Kada wa CHADEMA
JF-Expert Member
- Feb 27, 2016
- 289
- 615
Hakika kuna mambo yanahuzunisha, yanasikitisha na yanafedhehesha.
Binafsi naamini kuwa CHADEMA ni chama makini na siku zote tumekuwa na ujasiri mkubwa wa kupambana na jambo lolote lenye manufaa kwa chama na taifa. Kabla ya mwaka 2015, CHADEMA tulikuwa chama kiongozi na tulifanya mambo mengi kwa manufaa ya taifa na tulifanikiwa. Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na suala la Richmond iliyomng'oa Edward Lowasa kwenye nafasi ya Uwaziri Mkuu. Hoja zingine ni pamoja na ESCROW, Operesheni Tokomeza nk. Haya yoye tulifanikiwa kwa vile tuliungwa mkono na wabunge wengi wa CCM na wananchi kwa ujumla.
Hata hivyo, hali imekuwa tofauti kwa sasa. Kila tunalopanga halifiki mwisho na ushirikiano kutoka kwa wananchi na washirika wetu ndani ya CCM hakika umekuwa mdogo. Siamini kwamba chama chetu kwa sasa hakina watu makini wa kushawishi mpaka tukaungwa mkono. Ila sielewi pia kwa nini tunaenda kombo.
Kwa upande wangu naamini kuwa CHADEMA tunakosea sana na hatujui nini wananchi wanahitaji na ni nani adui mkubwa ambaye kama tutamsakama lazima CCM ituunge mkono na wananchi pia. Kwa sasa tumepeleka Azimio la kutaka kumng'oa Naibu Spika, Dr Tulia Akson. Hata hivyo, tumekosea sana kwenye mashtaka yake ambapo miongoni mwa mashtaka hayo tunalalamika eti Naibu Spika anasimama sana upande wa Serikali na CCM. Haya ni mashtaka ya kijinga sana. Naita ya kijinga kwa sababu tunafahamu kuwa idadi yetu Bungeni ni ndogo na ili tufanikiwe malengo yetu, lazima tuwe na mbeleko ya wabunge wa CCM. Sasa kwa mashtaka kama haya lengo letu litafanikiwa? Mnadhani wabunge wa CCM watapiga kura ya kumuondoa Dr Tulia eti kwa vile anakipendelea chama na serikali yao?
Halikadhalika, je Dr Tulia amekuwa ni hatari sana kuliko Nyoka mwenye Makengeza, Mtemi Andrew Chenge ambaye kwa muda mrefu tulimsakama kuwa ni fisadi? Kwa nini tusianze kwanza vuguvugu la kumuondoa fisadi kuongoza Bunge badala yake tunapambana na mtu ambaye katuzidi uwezo na ana support kubwa bungeni? Are we serious?