Mzyondi
Member
- Nov 24, 2016
- 40
- 64
Ni zaidi ya mwaka sasa tangu kufanyika uchaguzi mkuu uliokuwa na ushindani mkubwa baina ya ccm na cdm(UKAWA)na hatimaye mgombea wa ccm kutangazwa mshindi kwa kura chache, kabla ya uchaguzi mchakato wa kuwapata wagombea uligubikwa na utata, baadhi ya washindi wa kura za maoni kwenye majimbo walienguliwa na nafasi zao walipewa wanachama wapya waliojiunga na chama kutoka ccm, kwa waliotoka ccm na kufanikiwa kupata ushindi ni wawili tu Esta Bulaya na Onesmo Ole Nangole, waliosalia wote majanga na walisababisha migogoro ndani ya chama kwa kuwa walioenguliwa ndio waliokuwa wamepanda mbegu ya mabadiliko na kustawi vyema halafu anakuja kuvuna mtu mwingine?
Gia ya angani iliyowezesha ujio wa Lowassa na kisha kuwa mgombea wa CDM(UKAWA) bila kupitia kwenye mchujo wa kushindania nafasi ya kugombea urais ilitushitua wengi ingawa tulimuunga mkono kwa kumpigia kura nyingi lakini aina hiyo ya uteuzi si afya kwa chama kinachoamini katika demokrasia.Yaliyopita si ndwele tugange yajayo ,kujikwaa si kuanguka ni wakati mwafaka sasa CHADEMA TUJISAHIHISHE KWA MASLAHI YA TAIFA tusirudie makosa tuliyofanya awal kwa kuanza na uchaguzi wa ndani ulio huru na haki na kisha tujenge chama taasisi ambacho msingi wake ni wanachama tusijenge chama juu ya migongo ya watu,Watanznia wengi wameshakichoka chama cha cha mapinduzi ila hawako tayari kupigia kura upinzani ambao haujimbambanui na kuonyesha utofauti wake na ccm ndio maana wengi hupigia kura ccm kwa mazoea tu,
Endapo Lowassa angeshinda uchaguzi Mh Mbowe angeingia kwenye kitabu cha guiness kwa gia yake ya angani kufanikisha kushika dola, kwa kuwa gia hiyo haikuzaa matunda tuliyoyataka sasa ni wakati mwafaka wa kutumia gia ya ardhini itakayowezesha kuwa na mchakato huru kwa mwanachama yeyote kuomba kuteuliwa kugombea urais, huyo mh Lowasa kama anatakak kugombea tena basi apambane na watu wengine atakayepita apeperushe bendera ya chama,
Magufuli anajua kabisa chama chake kimechoka na kimechokwa ndio maana amezuia shughuli za kisiasa kwa malengo ya kukijenga chama chake ambacho kimezeeka na hata afanye nini hawezi kuiokoa tena ccm mbele CHADEM na washirika wake wa UKAWA.