Ritz
JF-Expert Member
- Jan 1, 2011
- 47,375
- 33,023
Wanabodi.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeendelea kunadi tuhuma badala ya kuwaeleza wananchi juu ya sera zao. CHADEMA inapaswa kuwaeleza watanzania itawafanyia nini wakipata fursa ya kushika dola.
Linalowasikitisha watu makini CHADEMA haiwaelezi wananchi chochote juu ya mema yao au zuri lolote walilonalo wakiwa kama chama cha upinzani. Kinyume chake CHADEMA wameanza kunadi tuhuma wakati Watanzania hawahitaji kujulishwa tuhuma.
Bahati nzuri hizo tuhuma zimewarudia wenyewe wameanza kulipuana wao kwa wao na kutuhumiana wenyewe kwa wenyewe, tayari Arusha, Karatu, Mwanza, Mbeya, Tanga, wameishatimuana. CHADEMA hawakutambua kwamba kwenye uchaguzi kilichokuwa kimewanyima kura ni kutowaeleza Watanzania juu ya mema yao kwamba watawafanyia mambo gani mazuri Tanzania yetu endapo watafanikiwa kuchukua dola.
CHADEMA hawakujua ajenda yao ya ufisadi na mafisadi imepokelewa vipi na wapigakura. Wakaamua kuendeleza vijembe vya uchaguzi huku wakiugeuza upinzani uwe sawa na ukaidi, ubishi, na kusigana ama kubishana na dola.
Kimsingi vyama vya siasa vinashindana na kuzidiana kwa sera na siyo kuzidiana tuhuma.