CHADEMA Vs ACT-Wazalendo

CHADEMA Vs ACT-Wazalendo

GHIBUU

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2011
Posts
4,432
Reaction score
3,016
Nimekuwa nikifuatilia siasa zetu za Tanganyika na Zanzibar toka tumalize uchaguzi mkuu Oktoba 2020, kwanza nimeona mivutano baina ya upinzani na ccm hasa chadema Baada ya uchaguzi kususia kushiriki bunge la jamuhuri ya muungano Tanzania.

Pia nimeona vikao vya ACT-Wazalendo juu ya kutaka kushiriki katika serikali ya umoja wa kitaifa, na mivutano yao ya hapa na pale na kufikia uwamuzi ulio sahihi kwa maslahi ya Taifa la Zanzibar.

Chadema wao nao walikaa kikao na kufikia hatua kwamba kutopeleka wabunge wa viti maalum, ili kutohalalisha sherikali ilio kaa kimabavu kwa kuharibu uchaguzi mkuu.

Nikiangalia utaratibu wa vyama vya siasa, kila chama kina maamuzi yake , na ikumbukwe kwamba this year kulikuwa hakuna umoja wa vyama vya siasa, kila chama kiliamua kusimamisha mgombea wake na kupigania majimbo yao.

Sababu kuu ya ACT kushiriki serikali ya Umoja wa kitaifa.

Unajua Chadema sio kama hawajui sababu za Act kushiki kwenye serikali ya umoja wa kitaifa, wanajua exactly, wanachojaribu sasa ni kupotoa na kuwapoa Watanganyika wanao ipenda ACT Wazalendo.

Siasa za Zanzibar adui yake sio ccm Zanzibar, adui yake ni Muungano, na vikosi vilivyo fanya mauwaji Zanzibar ni vya muungano, na wanafata order za juu kutoka Tanganyika.

Act kushiriki SUK sio kuwaunganisha wazanzibari kama inavyo semwa kwenye mitandao, ita make sense ukisema kuwaunganisha wazanzibari na serikali ya SmZ kwa sababu ipo pale kwa tone la damu.

Bila ya ACt kwenye SUK inaweza Zanzibar Na wazanzibari wakaathirika zaidi awe ccm au AcT kwa sababu sera za Tanganyika huletwa Zanzibar kwenye baraza la Mapinduzi ili zitekelezwe , na moja ya sera hizo ni kuitawala Zanzibar kwa kadiri itakavyo wezekana.

Hivyo ikiwa Act haitishiriki wazanzibari tunaendelea kuumizwa na muungano kwa kuwatumia ccm Zanzibar, hio ndio athari ya wazanzibari.

Lakini Tanganyika hata chadema wakisusia mtaendelea kufaidika nyinyi wenywe, hakuna mzanzibar atakae kuja kuwapangia nini mule nini msile nini mfanye nini msifanye, nyie ndio mabwana.

Waacheni wazanzibari wajenge nchi, ila mjue uchaguzi wa 2020 umeacha makovu makubwa kwa wazanzibari na ile Case ya ICC ni kutaka serikali ya jamuhuri ya muungano na viongozi kuwajibika kwa kuvunja haki za binadamu na sio kudai uchaguzi huru.

Au yupo mtu wa kutueleza maombi ya ICC yana lengo gani ! Ili tuendelee kususia na kutokubali kushiriki kwenye serikali?

Ghibuu
 
Back
Top Bottom