Ufipa-Kinondoni
JF-Expert Member
- Jan 3, 2012
- 4,582
- 2,783
Ni lazima tuseme na hakuna wa kutunyamazisha.
[Na ahidi tarehe ya kuja kwa Lowassa CHADEMA kuleta andiko la Malengo makuu ya SUMAYE na LOWASSA].
Ni kama chama kimekosa mwelekeo, kinawayawaya. Kinaendeshwa na kila anayejisikia. Hakuna mipango, hakuna msimamizi wa mipango na hakuna vikao vya kimaamuzi. Ni wakati wa kusema tunahitaji chama kirudi kwenye msingi yake. Msemaji wa chama yupo?
Nimeona sahizi tumegraduate na kuwa chama cha siasa. Wawakilishi wetu wameambiwa, waanze kufanya kazi na waache siasa na kuzuia kazi za serikali. Hili nakubaliana nalo. Ila naona linapingana na kauli ya Mbowe ya Madiwani kutoshirikiana na serikali. Na ndo ile imetokea kwa Meya wa Kinondoni akitekeleza agizo la chama. Leo ataficha wapi uso wake baada ya kupata agizo jipya??? .
Sijajua viongozi wa ngazi za chini za chama na mabaraza yake yanafanyia kazi kauli za nani.
Mbowe anasema, Lowassa anasema!!!!!
Nani kiongozi wetu hapa Ufipa? Nani msemaji wetu hapo? Matamko na maelekezo ya kuendesha chama yanatoka kwa nani? Hakika miluzi mingi humpoteza mbwa. Ndo kinachotokea. Tunahitaji msimamo wa chama kabla muda haujaisha wa kuponya vidonda vikubwa zaidi.
Mwenyekiti upo? Katibu upo? Au ndo kauli na ubashiri wa Lowassa kuchukua chama umetimia?
Kwa leo nitaishia hapa.