CHADEMA wahitaji mabadiliko yafuatayo kuwaokoa 2020 na chama kwa ujumla, enzi za Rais Magufuli

Hisha Sorel

Senior Member
Dec 27, 2017
192
140
Angalia video mpaka mwisho ili kuelewa mtazamo wangu. Mtazamo wako unakaribishwa.

Elewa kwamba mimi si mshabiki wa vyama, bali ni wa maendeleo, ndo maana, mwaka 2015 nilisupport kambi ya UKAWA, ila kwa mwendo wa sasa, nimesuport sera za Rais Magufuli: shangaa sio zote.

Shangaa mafanikio ya uchaguzi wa mwaka 2015, chama cha CHADEMA kimeonekana kupoteza moto. Mpaka ninavyo andika, wabunge wamezidi kuhama chama, pamoja na chaguzi mbali mbali kushindikana.

Ni nini chama kifanye kujioko A: kwenye hii video, nimejaribu, "kiuwepesi", kutaja baadhi ya vitu nionavyo vitakavyo okoa CHADEMA.

TAFADHALI: usi-comment kabla ujaangalia video na kuielewa kiundani: kwani ni vyepesi kupoteza mada.
 
Mkuu ni mawazo mazuri ila ambacho mnakosea ni kwamba sio kama CHADEMA haina sera maana bungeni tumeona wakitoa hoja nyingi tu zinazogusa maisha ya mwananchi ila shida ni hali ya kisiasa ya sasa hairuhusu CHADEMA kuwa frontline na hata wakitokea watu wanaoonekana kuwa na hoja mbadala wananyamazishwa hivyo haya yote uliyoyasema bila mazingira ya siasa kubadilishwa hayatosaidia lolote.... Nakumbuka hata siku halima mdee anachambua bajeti kwenye press conference aliongea mambo ya msingi sana ila aliishia kuwekwa mahabusu kwa uchochezi sasa kwa mazingira hayo ni muda gani basi chama kitatekeleza hayo mawazo yako if at all mazingira haya hayabadilishwi

All in all una hoja za msingi sana ila sijui kwanni hauoni kuwa mazingira ya sasa hayaruhusu vyama kukua zaidi unalaumu chama kinakufa kisa sera zake!! Hivi awamu iliopita kungebanwa hivi unafkiri CHADEMA ingepata umaarufu licha ya kwamba ingekuwa na sera ?? Mawazo ni mazuri ila bila katiba mpya na mazingira ya siasa kubadilika hakuna litakalofanikiwa hapa
 
Nadhani ungesema Tanzania kwanza inahitaji katiba mpya ya wananchi, Katiba ambayo itafuatwa na kila kiongozi au chama ambacho kitashika hatamu ya kutawala.. Ukisema Chadema wahitaji mabadiliko wakati serikali iliyo madarakani imeamua kwa makusudi kufifisha upinzani kwa gharama yeyote, utakuwa huutendei haki mchango wako hapa.. Tuanze kwanza na Katiba mpya ili kuwe na uwanja sawa kwa vyama vyote..
 
Bila shaka amekuelewa
 
Aseee comment of the week....Mabadiliko ni pande zote mbili period!!
 
Point zuri sana. Elewa kwamba mi naongea ki siasa zaidi; siasa ni maonesho: Kama watu hawaoni, hawata kusikiliza. Chadena ya zamani walihua hiki, ndo maana walichagua uniform, maandamano, na hoja na moto kujenga chama. Lakini cha muhimu ni, zaidi ya kuwa na points nzuri ( mia na) mbele ya vyombo za habari; chadema walikuwa na point moja tu mbele ya jamii <mapambano dhidi ya ufisadi>. Hii ni message ambayo ilijenga sura ya chama na kukinyanyua zaidi ya zote. Muonekano ni kila kitu, ndo maana serikali yaweka vikwazo kuzuia hiki. Lakini, kupishana kwa ajenda kila kukicha, kuna zuia kujengwa kwa sura moja. Mi nasema chadema wachague ajenda moja, inayolenga vijana, waiuze tena na tena, waipiganie mwanzo mpaka mwisho. Mpaka wananchi wa kawaida waone, sio wasomi tu.

Ila mi naelewa kwamba, wabunge wa chadema wananyanyaswa na serikali sana; ila hii sio sababu ya watu kuhama: watu wanahama kwasabu wanajua, mipango ya ccm ya miundo mbinu ikizaa matunda itakua vigumu upinzani kuitoa ccm. Bali ni moja ya sababu chama kififia: kwani inazuia chama kutulia na kutoa message moja, mwishoe kupoteza mda kudeal na kesi baada ya kesi, na kutumia influence ya chama.

Zaidi na mabavu; magufuli ni mtaalamu wa siasa. Kila anapoongea message yake ni moja; hategemei bunge kuelezea mipango yake. Sera za ccm, chini za magufuli, ni "consistent"; "simple"; "zinafaamika"; "zinaeleweka"; "zinarudiwa". Hii imeipa ccm sura mpya, na inavutia. Chadema wanahitaji hichi.
 
Hii ni siasa ndugu, CCM wanashinda, hawanashida ya kubadilika, tena mi nasema fomula ta ccm (tofauti na kukamata wanasiasa: hii ni mbaya tena inawaharibia) inafanya kazi ndo maana watu wanahama.

Message moja, ajenda moja, irudie na uirudie na uirudie. Hii fomula inanyanyua ccm, na hii fomula ni ya chadema ya zamani.

Wachague issue kubwa, inayogusa vijana (hili ndo tabaka kubwa la watanzania), wawauzie, na waanza kuipigania "mbele zao", sio tu bungeni.
 
Back
Top Bottom