CHADEMA, Tunataka Moshi liwe JIJI

Kwa Tanzania mi naona kuitwa jiji is just a name, nothing special. Kuna manispaa zimeitwa jiji hazina miundombinu ya kueleweka mfano hakuna double road hata moja.
 
Mangi una wasiwasi gani na kilimanjaro ni jiji kiuhalisia kwa maana ya kipato na elimu ya mtu mmoja mmoja
 
Kwa moshi inawezekana umetoa wazo nzuri litafanyiwa kazi
 
Jiji linalofuata ni Dodoma,


Moshi bado washamba sana kuwa jiji
 
Moshi iwe jiji 🙄🙄🙄 😱 😛😀

Hivi inashangaa nini? Mkoa kama Mbeya ni jiji ukiachana na kigezo cha population haufikii moshi hata Robo.

Kwanini moshi isiwe jiji?
 
hivi faida ya kuwa jiji ni ipi, au jina tu kwamba moshi ni jiji..
kwa mfano tokea Tanga na Mbeya zimekuwa majiji wao wamepata faida gani ambayo wasingeipata kama wasingekua jiji..
 

Ili kufanikisha azma hii inabidi:
1. Mipaka ya sasa ya manispaa ipanuliwe kwa makubaliano maalum na H/shauri za Moshi (V) na Hai
2. Kuhamisha watu na kuwalipa fidia - maeneo kama ya Boma mbuzi, kwa Mtei, Relini kuelekea Njoro nk yako eneo la manispaa ila nyumba hazikidhi mahitaji ya wakati, na nyingine zimejengwa kwenye viwanja visivyopimwa bila mpangilio!
 
Kumbe Ibilisi naye hunena yale yampendezayo muumba!!!
Viongozi msisahau pia Moshi ilichelewa sana kuwa manispaa.Sababu kubwa ni hcho kigezo cha idadi ya watu.Moshi watu wengi huja kazini asbuhi na kurudi majumbani Hai,Moshi vijijini na Hata Arusha na Rombo.Sensa zetu hufanyika J2 hhivyo wafanyakazi wengi wanakuwa majumbani ndiyo maana Moshi huonekana na wakazi wachache.
 
Kwa Tanzania mi naona kuitwa jiji is just a name, nothing special. Kuna manispaa zimeitwa jiji hazina miundombinu ya kueleweka mfano hakuna double road hata moja.
Hasa jiji la tanga, yani kumepoozaa
 
hivi faida ya kuwa jiji ni ipi, au jina tu kwamba moshi ni jiji..
kwa mfano tokea Tanga na Mbeya zimekuwa majiji wao wamepata faida gani ambayo wasingeipata kama wasingekua jiji..
Bajeti ambayo hutengwa na serikali kila mkoa huzingatianpia hadhi ya eneo, kama ni jiji au manispaa, pia mikopo ya benki ya dunia au misaada mara nyingi huelekezwa kwenye majiji
 
Hongereni Moshi kwa kujiombea wenyewe kupewa jiji.Moshi serikali hii imewabeba kwa miaka mingi lakini kwa jiji wamewasahau kwakweli.
 
Kamwe hadi manispaa ya musoma kwanza iwe jiji.
 
Mkuu hapo kuna kigezo kimoja nadhani kipo nje ya uwezo wao kama binadamu wa kawaida cha kuufanya mji wa moshi uwe na idadi ya watu wanaohitajika ili uwe na sifa ya kuwa jiji
Labda wasombe watu kutoka miji mingine na 'kuwahamishia' Moshi ili kukidhi vigezo, au washawishi wanaume wote waoe wake wanne kila mmoja na ndani ya miaka mitan kila 'couple' iwe imepata watoto watatu, hapo naamini idadi itafikiwa...

Just kidding!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…