa ni kuelezea kutoridhika kwa chama hicho na mchakato wa uchaguzi wa 2000 na baada ya hapo walichodai kuwa ni unyanyasaji na ukiukwaji wa haki za biandamu.
Mabalaa yaliendelea kuiandama CUF pale ambapo siku moja kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Omar Mahita, alikutana na waandishi wa habari na kukituhumu CUF kwamba kimeingiza makontena ya visu na majambia kwa ajili ya kuchafua amani.
CUF, wakati huo kikiwa chama chenye nguvu zaidi miongoni mwa vyama vya upinzani, hakikupata hata nafasi wa kukanusha habari zile. Kulipokucha wananchi wote walikuwa wakizungumzia tukio hilo huku wakisubiri kupiga kura. Hata wana CUF wenyewe walichanganyikiwa wasijue kama habari zile ni za kweli ama la. Inasemekana wengi hawakujitokeza hata kupiga kura.
Hujuma hizi za CCM zisingefanikiwa bila CUF wenyewe kujenga msingi mbaya kwa kuanzisha na kutumia kaulimbiu hizi ambazo si tu zinaweza kutafsiriwa kama za kuchochea fujo lakini pia zinaenda kinyume kabisa cha falsafa ya moja ya dini kuu za Watanzania, ukristu, unaohubiri ukichapwa kofi shavu moja, geuza shavu la pili.
Kwa mujibu wa Kambaya, pamoja na CUF kuamini kuwa vyombo vya habari vimepotosha kaulimbiu hizo za ngangari na jino kwa jino, viongozi waliona umuhimu wa kujitathmini na kujiuliza kama kaulimbiu hizo zinakisaidia chama. Wakaamua kuachana nazo. Wakaamua wapunguze siasa za mapambano.
Pamoja na kutumia kaulimbiu hizo, si kwamba CUF haikuwa na wafuasi. Walikuwapo wengi ingawa si idadi ya kutosha kushinda uchaguzi mkuu.
Tatizo lililoikumba CUF ni kuwa haikuweza kuvutia wafuasi wapya, nje ya kundi la kijamii ambalo CUF kiasili ina ufuasi. Na hata kundi hilo ambalo CUF kiasili ina ufuasi si lote liliunga mkono chama hicho. Kwa mfano, inaaminika CUF imetaga mayai kusini mwa nchi na maeneo ya pwani, lakini mbona haijafanikiwa kupata wabunge wa kutosha maeneo hayo?
Kwa maoni yangu kulikuwa na tatizo katika taswira ambayo chama hicho kilijijengea kwa umma, taswira ya chama cha kigaidi na fujo. Taswira hii iliogofya makundi fulani ya kijamii. CUF imejaribu kubadilisha taswira hiyo iliyoogofya watu, ingawa ilishawagharimu huko nyuma.
Bahati mbaya ni kuwa CUF walichelewa kung’amua tatizo la taswira lililotokana na si tu kaulimbiu lakini hata baadhi ya vitendo vyao. CUF walichelewa kuona tatizo kwa sababu waliamini tayari wanaungwa mkono na Watanzania wengi.
CUF hawakujua kuwa katika siasa, kelele na kujitokeza kwa watu katika mikutano si kipimo cha ushindi. Unaweza kuwa na wafuasi wachache wenye mwamko mkubwa ambao wapo tayari kusafiri kila penye mkutano wa chama kupeleka hamasa. Unaweza kudhani unafanya kampeni kumbe unaimarisha tu imani ya wanachama wako.
Kutokana na matukio ya karibuni ni wazi kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) nacho kinaelekea kupita njia ile ambayo CUF walishaijaribu, wakaiona haiwafai na kuamua kuiasi.
Sisemi kwamba lazima mkakati ulioshindwa kuisaidia CUF lazima ushindwe pia kwa CHADEMA, hasa ukizingatia tunalinganisha nyakati tofauti, vyama tofauti, viongozi tofauti, na hata uwezo tofauti wa kukabiliana na propaganda. Hata hivyo, ni vema CHADEMA wawe waangalifu.
Katika miaka ya karibuni, mikusanyiko ya CHADEMA imewahi kukumbwa na vurugu zilizosababisha mauaji katika maeneo kadhaa ikiwemo Arusha, Iringa na Morogoro, ingawa mara nyingi ni matendo ya polisi ya kuzuia mikusanyiko ndio ilikuwa chanzo cha fujo. Kadhalika, kumekuwa na jitihada za CCM za kuihusisha CHADEMA na matukio kadhaa ya kigaidi ikiwemo kutesa na kupanga mipango ya kuumiza watu (rejea video ya Lwakatare) na kadhalika.
Lakini, pamoja na jitihada za CCM za kukihusisha chama hicho na fujo, CHADEMA imeendelea kukua na kupata uhai kutokana na kazi yake ya kuhimiza maendeleo na kupambana na ufisadi na kwa hivyo imekubalika maeneo mbalimbali.
Hata hivyo, pamoja na Watanzania kuunga mkono CHADEMA na kukifanya chama kikuu cha upinzani kwa Tanzania Bara, ni muhimu chama hicho kitathmini mwelekeo wake na kuhakikisha hakipotezi umaarufu wake, kinakua zaidi na kuvutia makundi ya wafuasi nje ya makundi ya wafuasi wake wa sasa.
Je, mwelekeo wa kimapambano kinaouchukua sasa wa kuhimiza maandamano yasiyo na kikomo utakisaidia chama hicho kukua kisiasa ama la? Msimamo huo una faida? Hilo ni swali la msingi CHADEMA wanapaswa kujiuliza.
CUF ambao wamo katika muungano wa UKAWA si wajinga kunyamaza na kuwaachia CHADEMA waongoze maandamano.
Kwa CUF huu ni mkakati wa kisiasa unaotokana na miaka ya uzoefu wa siasa za mapambano. Walijifunza kuwa siasa za mapambano hazilipi.
Watanzania wengi wanapenda maendeleo sana lakini wanapenda amani zaidi. Hawa ndugu zangu Waswahili ninaoishi nao huku Magomeni, Dar es Salaam ukiwaambia maandamano ya kudai kuahirishwa Bunge la Katiba wanakuona chizi tu.
Hata marafiki zangu wa daraja la kati, wanaweza kukuunga mkono katika misimamo yako ya kudai serikali tatu lakini maandamano!? No way.
 
Ccm bado haijapata mpinzani...

Kumbuka Rais ajaye ndiye atakaye amua kama aendelee na rasimu hii ya Sitta au aachane nayo!

CCM mnashangilia kitu msichokijua kabisa na inaonekana hata ww unajua kuwa alichopitisha Sitta jana ndiyo katiba tayari!
 
MIAKA kadhaa iliyopita Chama cha Wananchi (CUF) kilikuwa na sera au kaulimbiu za ‘ngangari' na ‘jino kwa jino'.
Nakumbuka Uchaguzi Mkuu wa 2000 hadi 2005 sera hiyo ilikuwa katika kilele chake. Ukienda katika mikutano viongozi waliwasalimu wanachama kwa: ‘CUF' ngangariii' ‘vijana ngangariiii', ‘akina mama ngangariii'. Wafuasi nao walijibu: ‘ngangariiii'.
Ukiacha salamu hizo, kulikuwa na nyimbo na vidokezo vilivyobeba ujumbe wa jino kwa jino uliotumika kuhamasisha wanachama, wafuasi na wapenzi wa chama hicho katika mikutano, maandamano na shughuli nyingine za kichama.
Kwa mujibu wa Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mawasiliano na Umma wa CUF, Abdul Kambaya, ngangari neno ambalo maana yake ni ukakamavu au kwa lugha ya vijana ‘kukomaa katika jambo fulani'; na ‘jino kwa jino' msemo ambao unahimiza kulipa ubaya kwa ubaya (kisasi); ni kaulimbiu zilizoanzishwa kwa nia nzuri.
Akielezea maana ya kaulimbiu hizo, Kambaya anasema ‘ngangari' na ‘jino kwa jino' zilikuwa ni kaulimbiu zilizohimiza ukakamavu katika kudai haki, na kwamba ni wapinzani wao CCM na vyombo vya habari vilivyopotosha tafsiri ya kaulimbiu hizo.
Tafsiri mbaya anayoizungumzia Kambaya ni ile taswira iliyojengeka katika jamii juu ya CUF ya miaka ile ambapo baadhi ya wananchi walikichukulia (baadhi hadi sasa) kuwa ni chama cha kigaidi kinachoendeleza siasa za visasi, fujo, vurugu, matusi, ubabe na uvunjifu wa amani.
CCM ilitumia vema kaulimbiu hizo tata za CUF zilijojenga taswira mbaya mbele ya jamii kujinufaisha kisiasa kwa kukishambulia chama hicho kila walipopata nafasi. CCM walihakikisha wanaaminisha na kuimarisha taswira ya CUF kama chama cha kigaidi kwa kutumia kila aina ya hoja. Hata rangi nyekundu katika bendera ya CUF ilitajwa kuwa ni ushahidi kuwa ni chama kinachokusudia kumwaga damu.
Januari 27, 2001 taswira ya CUF kama chama cha kigaidi iliimarika zaidi baada ya kuendesha maandamano yaliyopigwa marufuku na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 30 (kwa mujibu wa takwimu za CUF), hususan kule Pemba huku wengine kadhaa wakikamatwa na kushitakiwa.
Lengo la maandamano yale ilikuwa ni kuelezea kutoridhika kwa chama hicho na mchakato wa uchaguzi wa 2000 na baada ya hapo walichodai kuwa ni unyanyasaji na ukiukwaji wa haki za biandamu.
Mabalaa yaliendelea kuiandama CUF pale ambapo siku moja kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Omar Mahita, alikutana na waandishi wa habari na kukituhumu CUF kwamba kimeingiza makontena ya visu na majambia kwa ajili ya kuchafua amani.
CUF, wakati huo kikiwa chama chenye nguvu zaidi miongoni mwa vyama vya upinzani, hakikupata hata nafasi wa kukanusha habari zile. Kulipokucha wananchi wote walikuwa wakizungumzia tukio hilo huku wakisubiri kupiga kura. Hata wana CUF wenyewe walichanganyikiwa wasijue kama habari zile ni za kweli ama la. Inasemekana wengi hawakujitokeza hata kupiga kura.
Hujuma hizi za CCM zisingefanikiwa bila CUF wenyewe kujenga msingi mbaya kwa kuanzisha na kutumia kaulimbiu hizi ambazo si tu zinaweza kutafsiriwa kama za kuchochea fujo lakini pia zinaenda kinyume kabisa cha falsafa ya moja ya dini kuu za Watanzania, ukristu, unaohubiri ukichapwa kofi shavu moja, geuza shavu la pili.
Kwa mujibu wa Kambaya, pamoja na CUF kuamini kuwa vyombo vya habari vimepotosha kaulimbiu hizo za ngangari na jino kwa jino, viongozi waliona umuhimu wa kujitathmini na kujiuliza kama kaulimbiu hizo zinakisaidia chama. Wakaamua kuachana nazo. Wakaamua wapunguze siasa za mapambano.
Pamoja na kutumia kaulimbiu hizo, si kwamba CUF haikuwa na wafuasi. Walikuwapo wengi ingawa si idadi ya kutosha kushinda uchaguzi mkuu.
Tatizo lililoikumba CUF ni kuwa haikuweza kuvutia wafuasi wapya, nje ya kundi la kijamii ambalo CUF kiasili ina ufuasi. Na hata kundi hilo ambalo CUF kiasili ina ufuasi si lote liliunga mkono chama hicho. Kwa mfano, inaaminika CUF imetaga mayai kusini mwa nchi na maeneo ya pwani, lakini mbona haijafanikiwa kupata wabunge wa kutosha maeneo hayo?
Kwa maoni yangu kulikuwa na tatizo katika taswira ambayo chama hicho kilijijengea kwa umma, taswira ya chama cha kigaidi na fujo. Taswira hii iliogofya makundi fulani ya kijamii. CUF imejaribu kubadilisha taswira hiyo iliyoogofya watu, ingawa ilishawagharimu huko nyuma.
Bahati mbaya ni kuwa CUF walichelewa kung'amua tatizo la taswira lililotokana na si tu kaulimbiu lakini hata baadhi ya vitendo vyao. CUF walichelewa kuona tatizo kwa sababu waliamini tayari wanaungwa mkono na Watanzania wengi.
CUF hawakujua kuwa katika siasa, kelele na kujitokeza kwa watu katika mikutano si kipimo cha ushindi. Unaweza kuwa na wafuasi wachache wenye mwamko mkubwa ambao wapo tayari kusafiri kila penye mkutano wa chama kupeleka hamasa. Unaweza kudhani unafanya kampeni kumbe unaimarisha tu imani ya wanachama wako.
Kutokana na matukio ya karibuni ni wazi kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) nacho kinaelekea kupita njia ile ambayo CUF walishaijaribu, wakaiona haiwafai na kuamua kuiasi.
Sisemi kwamba lazima mkakati ulioshindwa kuisaidia CUF lazima ushindwe pia kwa CHADEMA, hasa ukizingatia tunalinganisha nyakati tofauti, vyama tofauti, viongozi tofauti, na hata uwezo tofauti wa kukabiliana na propaganda. Hata hivyo, ni vema CHADEMA wawe waangalifu.
Katika miaka ya karibuni, mikusanyiko ya CHADEMA imewahi kukumbwa na vurugu zilizosababisha mauaji katika maeneo kadhaa ikiwemo Arusha, Iringa na Morogoro, ingawa mara nyingi ni matendo ya polisi ya kuzuia mikusanyiko ndio ilikuwa chanzo cha fujo. Kadhalika, kumekuwa na jitihada za CCM za kuihusisha CHADEMA na matukio kadhaa ya kigaidi ikiwemo kutesa na kupanga mipango ya kuumiza watu (rejea video ya Lwakatare) na kadhalika.
Lakini, pamoja na jitihada za CCM za kukihusisha chama hicho na fujo, CHADEMA imeendelea kukua na kupata uhai kutokana na kazi yake ya kuhimiza maendeleo na kupambana na ufisadi na kwa hivyo imekubalika maeneo mbalimbali.
Hata hivyo, pamoja na Watanzania kuunga mkono CHADEMA na kukifanya chama kikuu cha upinzani kwa Tanzania Bara, ni muhimu chama hicho kitathmini mwelekeo wake na kuhakikisha hakipotezi umaarufu wake, kinakua zaidi na kuvutia makundi ya wafuasi nje ya makundi ya wafuasi wake wa sasa.
Je, mwelekeo wa kimapambano kinaouchukua sasa wa kuhimiza maandamano yasiyo na kikomo utakisaidia chama hicho kukua kisiasa ama la? Msimamo huo una faida? Hilo ni swali la msingi CHADEMA wanapaswa kujiuliza.
CUF ambao wamo katika muungano wa UKAWA si wajinga kunyamaza na kuwaachia CHADEMA waongoze maandamano.
Kwa CUF huu ni mkakati wa kisiasa unaotokana na miaka ya uzoefu wa siasa za mapambano. Walijifunza kuwa siasa za mapambano hazilipi.
Watanzania wengi wanapenda maendeleo sana lakini wanapenda amani zaidi. Hawa ndugu zangu Waswahili ninaoishi nao huku Magomeni, Dar es Salaam ukiwaambia maandamano ya kudai kuahirishwa Bunge la Katiba wanakuona chizi tu.
Hata marafiki zangu wa daraja la kati, wanaweza kukuunga mkono katika misimamo yako ya kudai serikali tatu lakini maandamano!? No way.

You can say it again!!

kuna tatizo sana tu

CDM tatizo wanajua kila kitu
 
Ingawa umeandika gazeti kwa niayakueleza jambo Moja labda unashindwa kuelewa kuwa maandamano nihaki kikatiba hili nijambo moja jambo la pili watanzania waleo sio wajana au juzi wanauwelewa wahali ya juu kuhusu maendeleo ya nchi yao zunguka Tanzania bara uwone wanasema nini juu ya siasa mwisho kama CCM wanajiamini kwa nini hawafanyi siasa za kiungwana kwenye chaguzi siwanauwakika?
 
Tatizo lililoikumba CUF ni kuwa haikuweza kuvutia wafuasi wapya, nje ya kundi la kijamii ambalo CUF kiasili ina ufuasi. Na hata kundi hilo ambalo CUF kiasili ina ufuasi si lote liliunga mkono chama hicho. Kwa mfano, inaaminika CUF imetaga mayai kusini mwa nchi na maeneo ya pwani, lakini mbona haijafanikiwa kupata wabunge wa kutosha maeneo hayo?
Kwa maoni yangu kulikuwa na tatizo katika taswira ambayo chama hicho kilijijengea kwa umma, taswira ya chama cha kigaidi na fujo. Taswira hii iliogofya makundi fulani ya kijamii. CUF imejaribu kubadilisha taswira hiyo iliyoogofya watu, ingawa ilishawagharimu huko nyuma.
.

Pole sana ndugu yangu,
naona hujuhi au unajifanya hujuhi.

Hivi unaweza nitajia Ubunge wa Upinzani uliopatika kwa Kirahisi bila Ngangari, maandamano na vitisho?

Sasa ulitegemea huko kusini bila kukomaa watapata vipi ushindi?
au hujuhi wnaavyochakachua hata kama umeshinda?

Ndugu tujifunze na tuombe Mungu 2015 vijana nchi nzima wawe majasiri kama walivyo vijanawa Arusha, Ubungo, Kawe,nyamagana na kwingine ambapo ubunge ulipatikana kwa Ngumi , kukesha na mazengwe na sasa basi 2015 watu wote wawe tayari kw alolote kwenye kila Kata na kila jimbo.
 
Katiba mpya . Kura yangu ni mahindi sio mchele
 
Nimeipenda sana mada yako ndugu yangu. Umejaribu kushauri jambo zuri sana lakini huwezi kwenda nje ya ukweli huu. Kumbuka wanaoharibu haiba ya cdm ni ccm kama mshindani wake. Nakuhakikishia kama cuf wasingefanya siasa za ngunguri ua ngangari leo hii bado ccm ingeendelea kufanya wafanyalo huko znz. Lakini nadhani ni ukweli usiotia shaka kwamba cuf sasa wanaheshimika kwa ajili ya siasa hizo. Kwa hapa walipofikia ccm hakuna namna yoyote ya kuendelea na siasa za kistaarabu tena. Ule muda wa kudanganya wananchi kwamba vyama vya upinzani vitaleta vita umepita, nani asiyeona jinsi ccm wanavyofisidi raslimali za nchi hii? Mikataba yote mibovu wameileta hao ccm. Leo hii kwenye uchaguzi tunaona vijana wanaotumiwa na ccm wakipiga watu, kujeruhi na hata kuwaua wapinzani wao huku jeshi la polisi likitumika na bila kuwachukulia hatua ccm. Hizo propaganda za kwamba wapinzani wanaleta uvunjifu wa amani zimetumiwa sana na ccm ili waendelee kubaki madarakani.

Mungu si Athumini, viongozi wengi wa dini walitumika sana kuombea amani lakini kwa bahati nzuri uongo hauwezi kudumu milele. Viongozi wa dini wamekaa chini na kujitafakari nini chanzo nadhani sasa wamegundua ccm ndio tatizo. Na la dhahiri ni kwenye huu mchakato wa katiba. Bila soni wala nini ccm wamechakachukua maoni ya wananchi yaliyokusanywa kisheria na tume ya JSW na wameamua kuandika vifungu vya kudanganya umma eti wameweka haki za wakulima, wafugaji, vijana, wasanii nk huku wakiacha msingi halisi wa maoni ya wananchi. Wananchi wenyewe walitaka rais apunguziwe madaraka kwani taasisi ya urais imetumika kama kichaka cha maovu kwa muda mrefu, ukomo wa ubunge, waziri asiwe mbunge ili awe muwajikabi, kufungua account nje ya nchi, je vifungu hivyo vipo kwenye rasimu hii? Waliotaka katiba mpya ni wapinzani tena sehemu kubwa ikiwa ni hapo kwenye uongozi. Lakini ambao hawakuitaka wameamua kuiandika bila ridhaa ya maridhiano kwa utashi wao na hila ili waendelee kutawala. Nadhani wewe ni shahidi jinsi jeshi la polisi lilivyotumika kukataza maandamano ya wapinzani tena ya amani kupaza sauti zao kuhusu bunge hilo. Viongozi wa dini nao walitaka maridhiano kwanza ndio bunge liendelee, lakini nadhani umeona lugha walizopewa na rasimu iliyoletwa.

Sasa nikuulize katika mazingira haya unadhani bado hao cdm waendelee kujinyenyekeza bila kufanya uasi wa kizalendo? Kwa sababu unaona wanaopiga kelele za amani ndio waliokuwa wanapindisha kanuni za mchezo kila siku ili washinde mechi. Zimewekwa kanuni za mpaka kupiga kura nje ya nchi, idadi kabla ya kupiga kura ilitolewa nyingine na baada ya kupiga kura idadi ikatoka nyingine. Majina ya wapiga kura kisheria yanatakiwa yatajwe je umeyasikia? Wale waliopiga kura za hapana nadhani uliwasikia kwa masikio yako hali gani iliwakuta. Kweli unaweza kusimama ndugu yangu mbele ya hadhara uwafundishe cdm siasa za kistaarabu dhidi ya watu wanaofanya mambo yasiyo ya kistaarabu? Hapa tulipofikia itabidi tufanye uasi ninaouita wa kizalendo maana ni bora tufe kama Yesu msalabani ili wengine wakombolewe. Mikataba yote imekuwa siri na wanaoifanya iwe siri ndio hao wanaojifanya kwamba cdm hawana siasa za kistaarabu, basi hao ccm ambao ni wastaarabu watuonyeshe mikataba inasemaje ndio tupime ustaarabu wao. Kwa sasa tuna kundi kubwa nyuma yetu, akina Jaji Warioba, S. A. Salimu, Jaji Augustino Ramadhani nk. viongozi wa kidini, asasi za kiraia, ukawa nk. Tumeshamjua adui yetu ambaye ni ccm na ni lazima tutamtoa njia tutakayotumia ni ya kistaarabu ya kura. Lakini kwa kuwa tunajua sio wastaarabu tuko tayari kwa njia nyingine ambayo damu zetu bora zimwagike kama Yesu msalabani ili tz ikombolewe. Tumevumilia vya kutosha nadhani sasa hatuna budi kufanya uasi kwa ajili ya taifa letu na hatima ya vizazi vyetu.
 
Back
Top Bottom