Wanajamvi tunalirudia bandiko hili kwa makusudi zaidi ilimjadala unaofuata punde ueleweke.MBINU NA CHANGAMOTO ZA CHAGUZI
Chaguzi huambatana na mbinu , mikakati na changamoto
Chaguzi huwa na makundi ya wapiga kura. Kwa hali ya kisiasa yapomakundi yafuatayo
(1) Kundi linalopiga kura ya hasira- hili ni lile lisilo naupande, lilichoshwa na hali iliyopo
(2)Kundi la wanachama watiifu, hili linachagua tu kutokanana vyama iwe ni CCM, UKAWA au kingine
(3) Kundi lenye mashaka- hili halina uhakika lisimame wapi namara nyingi huangalia hoja ingawa si jambo linalotazamwa sana ukilinganisha na personality
CCM inategemea makundi 2 na 3 kwasababu tayari ni mwathirika wa kundi la 1
Wapinzani wana ‘advantage' ya makundi yote. Ushindani upo kundi la 3 litakaloamua nani anashinda majimbo au dola
Wapinzani kama ilivyo kwa CCM, wana ‘disadvantage'.
Kwanza, uwezowa kufikia jamii una vikwazo tukijua CCM ina mtandao wa wakuu wa mikoa na wilaya na rasilimali za umma.
Pili,CCM wanaserikali inayomiliki vyombo muhimu.
Mfano, zipo taasisi za nishati zinazolalamikiwa kutotenda haki kwa maagizo ya serikali ili kuwanyima wananchi habari
Vyombo vya habari vinavyoegemea CCM, na vyombo vya dola kutumika vibaya
Ushindi hautaamuliwa kwa hesabu za kura, yapo mengine ambayo kama hayataangaliwa yatabadili mwenendo wa uchaguzi
Kwa mfano,hatujawahi kupata majibu ya kwanini watu wajiandikishe kwa asilimia 70 , wapiga kura wawe asilimia 30.
Kuna nini kinaendelea ambacho serikali au tume ya uchaguzi imeshindwa kubaini?
Mfumo wa pili , BVR, je, umehakikiwa kufanya kazi kamailivyokusudiwa?
Kukiwa na matatizo ya kifundi au ‘kufundwa' itakuwa ni kwa maumivu ya wapinzani
Lipo suala la ‘voters suppression' kusudio ni kuzuia watu wasitumie haki ya kura kwa udanganyifu kama ule wa 1995 watu walipoambiwa siku ya kwanza ni CCM na ya pili wapinzani
Au inaweza kuwa vitisho kwa wapiga kura (2010) kwa jeshi kutoa tamko, au kutumika nguvu za dola kwa namna yoyote.
CCM wanakiri hali ngumu inayowakabili. Istegemewe CCM itatoa dola au bunge au vyote katika kisahani cha dhahabu.
Itapigana hadi tone la mwisho ikitambua kuwa KANU imetoweka kama ilivyo UNIP
Kitakachosaidia wapinzani ni ushindi usio na shaka ‘decisive victory'.
Itawezekana wakijiweka vema kupambana na hila, kukabiliana na hoja, kujenga hoja na kujibu hoja.
Kuzuia uharibifu kwakushambulia na si kujilinda ni muhimu kwao.
Kuwepo na uthubutu ‘courage' ya kupambana na changamoto si chaguo ni lazima kwa wapinzani
Tusemezane
Alinda , kinachotokea ni mtihani wa demokrasia ambao nchi yetu haijawahi kukumbana nao.Kinachoendelea Mwanza kama ni kweli basi ninaanza kuwa na wasi wasi na uchaguzi wa mwaka huu, endapo NEC wataamua kufanya uchakachuaji kama walivyozoea.
Picha: Mwanza usiku vijana wakikesha kumlinda Lowassa.
Sina uhakika kama hawa watu wanampenda Lowassa sana, si uhakika kama wanampenda Mbowe au viongozi wa Chadema/Ukawa sana na si kwamba Lowassa ua viongozi wa Ukawa wako kwenye hatari hivyo wanawajibu wao kuwalinda BALI kitu ambacho nina uhakika nacho ni kuwa hawa watu wanataka mabadiliko, hawa watu wamechoka na matusi, manyanyaso, kejeri, dharau, kuitwa ni wanywa viroba, kukosa thamani katika nchi yao, kuwa daraja la tatu katika nchi na nk. Hivyo wanachotaka ni mabadiliko nani alete mabadiliko na ni mabadiliko yapi kila mtu ana ndoto zake kichwani na kwa hizi ndoto zao hawako tayari kusubiri miaka 5 tena bali wanataka sasa..
Ni wajibu wa tume ya uchaguzi kusoma alama za nyakati, na kuandaa mazingirai mazuri ambayo yatatoa haki bin haki kwa pande zote mbili yaani chama tawala na vyama vya upinzani la sivyo tujiande kwa nchi yetu kumwaga damu.. Huu ndio ukweli ambao tunapaswa kuusema.
Mkuu hili swali ni gumu kwa kuzingatia kuwa hatujui nini kinaendelea na mapungufu ya habariMkuu Nguruvi3 nini matarajio yako kwa post namba 251 je tume itafanya yanayotegemewa? Yaani haki au itaendelea na staili yake ya kusikiliza aliewachagua?
Kuhusu kudai tume huru ya uchaguzi, hili suala lina sura nyingi kidogoJe huoni kama vyama vya upinzani kwa kuchelewa kudai tume huru kama Kenya ni kosa? Kama ni kosa kwa muda huu tutarajie huruma au uwajibikaji usio egemea upande mmoja ambao ni ngumu. Nini ni way forward kwa hapa tulipo?
Adharusi , kwanza nimefikiria kwanini umekuja kwa njia uliokuja nayo, sijapata jibuAlinda " Ni wajibu wa tume ya uchaguzi kusoma alama za nyakati, na kuandaa mazingirai mazuri ambayo yatatoa haki bin haki kwa pande zote mbili yaani chama tawala na vyama vya upinzani la sivyo tujiande kwa nchi yetu kumwaga damu.. Huu ndio ukweli ambao tunapaswa kuusema."
Hivi ALINDA hii damu unayoisemwa tujiandae kuimwaga ni ya binadamu au mbuzi?
tumwage damu sababu ya madaraka au,tufanye damu imemwagika watanzania wote wamekufa,wamebaki wanao ishi NJE YA Tanzania,itakua imekusaidia nini wewe na wenzako mnao tamani damu imwagike kisa madaraka,
ishu ya amani ni ya vyama vyote,alianza Mbowe kusema uchaguzi mwaka huu hautafanyika,hivyo damu itamwagika,ajatuomba radhi mpaka sasa watanzania
UTANZANIA WETU NI BORA KULIKO VYAMA VYETU
vyama vyote na viongozi wao na wafuasi wao wajiepushe na kauli za uchochezi,upinzani na CHAMA tawala
Mungu ibariki Tanzania
Alinda " Ni wajibu wa tume ya uchaguzi kusoma alama za nyakati, na kuandaa mazingirai mazuri ambayo yatatoa haki bin haki kwa pande zote mbili yaani chama tawala na vyama vya upinzani la sivyo tujiande kwa nchi yetu kumwaga damu.. Huu ndio ukweli ambao tunapaswa kuusema." Hivi ALINDA hii damu unayoisemwa tujiandae kuimwaga ni ya binadamu au mbuzi? tumwage damu sababu ya madaraka au,tufanye damu imemwagika watanzania wote wamekufa,wamebaki wanao ishi NJE YA Tanzania,itakua imekusaidia nini wewe na wenzako mnao tamani damu imwagike kisa madaraka,ishu ya amani ni ya vyama vyote,alianza Mbowe kusema uchaguzi mwaka huu hautafanyika,hivyo damu itamwagika,ajatuomba radhi mpaka sasa watanzania
UTANZANIA WETU NI BORA KULIKO VYAMA VYETU,vyama vyote na viongozi wao na wafuasi wao wajiepushe na kauli za uchochezi,upinzani na CHAMA tawala
Mungu ibariki Tanzania
Hivi wewe uwe unasoma na kuelewa maana nzima ya mstari au maana mzima ya paragraf? au unasoma neno moja na kulitungia maana unayoelewa wewe?
Vijana (kwa maandishi nategemea kuwa wewe ni kijana) mstaki kukaririshwa kama watoto wadogo, jifunzeni kusoma na kuelewa nini dhana mzima ya andishi fulani, wakati mnasoma kitu/ jambo fulani jaribu kulinganisheni mnachokisoma/kiona na hali halisi ya maisha yako au maisha ya watanzania kwa ujumla ukifanya hivyo utaona mantiki nzima ya kitu au jambo linalosemwa.
Hivi kwa akili uliyojaliwa na mwenyezi Mungu kusema "kama haki hisipotendeka kuna uwezekano wa kumwaga damu ni uchochezi? Ni uchochezi wa nini na wa nani kwenda kwa nani?
Je ni kweli haki zinatendeka ktk changuzi zetu? na kama haki hazitendeki unachoshauri ni nini? watu wakae kimya wakiangalia baadhi ya wataule wakisigina haki zao? au watu wapaze sauti zao? na je unafahamu watu wakipaza sauti zao ni nini kinachotokea?
Labda nikupe mfn kidogo tu labda utaelewa ninachomaanisha:
Je unakumbuka 2010 "boss" wako Zitto alitiwa ndani baada ya kuilazimisha tume kutangaza matokeo kama yalivyo?
Je hapo kwa akili zako ni nani mchochezi ni Zitto aliyetaka haki itendeke au ni tume ya uchanguzi uliyotaka kutangaza matokeao jinsi watakavyo wao?
Pia kwani watanzania kumwaga damu ni mara ya kwanza? Si ulisikia kiongozi wako mkuu akisema "wakati wanakigoma wakipigwa mabomu watu wa Arusha Iringa walikuwa wanakumbatia watawala! Labda nikuulize je hiyo damu uliyomwagika miaka ya 1990 huko mkoani Kigoma ilikuwa ni damu ya Mbuzi au ya binadamu? Na je hii damu ilimwagika kwa ajili ya madaraka au kwa ajiri ya kutaka haki sawa?
Hakuna ninachochukia kuona kijana kama wewe mtu ambaye ungekuwa mstari wa mbele kutaka haki sawa, kupigania haki zako, haki za watoto wako, haki za mkeo, haki za wazazi wako, unalishwa propoganda tena propoganda unazolishwa unalishwa na mtu kama Nape na wewe hauhoji bali unazitafuna na kumeza huu ukigawia watoto wako(km unao).
Nitapenda ujibu hayo maswali maana wewe unafahamika kwa "kusepa"
Wewe mwanamke sijui Zitto alikukosea nini daah!!!.Hivi wewe uwe unasoma na kuelewa maana nzima ya mstari au maana mzima ya paragraf? au unasoma neno moja na kulitungia maana unayoelewa wewe?