Chadema twendeni mahakamani kudai haki yetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema twendeni mahakamani kudai haki yetu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by makoye2009, Nov 5, 2010.

 1. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #1
  Nov 5, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Hili swala la CCM,NEC,UWT(Usalama wa Taifa) KUCHAKACHUA matokeo ya kura za Urais na Ubunge liko wazi kabisa na ushahidi upo.

  Mifano halisi ni ucheleweshaji wa kutangaza matokeo kwenye maeneo yenye nguvu kubwa ya Upinzani hasa CHADEMA. Hii haikutokea kwa bahati mbaya ni MAKUSUDI. Angali kilichotokea Dar,Arusha,Mwanza,Mbeya,Shinyanga na maneneo mengine mengi.

  Majimbo ya Nyamagana,Ilemera,Arusha Mjini,Karatu,Shinyanga Mjini kura zake mpaka jana Usiku NEC walikuwa bado HAWAJAZIJUMLISHWA KWENYE IDADI YA KURA ZA DR.SLAA KWA MAKUSUDI wakti tayari wasimamizi wa majimbo walizitangaza kwa SHINIKIZO ZA WANANCHI. Nec wamefanya kusudi kuchelewesha kujumlisha ili Kiwete aonekana kuwa anaongoza kwa mbali.

  HAINGII AKILINI MTU UMPIGIE KURA MBUNGE WA CHADEMA HALAFU KURA YA URAIS UMPE MGOMBEA WA CCM KIWETE. MTU UNACHAGUA SERA ZA CHAMA SIYO MTU. MIFANO:

  JIMBO: CHAMA: UBUNGE: RAIS:

  ARUSHA MJINI CHADEMA......................56,208.......................54,208
  CCM.............................36,107.......................39,107

  MBEYA MJINI CHADEMA......................46,411........................42,917
  CCM.............................24,236........................32,249

  MWANZA-NYAMAGANA CHADEMA......................38,171.........................30,991
  CCM.............................27,883.........................32,320


  MWANZA-ILEMERA CHADEMA.......................31,256..........................29,701
  CCM..............................26,870.........................29,143

  MASWA MAGH CHADEMA........................17,456.........................11,742
  CCM...............................12,824.........................17,104

  MASWA MASH CHADEMA........................17,075.........................12,203
  CCM...............................17,014.........................21,150


  Mpaka sasa ukiingia kwenye WEBSITE YA TUME: http:/www.nec.go.tz Bado KURA HIZO HAZIONEKANI KWENYE MTANDAO. KWANINI HAWATAKI KUZIJUMLISHA? WANOGOPA NINI?

  Soma hizi nukuu toka Gazeti la MWANANCHI toleo la leo 5/11/2010:

  ''..............Nao wasomi wameungana na madai ya Dk Slaa wakisema kuwa uchakachuaji matokeo ya kura nchini umekuwa aibu kwa taifa.
  Wakizungumza kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam jana, wasomi hao walisema kuna dalili zinazotia shaka kwamba matokeo ya urais yamechakachuliwa kwa kuwa hawaoni sababu kucheleweshwa kutangazwa.
  “Tunajua kuwa hata kama CCM ingeshinda, isingeshinda kwa kura nyingi kiasi hicho. Kwa nini tumsifie mtu kuwa ameshinda kwa kishindo na huku amechakachua matokeo?”alisema Dk Fairles Ilomo, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tumaini, Iringa.
  Dk Ilomo alisema haiingii akilini kuelezwa kuwa matokeo yamechelewa kutangazwa kwa sababu ya matumizi ya kompyuta katika hatua ya kuhesabu kwani wakati wa upigaji, wananchi hawakutumia kompyuta.

  "Kwanini matokeo yasubiri kompyuta? Hakuna logic (mantiki) kusema kuwa kuingiza data kwenye kompyuta kulisababisha ucheleweshaji maana hata uchaguzi wa Marekani, walitumia kompyuta na matokeo yakawahi kutolewa," alisema Dk Ilomo.
  “Ni kweli uchaguzi ulifanyika vizuri na kulikuwa na amani lakini katika hatua ya kuhesabu kura na kutangaza matokeo kulikuwa na uchakachuaji hasa katika maeneo nyeti.
  “Rais aapishwe, lakini Dk Slaa ana haki ya kuendelea na malalamiko yake. Kama malalamiko hayo yakionekana yana ukweli, maamuzi mengine yafuate."

  ..............Mhadhiri mwingine chuoni hapo Harod Tairo alisema amestuka kuona matokeo hayo yanaonyesha kuwa watu wengi wamewapigia kura wabunge wa Chadema lakini si mgombea wake wa urais, yaani Dk Willibrod Slaa
  “Mimi naamini kwamba wabunge wengi wa Chadema walichaguliwa kwa juhudi za Dk Slaa. Wananchi hawawezi kuchagua mbunge wa Chadema halafu rais wamchague wa CCM. Mimi naona matokeo hayaakisi halihalisi,” alisema Tairo.

  Hawa wasomi na Wahadhiri naungana nao kwa 100%.
   
 2. Avanti

  Avanti JF-Expert Member

  #2
  Nov 5, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 1,209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hiyo idadi ni ya kweli na inawezekana kabisa but I wl not comment further on this, ila tu kwa utafiti wa haraka kwa kuwa hata Bukoba mjini CCM walishinda Ubunge lakini Uraisi kachukua Chadema, je hapo tunaweza sema Chadema walichakachua ya Uraisi?
   
 3. kalagabaho

  kalagabaho JF-Expert Member

  #3
  Nov 5, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,276
  Likes Received: 2,059
  Trophy Points: 280
  "HAINGII AKILINI MTU UMPIGIE KURA MBUNGE WA CHADEMA HALAFU KURA YA URAIS UMPE MGOMBEA WA CCM KIWETE. MTU UNACHAGUA SERA ZA CHAMA SIYO MTU".  Binafsi Urais nimempa wa chama kingine na ubunge wa chama kingine kwa hiyo, hiyo sio sababu cha muhimu ni kuangalia nani anaweza kusimamia ahadi zake tuu! Acha kuwasemea watu, kila mtu ana akili na maamuzi yake! kisichoingia akilini kwako wewe kinaweza kuingia kwa mwingine!
   
Loading...