CHADEMA tujitafakari

Tunko

Senior Member
Dec 24, 2013
181
41
Nikiwa kama Mtanzania wa kawaida kabisa nachukua fursa hii kuwapa ushauri tu mjitafakari kuna sehemu mmejikwaa na hama hama hii ya wabunge wenu ipo siku mtajikuta hamna mbunge hata mmoja na ndio itakua mwisho wa CHADEMA.CHADEMA badilikeni mambo yanayosemwa semwa ndani ya chama chenu yawezekana yana ukweli kaaeni chini mchunguze alafu mtafute suluhu,naamini mimi kuna tatizo ndani ya chama na mkibaki na akili kwamba kila anae hama kanunuliwa chama ndio kinafutika hivo mtakumbuka shuka asubuhi huku chama ndio kimeshajifia itabaki kila mtu kuchukua kilicho chake.Asanteni ulikua ni ushauli tu.
 
Ushauri huu unawapa wapenzi wa chama?, viongozi wa chama?,au wanachama?.maana chadema imegawanyika kihivyo.wanachama wapo wenye msimamo ishu ni viongozi Sasa waliobadilisha gia angani
 
Upinzani uliobaki ni wa wananchi kutaka serikali iwafanyie mambo fulani. 2020 cdm ikipata jimbo hata moja, watakua wamejitahidi zaidi ya sana.
 
Watabaki Wachaga tu ambao ndiyo wenye chama hata na hivyo baadhi wanaojua kusoma Alama za nyakati watachomoka maana hawata vumilia kukaa sehemu ambayo hakuna hela😬😬😬😬😬😬
 
Kinachoendelea ndani ya Chadema kitakoma tu pale ambapo Rais JPM atasitisha kuendelea na mpango wake wa kuuwa vyama vya upinzani kwa masirahi yake ya baadae, kwani hakuna chama kisicho na matatizo hata Ccm yako mengi yanayoweza kuwafanya wabunge, madiwani na viongozi kuondoka ndani ya chama hicho ila wanamwogopa Magufuri.
 
Nataka nikuhakikishie kuwa CDM hakuna shida unayodhani. Shida tu ni kuwa mkakati ambao mkuu wa nchi anao ni kuua kabisa upinzani. Na kila njia inatumika kufikia adhma hiyo. Lakini dhuluma yoyote ina malipo yake hapahapa duniani. Na hakuna popote duniani tawala yenye dhuluma ikawa na mwisho mzuri. CCM jiangalieni sana kama kweli mnatenda haki kuvikandamiza vyama vya upinzani. Mwisho unakuja soon or later na muda unakuja wa kuijenga Tanzania bora kwa ajili ya watoto wetu na watoto wa watoto wetu.
 
Hii tabia ya wanaccm kujifanya wanaihurumia chadema ni ya kulaaniwa na kupuuzwa kwa nguvu zote. Tuachieni chadema yetu ikikosa mbunge hata mmoja inawauma nini?
 
Nikiwa kama Mtanzania wa kawaida kabisa nachukua fursa hii kuwapa ushauri tu mjitafakari kuna sehemu mmejikwaa na hama hama hii ya wabunge wenu ipo siku mtajikuta hamna mbunge hata mmoja na ndio itakua mwisho wa CHADEMA.CHADEMA badilikeni mambo yanayosemwa semwa ndani ya chama chenu yawezekana yana ukweli kaaeni chini mchunguze alafu mtafute suluhu,naamini mimi kuna tatizo ndani ya chama na mkibaki na akili kwamba kila anae hama kanunuliwa chama ndio kinafutika hivo mtakumbuka shuka asubuhi huku chama ndio kimeshajifia itabaki kila mtu kuchukua kilicho chake.Asanteni ulikua ni ushauli tu.
Mkuu usijidanganye. Kwa upande wangu mimi naamini hawa watu wananunuliwa na wanaahidiwa kabisa kurudishwa bungeni. Maana yake ni kuwa panakua na makubaliano baina ya muhamaji na huko anakohamia ndio maana unaona kila anayehama, anapewa nafasi ya kugombea tena. Kwa akili ndogo tu, utajua nini kinaendelea
 
Nikiwa kama Mtanzania wa kawaida kabisa nachukua fursa hii kuwapa ushauri tu mjitafakari kuna sehemu mmejikwaa na hama hama hii ya wabunge wenu ipo siku mtajikuta hamna mbunge hata mmoja na ndio itakua mwisho wa CHADEMA.CHADEMA badilikeni mambo yanayosemwa semwa ndani ya chama chenu yawezekana yana ukweli kaaeni chini mchunguze alafu mtafute suluhu,naamini mimi kuna tatizo ndani ya chama na mkibaki na akili kwamba kila anae hama kanunuliwa chama ndio kinafutika hivo mtakumbuka shuka asubuhi huku chama ndio kimeshajifia itabaki kila mtu kuchukua kilicho chake.Asanteni ulikua ni ushauli tu.
Utatukanwa tuu
 
Back
Top Bottom