CHADEMA waanza kumkubali Rais Magufuli

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,375
CHADEMA WAANZA KUMKUBALI RAIS MAGUFULI


MARA

BAADHI ya viongozi na makada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilayani Tarime mkoani Mara wameeleza kuridhishwa na utendaji wa Rais John Magufuli kutokana na ushahidi unaoonekana kwa vitendo katika nia yake ya dhati ya kupambana na ufisadi na kasi katika kutekeleza miradi ya maendeleo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti mjini hapa, walisema imefika wakati wananchi na viongozi kuweka tofauti zao za kisiasa pembeni katika masuala muhimu ya maendeleo kwa taifa ikiwemo kulinda rasilimali za taifa na kuongeza uwajibikaji katika serikali ili kuleta ufanisi katika maendeleo ya nchi.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Uwanja Ndege katika Halmashauri ya Mji wa Tarime, Musa Mgunyi (CHADEMA) alisema kwa sasa jinsi hali ilivyo hakuna sababu ya kutilia shaka uongozi wa serikali iliyopo madarakani, badala yake akawataka wananchi wote bila kujali itikadi za vyama wamuunge mkono Rais Magufuli.

Alisema ingawa alipata ridhaa ya uongozi kupitia CHADEMA, hakuna sababu kwa sasa kuendekeza siasa za mgawanyo wa kiitikadi bali kumuunga mkono rais kutokana na kutetea yale yote ambayo yalipiganiwa na vyama vya upinzani hapo kipindi cha nyuma ikiwa ni pamoja na kupambana na ufisadi.

Chanzo: Mtembezi
 
Ni kweli wote tunamuunga mkono maana mafisadi ambayo yangetumbuliwa na UKAWA kwa sasa anayatumbua Magufuli na karibu yote kama siyo wote ni CCM
 
Babu Duni mwenyewe amesepa....anadai ndani ya CHADEMA kila mtu ni Kambale...hakuna baba wala mtoto, wote wamejaa sharubu na shalafa
 
utawala huu kuupinga unaweza kuupinga ili kuonyesha kwamba na wewe umetoa maoni yako.

lakini kwa uhalisia kwa utawala ambao bado haujamaliza hata miezi sita na mambo ambayo JPM. amefanya anastahili pongezi na kutiwa moyo ili asonge mbele.
 
Mimi hatua aliyoifikia Magufuli pongezi nyingi zinaenda kwa vyama vya upinzani hasa na hasa CHADEMA kiukweli mi naamini hata yeye Magufuli analijua hilo na ndio maana hataki kukosea kwa hilo
 
Mimi hatua aliyoifikia Magufuli pongezi nyingi zinaenda kwa vyama vya upinzani hasa na hasa CHADEMA kiukweli mi naamini hata yeye Magufuli analijua hilo na ndio maana hataki kukosea kwa hilo
Huo ndio ukweli ingawa kwa chumia tumbo siyo rahisi kuukubali
 
Mimi hatua aliyoifikia Magufuli pongezi nyingi zinaenda kwa vyama vya upinzani hasa na hasa CHADEMA kiukweli mi naamini hata yeye Magufuli analijua hilo na ndio maana hataki kukosea kwa hilo
Kama pongezi unazielekeza kwa wapinzani, sasa mbona akina Mbowe na Lowasa wanalialia Magu anapotumbua majipu?
 
Ukumbuke napozungumzia CHADEMA sizungumzii akina mbowe na akina lowasa
Kuna watu walikuwa na wengine bado wamo CHADEMA ambao kiukweli waliiitetea hili taifa kwa nia yao ya dhati pasipo kujali masilahi yao ya umaarufu au kipato
Sio mda wake kuwataja ila nadhani mifano unayo wewe

Nakumbuka jinsi baadhi ya wanachadema wengi waliopoteza uhai kutetea maslahi ta taifa letu

Leo ukizungumzia akina Lowasa mimi naona kama wapo tuuu lakini kuna walioifikisha CHADEMAN hapo ilipo kabla haijapoteza mwelekeo

Na sasa leo Mungu kajibu maombi yao kawapa Magu ambaye ni mwiba kotekote

Na swala la mbowe kuonea huruma wanaotumbuliwa majiblpu mi nadiliki kusema ni UNAFIKI uliokomaa

Ikumbukwe mchezo huo wa kutumbua majipu waliuanzisha wao au sisi nisijitoe,, kwani akina zito walipobainika kwa makosa yale walitumbuliwa na akina slaa nyoote ni mashahidi kwa hilo
 
Kama pongezi unazielekeza kwa wapinzani, sasa mbona akina Mbowe na Lowasa wanalialia Magu anapotumbua majipu?
Presha ya upinzani ndio imewafanya mruhusu akina magufuli, japo inajulikana wazi chama nambari wani hawafurahishwi na Magu maana wanaisoma namba. mwaka jana tu mwezi kama huu mlikuwa mnasifia serikali yenu ya kifisadi, leo mnashangilia kwamba Magu anasafisha, anasafisha uozo gani ambao siku zote mnasifia? wa kusema kwamba kuna angalau usafi unafanyika, ni wale waliokuwa wanasema kwamba kuna uozo. sasa nyie kila siku mnasifia, leo mnasifia usafi unafanyika wakati jana mlisifia kuwa mambo safi, huo ndio ukasuku
 
bara ya CHADEMA wanaonyesha uzalendo na ukomavu wa siasa, kuliko ninyi wanaCCM mliolaaniwa na siasa za Ujima na ubinafsi, mpaka mnamkabidhi mkuu wa mkoa machinga complex badala ya Almashauri ya jiji! Kisa jiji linaongozwa na ukawa?

Mnatia kinyaa kabisa ninyi, kama msipo badilika na kuleta sura ya utaifa badala ya uchama, nakuhakikishia tanzania kupata maendeleo chini ya chama cha mapinduzi itakua ni ndoto za alinacha.
 
bara ya CHADEMA wanaonyesha uzalendo na ukomavu wa siasa, kuliko ninyi wanaCCM mliolaaniwa na siasa za Ujima na ubinafsi, mpaka mnamkabidhi mkuu wa mkoa machinga complex badala ya Almashauri ya jiji! Kisa jiji linaongozwa na UKAWA?

Mnatia kinyaa kabisa ninyi, kama msipo badilika na kuleta sura ya utaifa badala ya uchama, nakuhakikishia tanzania kupata maendeleo chini ya chama cha mapinduzi itakua ni ndoto za alinacha.
Siyo CHADEMA yote inayoonesha ukomavu wa kisiasa, iulize CHADEMA KASKAZINI kama bado haijaifanya mioyo kuwa migumu.
 
Vp wamekubaliana na LUGUMI? Na zile kashfa za February Marope? Km wamekubali sioni sababu ya upinzani.
Huwezi kulishwa na LOWASSA ukasema lolote kuhusu Lugumi, Bashir Awale, Sioi Sumari n.k. kama bado unajipa matumaini kuwa CHADEMA wanapingana na watu hao umeachwa nyuma. Kazi hiyo sasa inafanywa na CCM ikiongozwa na mzalendo JPM.
 
Back
Top Bottom