CHADEMA tujirekekebishe kwa haya...

CHADEMA tujirekekebishe kwa haya...

G4N

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2014
Posts
4,449
Reaction score
10,300
Uchaguzi umekwisha yaliyotokea tumeyaona. Rais wa mioyo ya watanzania tunamjua na rais wa Tanzania tunamjua. Kwa kuwa siasa ni maisha hatuna budi kujipanga upya kwa uchaguzi ujao. Ili kujipanga vema tuangalie mapungufu ndani ya chama chetu na tuyafanyie kazi ili kuongeza nguvu ya ushindi ktk chaguzi zijazo.
Sina nia ya kukidhalilisha chama, hapana. Chadema kama chama cha upinzani lazima kijipambanue kwa ubora na uwazi zaidi tofauti kabisa na ilivyo kwa ccm. Sitegemei kupewa majibu ama hoja kuwa "hata ccm hayo yapo". Chadema haikuanzishwa ili kuiga toka ccm bali kuwa chama mfano na tumaini la watanzania.
Mapungufu niliyo yaona ni:-
1. Hakuna uwezeshaji wa aina yoyote kwenye ngazi za chini (wilaya kushuka hadi ngazi ya msingi). Viongozi ktk ngazi hizi wana njaa ya kufa mtu kiasi kwamba mtia nia anapojitokeza atakamuliwa michango ya kila namna. Lakini pia inasababisha viongozi wa wilaya kugawanyika kwa kila mmoja kumpigania mtia nia mwenye fedha ili mradi kila mmoja apate chochote kitu.
Hii imeharibu nguvu ya umoja sehemu nyingi sana. Kwani kuna baadhi ya maeneo ilifikia hatua ya sehemu moja ya uongozi wa wilaya ambayo mtia nia wake hajapitishwa kuwa mgombea ilisusia kampeni na kuanza kumharibia mgombea wao. Njaa ni Kali saana kwa viongozi wa chini hawa. Hili liangaliwe kwa kuanza kupeleka mafungu ya fedha ktk ngazi hizi.

2. Rushwa: Chadema kuna rushwa sana ktk hatua ya kuwania uteuzi ndani ya chama. Chadema haina tofauti na ccm kabisa. Ndani ya chadema kama huna fedha ya kuwahonga viongozi wa kata na wale wa wilaya hupitishwi hata ufanye vipi.
Hili utatuzi wake ni kuongeza wigo wa wajumbe wa kupiga kura za maoni. Ikibidi tufanye kama ccm ambapo kila mwanachama hai ktk jimbo/kata husika anapiga kura. Tuige hili toka ccm.

3. Kuna upendeleo wa wazi. Kuna mahali tumekosa ushindi kwasabb tu aliyepitishwa anajulikana na ngazi za juu..namaanisha taifa. Lkn hakubaliki kwa wananchi. Utatuzi mnao wenyewe viongozi wa juu kwa kuacha matakwa ya watu yaheshimiwe.

4. Hakuna msaada wowote kwa watia nia na wagombea....hata wa mawazo tu. Kila MTU anahaingaika kivyake halafu mwisho wa siku katiba ya chadema inamtaka mbunge/diwani kuchangia chama toka sehemu ya masurufu yake. Kuchangia sawa lkn vipi wakati wa kampeni mbona hakuna msaada wowote?
Sana sana kuna aina Fulani ya utapeli unafanywa huko ngazi za chini. Mtia nia anatumiwa ujumbe na viongozi wa kanda, mkoa ama wilaya na kuombwa achangie laki moja kwa ajili ya semina itafanyika tarehe fulani, itaendeshwa na kiongozi wa ngazi ya kitaifa. Tarehe ikifika utaambiwa kiongozi huyo anaomba radhi hatofika kwasabb fulani fulani. Fedha hairudishwi, utaambiwa ni mchango wa kuendesha chama.
Kuna watu ni Mara yao ya kwanza hawajui wafanye nn. Wanakata tamaa.
Tuyaangalie haya kwa mapana take yatasaidia kuongeza ushindi wa chadema ktk chaguzi zijazo.
 
hongera kwa mawazo na ushauri ulio tukuka sana naamini niwasikivu watachua yote na kuyafanyia kazi.
 
Hata madiwani wao wa awamu iliyopita esp. Mby mjini ni warushwa hatari. Sasa hivi nadhani itakuwa balaa zaidi.
 
Hata madiwani wao wa awamu iliyopita esp. Mby mjini ni warushwa hatari. Sasa hivi nadhani itakuwa balaa zaidi.

Sasa hivi tunahitaji mabadiliko ya kimifumo ndani ya chama. Hali ni mbaya kwa watia-nia na wagombea. Huna hela hufurukuti. Na haya unaambiwa ama unapewa ishara/picha live
 
Haya yote tuliyashauri sana baada ya uchaguzi wa 2010.
Mwaka 2011 mwenyekiti alisema tutaanzisha mfuko maalum wa kuwasaidia wagombea watakaokuwa na changamoto ya kifedha.Kilichotokea mwaka huu ni Mungu anajua.
Kuhusu rushwa kuanzia kuwapata wagombea na viti maalum hata CCM hawatukuti tena.
 
hivi kuna mtu ana akili timamu kabisa na yale yaliyotokea akaringa mahali kuwa ni mwanachama wa chadema?

labda awe anaringa akiwa under influence ya bangi, njaa ya hela, madawa ya kulevya au alcohol

wengi wapo sababu ya pili
 
hongera kwa mawazo na ushauri ulio tukuka sana naamini niwasikivu watachua yote na kuyafanyia kazi.
Nakumbuka kamanda Chacha Wangwe aliwahi kusema maneno kama hayo lakini kwa bahati mbaya ushauri huo ukamletea matata makubwa sana ikiwa ni pamoja na kuporwa Umakamu na mwishowe akafariki bila kuona matokea ya message sent.
 
hivi kuna mtu ana akili timamu kabisa na yale yaliyotokea akaringa mahali kuwa ni mwanachama wa chadema?

labda awe anaringa akiwa under influence ya bangi, njaa ya hela, madawa ya kulevya au alcohol

wengi wapo sababu ya pili
Waberoya, ulishaahamia ACT wazalendo?
 
hivi kuna mtu ana akili timamu kabisa na yale yaliyotokea akaringa mahali kuwa ni mwanachama wa chadema?

labda awe anaringa akiwa under influence ya bangi, njaa ya hela, madawa ya kulevya au alcohol

wengi wapo sababu ya pili
Mzee upo kumbe.
 
Sasa hivi tunahitaji mabadiliko ya kimifumo ndani ya chama. Hali ni mbaya kwa watia-nia na wagombea. Huna hela hufurukuti. Na haya unaambiwa ama unapewa ishara/picha live

Natamani kuona viongozi wa chama wakija hapa kutoa maelezo ya kukubaliana na ushauri wako. Lkn pia maelezo ya nn kinafanyika kuondoa kasoro hizi.
cc: Tumaini Makene
cc: John Mnyika
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom