Kada wa CHADEMA
JF-Expert Member
- Feb 27, 2016
- 289
- 616
CHADEMA tumekosea sana na tunaendelea kukosea. Tumemkosea Rais Magufuli na tumewakosea Watanzania. Tuna wajibu wa kumuomba radhi Rais Magufuli na Watanzania kama tunataka kufika salama 2020.
Tanzania ilioza sana. Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ally Hassan Mwinyi hakukosea aliposema kuwa nchi inaenda kama gari bovu. Hakukosea na msimamo wake ni valid hata leo kutokana na matukio yafuatayo;
1. Kukithiri kwa vyeti feki hasa kwenye ajira Serikalini
2. Uwepo wa wafanyakazi hewa
3. Ufisadi, wizi na ubadhilifu wa mali za umma
5. Usimamizi mbovu wa rasilimali za nchi na kusababisha madini kusafirishwa nje ya nchi kama mchanga usio na thamani
6. Uzembe kazini
7. Miundombinu mibovu
8. Kasi ndogo katika uwajibikaji kwenye sekta ya umma
9. Kufa kwa mashirika ya umma kama TTCL, ATCL, TRL nk.
10. Safari za nje zisizo na tija kwa taifa nk.
Thanks God. Kamleta mtu wa kuweza kututatulia matatizo hayo. Tena kajitolea kwa moyo thabiti na bila kuogopa. Cha kushangaza sisi kama chama kikuu cha upinzani tunajitokeza na kupambana naye. Mbaya zaidi si kwamba tunapambana kwa hoja bali vioja. Watanzania wanatushangaa na dunia nzima inatushangaa.
Ka hii aibu tunayolitia taifa letu, tuna wajibu mkubwa wa kuungama kwa Mwenyezi Mungu na kumuomba radhi Rais Magufuli. Kinyume cha hapo mjue kuwa tunapoteza kila kitu kwa maana laana ya Mungu itakuwa miguuni mwetu.