ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,279
- 7,690
Mkuu nadhani kuna wakati tukubaliane kuwa tofauti ya mawazo inajenga. Pia tuangalie mambo kwa upana wake
Kama utamuuliza Alinda hilo swali la mlungula basi pia usiache kumjibu, kwamba, wale wanaosema EL ni fisadi wana evidence yoyote?
Mama Tibaijuka kachukua za mboga, tumeambiwa kimaadili hapaswi. Lakini je, ilikuwa ni jambo pristine?
Tumesikia ya Escrow, kamati zimeundwa. Je, unataka kusema hakuna aliyehusika kwavile tu hakuna ushahidi huo?
Yule mzee aliyegawa kutoka mabenki amefanya hivyo kwa kutumia mikataba. Lakini je, hakukuwa na mziangira ya 'rushwa'?
Point yangu ni kuwa tuangalie mambo kwa mtazamo mpana si kwa kutaka kusikia tunachotaka bali hata tusichokitaka
Mkuu nadhani kuna wakati tukubaliane kuwa tofauti ya mawazo inajenga. Pia tuangalie mambo kwa upana wake
Kama utamuuliza Alinda hilo swali la mlungula basi pia usiache kumjibu, kwamba, wale wanaosema EL ni fisadi wana evidence yoyote?
Mama Tibaijuka kachukua za mboga, tumeambiwa kimaadili hapaswi. Lakini je, ilikuwa ni jambo pristine?
Tumesikia ya Escrow, kamati zimeundwa. Je, unataka kusema hakuna aliyehusika kwavile tu hakuna ushahidi huo?
Yule mzee aliyegawa kutoka mabenki amefanya hivyo kwa kutumia mikataba. Lakini je, hakukuwa na mziangira ya 'rushwa'?
Point yangu ni kuwa tuangalie mambo kwa mtazamo mpana si kwa kutaka kusikia tunachotaka bali hata tusichokitaka
Hao wengine wametoka wapi wakati tunajadili issue ya Dr. Slaa na kuchukua mlungula?
Ndio maana nasema tunakosea kuligeuza jukwaa la great thinkers kuwa sehemu ya propaganda.
Mtu akisema kuhusu escrow muulize kuhusu escrow na ajibu escrow. Lakini mtu anaposema Dr. Slaa kachukua mlungula halafu anapoulizwa anajibu escrow ni ishara ya kutokulitendea haki hili jukwaa.
Nadhani wote tunajuana kwenye majukwaa ya kejeli kuwa tunaziweza, ila sifa mojawapo ya usomi ni kujua kuwa kila kitu na mahali pake. Kwa kutambua hilo ndio maana jukwaa hili likaanzishwa.
Hivi ulitaka kuanzia pg ya 1 mpaka ya 26 tunajadili Dr. Slaa na mlungula? Yaani unataka tustick kwa Dr. Slaa na Mlungula bila kupanua mjadala kwa jinsi mtu anavyoona inafaa? hili ni jukwaa huru kuna watu wenye maona tofauti na kila mtu anandika kwa jinsi anavyoona inafaa..
Mfn wakati sisi wengine mahusiano ya katii ya Gwajina na Lowassa au na Dr. Slaa haikuwa "issue" kwako wewe ulipenda kufahamu undani wa utatu huu.. Hii inaonyesha tulivyo watu totauti na unachokiona kwako wewe hakifai si lazima na kwa mwingine kiwe hivyo hivyo..
kuoanisha tukio hili na lile? Mjadala wa namna hii ulishauona wapi?
Katika jukwaa hili la great thinkers nimesoma for the first time kuwa Dr. Slaa kachukua mlungula. Hiyo ni taarifa muhimu ambayo anayeitoa anawajibika kuwa tayari kuitolea ufafanuzi.
Tafadhali litendee haki jukwaa hili kwa kutoa ufafanuzi. Je, Slaa amechukua mlungula toka kwa nani?
Nimekuuliza hivi kama Dr. Slaa anakula mihogo hela ya kurushwa press yake alilipiwa na nini? Na je huyu aliyemlipia hakumpa hela (mlungula) wa kununua mkate?
ZeMarcopolo kuna jambo hapa nadhani ni la kitaifa, hebu tulitendee haki taifa kwa muda
Sitta ananukuliwa na Alinda akiwa Tabora na kusema 'EL ni fisadi kaleta kampuni feki na hadi sasa tunalipia gharama kubwa za umeme''
Kwakweli alichosema ni jambo zito kwasababu kama taifa linaumia kwa ajili ya mtu ,ni jambo la kuangaliwa sana
Turudi upande wa Pili. Kumbu kumbu zinaonyesha suala hilo liliibuka tena bungeni. Mwakyembe akamuomba Sitta kama Spika lifunguliwe na kujadiliwa tana. Kumbu kumbu zinaonyesha Spika Sitta kwa wakati huo akakataa lisijadiliwe
Kumbu kumbu zinaonyesha ziliundwa kamati za kwenda undani wa jambo hili. Hadi leo hatujui matokeo ya kamati hizo
Sasa naomba maoni yako kuhusu hili. Je, kauli ya Sitta inaonyesha ukweli wowote tukizingatia kuwa naye alikataa kulisaidia taifa kwa hoja kurudishwa na Mwakyembe? Nini mtazamo wako kwa ujumla wake
Alinda unaweza kutusaidia clip ili mkuu atupe mtazamo wake?Mkuu, kipindi hiki cha kampeni kunakuwa na matukio na kauli nyingi. Bado sijapata fursa ya kusikiliza alichosema Sitta Tabora, kwa mantiki hiyo siko kwenye position ya kuweza kuitolea tamko kauli hiyo ya Sitta.
Mkuu, kipindi hiki cha kampeni kunakuwa na matukio na kauli nyingi. Bado sijapata fursa ya kusikiliza alichosema Sitta Tabora, kwa mantiki hiyo siko kwenye position ya kuweza kuitolea tamko kauli hiyo ya Sitta.
ZeMarcopolo kuna jambo hapa nadhani ni la kitaifa, hebu tulitendee haki taifa kwa muda
Sitta ananukuliwa na Alinda akiwa Tabora na kusema 'EL ni fisadi kaleta kampuni feki na hadi sasa tunalipia gharama kubwa za umeme''
Kwakweli alichosema ni jambo zito kwasababu kama taifa linaumia kwa ajili ya mtu ,ni jambo la kuangaliwa sana
Turudi upande wa Pili. Kumbu kumbu zinaonyesha suala hilo liliibuka tena bungeni. Mwakyembe akamuomba Sitta kama Spika lifunguliwe na kujadiliwa tana. Kumbu kumbu zinaonyesha Spika Sitta kwa wakati huo akakataa lisijadiliwe
Kumbu kumbu zinaonyesha ziliundwa kamati za kwenda undani wa jambo hili. Hadi leo hatujui matokeo ya kamati hizo
Sasa naomba maoni yako kuhusu hili. Je, kauli ya Sitta inaonyesha ukweli wowote tukizingatia kuwa naye alikataa kulisaidia taifa kwa hoja kurudishwa na Mwakyembe? Nini mtazamo wako kwa ujumla wake
Mkuu ZeMarcopolo nadhani tutendee taifa haki. Nukuu yangu ya hoja hapo juu sasa unaweza kuijadiliMkuu, kipindi hiki cha kampeni kunakuwa na matukio na kauli nyingi. Bado sijapata fursa ya kusikiliza alichosema Sitta Tabora, kwa mantiki hiyo siko kwenye position ya kuweza kuitolea tamko kauli hiyo ya Sitta.
Jamani maana na great thinkers ni nini? uliposema Lowassa ni mtoa rushwa ulimkamata akitoa rushwa? si unatumia akili zako kujua kile na kile kinatokea hiki au!!Hiyo Richmond nikikuuliza Lowassa alijigawai sh. huna jibu,
Ninachoandika ninaandika mawazo yangu na maono yangu, Sasa wewe ukiona kuwa haviendani na jukwaa hili ni sawa na ni haki yako.. Siwezi kuandika kilichomo kichwani mwako au unachotaka kusikia kwa sababu mimi siko kichwani mwako na sijui unataka kusikia nini..
Umeuliza Gwajima nimekujibu jinsi nilivyoelewa...
Mlungula wa Dr. Slaa nitakuuliza hili swali..
Hivi Dr. Slaa pesa za kuitisha press alizitoa wapi hali alituambia kuwa anashindia mihogo? Sasa kama waliweza kumlipia Press kwa vyombo vyote walishindwa kumpa hela ya kula walau mkate?
My two cents;
Wachangiaji wote humu kwenye jukwaa, hakuna hata moja anayeongelea kiini cha matatizo yaliyotufikisha hapa tulipo nacho ni haki. Imefikia mahali wengi mnaona tendo la kukosa haki ama kunyimwa haki ni la kawaida tu kama sehemu ya maisha. Mnachosahau ni kwamba bila haki hakuna amani, haki hujenga ustaarabu na hivyo kuwezesha maisha kuendeshwa kiutaratibu kwa kufuata sheria.
Ukosefu wa haki hustawisha uonevu kwa mnyonge na kumjengea kiburi mwenye nguvu, kiburi ambacho bila kudhibitiwa hufungua milango ya uhalifu wa aina zote. Binadamu kwa hulka yake hakubali uonevu na ingawa anaweza akavumilia uonevu kwa muda, iko siku uvumilivu wake utafikia mwisho. Hakuna kiumbe hatari kama binadamu anapofikia hali hiyo ya kukata tamaa ya maisha.
Watu mnaongea kama vile uwanja wa ushindani kisiasa upo sawa, mnaongea kama vile uchaguzi ujao, kama zilizopita, utaendeshwa kwa uhuru na haki na mnaongea kama vile vyama vyote vitakayoshiriki vina haki sawa na chama tawala. Manongea kama vile hamuishi Tanzania, mnaishi nchi nyingine tofauti...nchi iliyostaarabika na inayoheshimu misingi ya utawala unaofuata sheria.
Siku Dr. Slaa alipoongea, aliondoa mashaka yote yaliyokuwa moyoni mwangu kuhusu kuteuliwa kwa Lowassa kugombea Uraisi na UKAWA kupitia chama cha Chadema. Mwanzoni, pamoja na kutaka CCM iondoke, nilipokea uteuzi huo shingo upande kidogo nikisubiri msimamo wa Dr. Slaa...naam, nilimsikiliza kwa makini sana na baada ya kumsikiliza sikuwa na wasi wasi tena, UKAWA walikuwa sahihi.
Kauli zinazoendelea kutolewa na viongozi na wafuasi wa CCM si kauli za kiungwana, ni kauli za walevi wa madaraka,kauli za waliojawa kiburi na kauli zisizo na chembe cha ustaarabu...naam ndiko walikotufikisha CCM na kama Lowassa atatusaidia kuondokana na kadhia na manyanyaso haya ya miaka 50 naunga mkono. Dr. Slaa nitaendelea kumheshimu lakini kwangu hapa kapotoka.
Sitaki kuingia ndani sana kwenye swala la Dr. Slaa kwani ni moja katika watu niliokuwa na imani kubwa nao lakini kwa kitendo chake ameonesha ama hakuwa tayari kwa mabadiliko au alijiaminisha bila yeye mabadiliko hayawezekani. Ninachoomba ni wananchi wapewe haki na wawe huru kumchagua watakaye. Serikali isitoe upendeleo kwa CCM bali itoe fursa sawa kwa vyama vyote vinavyoshiriki.
Ndugu zangu, gari (Tanzania) limekwama, limegota kwenye tope...Magufuli anataka kulinasua kwa kulisukuma bila kutoka ndani ya gari, Lowassa kavua buti katoka kwenye gari alisukume. Nawaacha na usemi huu, adverse circumstances need desperate measures...kama hakuna upepo wa kusukuma boti, dawa si kusubiri upepo bali ni kupiga makasia. UKAWA wanapiga makasia.
Leo nimemsikiliza tena Dr.Slaa Star Tv, nimezidi kuwa confused, yaani bora hata angekaa kimya, most of the time anakwepa hoja za msingi, mara nina moyo wa nyama toka February chama changu kiliniandaa kugombea uraisi na mpaka ziara za nje, mara nasimamia misingi, mara ubunge karatu au kinondoni, duuu mm sijamuelewa kabisa.
labda nimsubiri mwalimu wangu Nguruvi3 aje anipe roadmap sijaelewa kabisa.
Zakumi kuna tofauti kubwa sana kati ya kuiondoa CCM na kumuondoa Lowassa. Nataka kwanza tulivunjilie mbali hili kambi la mafunzo linalotuzalishia viongozi hao...Mwinyi alitoka akaingia Mkapa, akatoka Mkapa akaingia Kikwete. Wakati sisi tunahangaika na taasisi, wewe na wengine wengi tu mmeamua kuhangaika na individual...mimi sihangaiki na individual, nahangaika na institution.Mag3;
Nakuelewa na nakubaliana na wewe kuwa kuvunjwa kwa haki ni msingi wa matatizo mengi. Wazazi wetu walipodai uhuru, walidai haki zao. Hawakudai kuwa matajiri.
Hivyo haki ni msingi wa taifa. Na hatuwezi kusema kuwa haki ni msingi wa taifa na maisha iwapo hatutakuwa wakweli. Hili ndilo tatizo nililonalo mimi na ndugu Lowassa. Kwetu Morogoro kachukua ranchi. Ndani ya ranchi hiyo walikuwa wanakaa watanzania wenye kufanya shughuli za kujikimu. Kawafukuza na kujengea uzio. Tena wengi walioathirika ni wananchi wa jamii ya kimasai waliohamia Morogoro miaka ya 70. Niambie huyu mtu anaijua haki toka lini?
Niambie huyu mtu ataleta mabadiliko gani iwapo kwa like kidogo alichojinyakulia hakuweza kufanya hivyo? Ni kweli ni mtoaji wa vibahasha. Lakini hanavitoa kwa kujipatia yeye umaarufu na sio kunyanyua maisha ya wananchi au kupigania haki zao.
Mimi ni mtafuta ukweli. Katika uchaguzi huu sioni ukweli wowote zaidi ya vichekesho. Kama Lowassa atasaidia kuindoa CCM, hicho ni kitu kimoja. Lakini baada ya hapo na yeye awe njiani. Kwanini upende nusu kamili, wakati kamili inawezekana.
Zakumi kuna tofauti kubwa sana kati ya kuiondoa CCM na kumuondoa Lowassa. Nataka kwanza tulivunjilie mbali hili kambi la mafunzo linalotuzalishia viongozi hao...Mwinyi alitoka akaingia Mkapa, akatoka Mkapa akaingia Kikwete. Wakati sisi tunahangaika na taasisi, wewe na wengine wengi tu mmeamua kuhangaika na individual...mimi sihangaiki na individual, nahangaika na institution.
Naomba nikuulize swali moja Zakumi, unadhani ni kwa nini ndani ya CCM ghafla bin vuu, adui nambari one amekuwa Lowassa? Ni kwa sababu Lowassa ni threat kwa institution, he was once part of it but now he is on the other side na hili CCM walilijua toka kitambo na kujiweka tayari. Ambacho hawakutilia maanani ni kiu ya mageuzi waliyo nayo Watanzania...CCM siyo tu kwa sasa haipendwi, inachukiwa.
CCM kwa hulka yake ime declare an all out war against opposition kwa kutumia silaha yoyote ile na zozote zile na moja wapo katika silaha hiyo ni mtu moja vulnerable kwa jina Dr. Slaa. He will soon wake up out of his slumber and slowly realize kwamba Watanzania wa sasa si wale wa 2010, this is a completely new breed. Bila kujua Dr. Slaa anaijeruhi CCM kuliko Lowassa or UKAWA for that matter, mark my words.