chadema SIKIO LA KUFA?

A

assadsyria3

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2013
Messages
6,733
Likes
2,303
Points
280
Age
38
A

assadsyria3

JF-Expert Member
Joined Apr 9, 2013
6,733 2,303 280
WAKATI mazingira ya mgogoro uliopo ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya kusimamishwa uongozi kwa Naibu Katibu Mkuu wake, Kabwe Zitto na mjumbe wa Kamati Kuu, Dk. Kitila Mkumbo yakielekeza umma kujiuliza kama chama hicho ni sikio la kufa kwa sasa, vyama vitatu vya siasa hapa nchini vimemkaribisha mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto (pichani kushoto), kujiunga navyo endapo atafukuzwa katika chama chake cha sasa, Raia Mwema linafahamu.
Taarifa hii mpya inakuja katika kipindi ambacho chama hicho kikuu cha upinzani nchini kikiwa, labda, katika mgogoro mkubwa zaidi kuwahi kukikuta tangu kilipoanzishwa miaka 20 iliyopita.
Gazeti hili limezungumza na baadhi ya viongozi wa vyama hivyo na wamethibitisha kwamba wako tayari kumpokea mwanasiasa huyo, endapo chama chake kitamfukuza kama dalili zinavyoonyesha kwa sasa.
Kamati Kuu ya CHADEMA imempa Zitto na mjumbe wa kamati hiyo, Dk. Kitila Mkumbo, muda wa siku 14 kuanzia Ijumaa iliyopita wajieleze kwa nini wasifukuzwe kutoka kwenye chama hicho kutokana na kutuhumiwa kufanya uhaini.
Vyama ambavyo gazeti hili linafahamu kuwa viko tayari kumpokea Zitto ni Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama Cha Wananchi (CUF) na chama cha NCCR-Mageuzi; ambavyo pia ndiyo vyama vinara kwa siasa za hapa nchini, kama ilivyo kwa CHADEMA.
Ingawa jitihada hizo hazijawa rasmi, haswa kwa upande wa upinzani kwa sababu ya heshima baina ya vyama husika, angalau baadhi ya viongozi wamekuwa wazi na kueleza kwamba suala hilo lipo hata kama halijatangazwa.
Kiongozi wa kwanza wa kisiasa kutoa kauli baada ya hatua ya CHADEMA kumvua Zitto na Kitila vyeo vyao vyote vya kisiasa walivyokuwa navyo ndani ya chama chao alikuwa ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba.
Akiandika katika mitandao mbalimbali ya kijamii, Mwigulu alieleza kwamba kilichomkuta Zitto na Kitila ni matunda ya kuwemo katika chama ambacho hakiendani na kaliba yao kwa sasa.
“Kwenye CHADEMA, wale wote wenye akili wako nje ya uzio wa chemichemi ya mawazo. Mfano ni bungeni, wana CHADEMA waliowahi kufundisha vyuoni hawapewi hata unaibu waziri kivuli kwa kuwa wanatumia zaidi akili badala ya nguvu.
“Lakini, walioishia kidato cha kwanza, pili, tatu na sifuri ndiyo majembe ya chama wanaopewa fursa zote kwa kuwa wao badala ya kutumia akili wanatumia nguvu na mabavu.
“Nawafahamu Zitto na Kitila tangu nikiwa Chuo Kikuu na nawajua kama watu mahiri wanaoweza kutoa mchango popote,” aliandika Mwigulu.
Hata hivyo, kauli hiyo ya Mwigulu ni tofauti kwa kiasi kikubwa na michango yake bungeni kila anapokosoa hotuba ya bajeti kutoka kwa Wizara (kivuli) ya Fedha inayoongozwa na Zitto, akiamini imekuwa ikifanywa bila umahiri wa kutosha.
Katika mazungumzo na gazeti hili wiki hii, Mwigulu alisema “Sisi hatuna tatizo na Zitto. CCM ni chama cha Watanzania wote kisichobagua watu kwa kutumia dhana za ukanda, udini wala ukabila.
Akitaka kuja, anakaribishwa kwa mikono miwili,” alisema Mwigulu.
Kwa upande wa CUF, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Julius Mtatiro, alisema wanafuatilia kwa karibu kila kinachoendelea ndani ya CHADEMA kwa vile ni chama mwenza katika upinzani na lolote linalotokea litakuwa na athari katika ulingo wa kisiasa hapa nchini.
“Sitakuwa nasema ukweli kama nikisema CUF haimuhitaji Zitto, Kitila au mwanasiasa yeyote mahiri kutoka chama chochote cha siasa hapa nchini.
Hata hivyo, si vizuri pia kwangu kusema tunamtaka mwanachama wa chama kingine maana hilo linaweza kumaanisha tunachochea machafuko,” alisema Mtatiro.
Hata hivyo, Raia Mwema linafahamu kwamba baadhi ya viongozi wa juu wa CUF walikuwa miongoni mwa watu wa mwanzo kutafuta mawasiliano na Zitto mara baada ya kuvuja kwa taarifa za mwanasiasa huyo kuvuliwa madaraka.
Mmoja wa viongozi wa juu wa CUF aliyezungumza na gazeti hili kwa masharti ya kutotajwa jina, alisema kama Zitto atahamia katika chama chao, watakuwa wamepata kitu kimoja tu ambacho walikuwa wakikikosa kwa muda mwingi.
“Unajua CUF Zanzibar wana Maalim Seif. Watu wanapenda sana chama chao lakini pia wana mtu ambaye wanampenda na anakiwakilisha vizuri. Mwenyekiti (Profesa Ibrahim Lipumba), amefanya kazi nzuri lakini haonekani kama anaweza kuongeza idadi ya wanachama na wapenzi wa CUF. Hana ule mvuto kama wa Maalim au alionao Zitto.
“Tunachohitaji ni mtu mmoja ambaye anaweza kuleta wanachama wapya na msukumo mpya kwenye chama.
“Bila shaka, Zitto anaweza kuleta hilo na ndiyo maana atakaribishwa kwa mikono miwili. Hata kama atatoa masharti ya kupewa cheo fulani, hilo litawezekana pia,” alisema kiongozi huyo.
Akizungumzia suala la Zitto, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, alisema binafsi hawezi kuwa na tatizo iwapo mwanasiasa huyo ataamua kuhamia kwenye chama chake ingawa alisema hajafanya mazungumzo na mbunge mwenzake huyo kuhusu kuhamia chama chake.
Mimi kama James, sijazungumza na Zitto kumshawishi ahamie NCCR. Hata hivyo, NCCR si James Mbatia, ni taasisi ambayo ina watu wengi. Kama umesikia kuwa chama changu kinamtaka basi inawezekana juhudi hizo akawa amefanya mtu mwingine lakini si mimi,” alisema.
Kama ilivyo CHADEMA kwa sasa, NCCR kiliwahi kuwa chama kikuu cha upinzani hapa nchini lakini kikakumbwa na migogoro iliyosababisha kushuka umaarufu wake ingawa sasa Mbatia anakijenga upya.
Mbatia alizungumzia pia mgogoro wa CHADEMA na kusema kutokana na uzoefu wa NCCR, anaamini kwamba namna pekee ya kushughulika na migogoro ni kuzungumzia kuhusu hoja na si watu binafsi na badala ya kutumia sana Katiba na sheria, viongozi watumie zaidi hekima na busara.
“Migogoro inaweza ikakijenga chama kama watu wataichukulia kwa njia chanya. Kama unapokea vibaya kutofautiana, lazima kutakuwa na matatizo. Jambo la msingi kwa CHADEMA kwa sasa ni kujibu hoja zilizotolewa na Zitto na si kumshughulikia yeye na mwenzake,” alisema Mbatia.
Hoja ya Zitto kuhamia NCCR inachochewa pia na ukweli kwamba ndiyo chama chenye nguvu zaidi mkoani Kigoma anakotoka kwa sasa na tayari baadhi ya maswahiba wake wa kisiasa kama Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, wamehamia huko wakitokea CHADEMA.
Kamati Kuu CHADEMA
Taarifa za ndani ya kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA zimedai kwamba kambi ya Zitto na Kitila ilimtuhumu mke wa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbrod Slaa, Josephine, kuwa ndiye aliyesambaza ulioitwa Waraka wa Siri –ambao pamoja na mambo mengine ulidai kuwa mbunge huyo anapokea fedha kutoka Idara ya Usalama wa Taifa na kuzihifadhi katika akaunti zake za nje ya nchi.
Raia Mwema limeelezwa kwamba Zitto ndiye aliyetoa madai hayo kuhusu Josephine ambaye katika siku za karibuni amekuwa miongoni mwa wachangiaji maarufu wa masuala ya CHADEMA katika mitandao ya kijamii.
Mpaka sasa haijulikani ni nani haswa aliyeusambaza waraka huo uliosababisha Zitto aende kushitaki polisi, lakini inajulikana kuwa Slaa ni miongoni mwa waliovutiwa na maudhui yake kiasi cha ku-like waraka huo mtandaoni.
CHADEMA kimekana kuhusika na waraka huo lakini malalamiko ya Zitto yalikuwa kuhusu hatua ya bosi wake (Slaa) ‘kuupenda’ waraka huo wakati ulikuwa ukimkashifu na kumvunjia heshima mmoja wa viongozi wa juu kabisa wa chama chao.
Gazeti hili linaarifiwa katika kikao hicho, Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu pamoja Mwenyekiti wa chama hicho katika mikoa ya Kanda ya Kusini, Matare Matiko, ndiyo walioongoza mashambulizi dhidi ya Zitto kwenye kikao hicho huku Msafiri Mtemelwa, akiongoza katika watetezi wa Zitto.
Ni Lissu ambaye baada ya Zitto na Kitila kutoa hoja ya kujiuzulu nyadhifa zao ndani ya chama – aliibua hoja ya kutaka wasikubaliwe kujivua wenyewe bali wavuliwe na chama na watakiwe kujieleza kwa nini wasifukuzwe chamani.
Hoja hii ya Lissu ndiyo iliyopitishwa na kamati kuu ya chama hicho.
- See more at: Raia Mwema - CHADEMA sikio la kufa?
 
Zuberi Magoha

Zuberi Magoha

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Messages
208
Likes
0
Points
0
Zuberi Magoha

Zuberi Magoha

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2013
208 0 0
WAKATI mazingira ya mgogoro uliopo ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya kusimamishwa uongozi kwa Naibu Katibu Mkuu wake, Kabwe Zitto na mjumbe wa Kamati Kuu, Dk. Kitila Mkumbo yakielekeza umma kujiuliza kama chama hicho ni sikio la kufa kwa sasa, vyama vitatu vya siasa hapa nchini vimemkaribisha mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto (pichani kushoto), kujiunga navyo endapo atafukuzwa katika chama chake cha sasa, Raia Mwema linafahamu.
Taarifa hii mpya inakuja katika kipindi ambacho chama hicho kikuu cha upinzani nchini kikiwa, labda, katika mgogoro mkubwa zaidi kuwahi kukikuta tangu kilipoanzishwa miaka 20 iliyopita.
Gazeti hili limezungumza na baadhi ya viongozi wa vyama hivyo na wamethibitisha kwamba wako tayari kumpokea mwanasiasa huyo, endapo chama chake kitamfukuza kama dalili zinavyoonyesha kwa sasa.
Kamati Kuu ya CHADEMA imempa Zitto na mjumbe wa kamati hiyo, Dk. Kitila Mkumbo, muda wa siku 14 kuanzia Ijumaa iliyopita wajieleze kwa nini wasifukuzwe kutoka kwenye chama hicho kutokana na kutuhumiwa kufanya uhaini.
Vyama ambavyo gazeti hili linafahamu kuwa viko tayari kumpokea Zitto ni Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama Cha Wananchi (CUF) na chama cha NCCR-Mageuzi; ambavyo pia ndiyo vyama vinara kwa siasa za hapa nchini, kama ilivyo kwa CHADEMA.
Ingawa jitihada hizo hazijawa rasmi, haswa kwa upande wa upinzani kwa sababu ya heshima baina ya vyama husika, angalau baadhi ya viongozi wamekuwa wazi na kueleza kwamba suala hilo lipo hata kama halijatangazwa.
Kiongozi wa kwanza wa kisiasa kutoa kauli baada ya hatua ya CHADEMA kumvua Zitto na Kitila vyeo vyao vyote vya kisiasa walivyokuwa navyo ndani ya chama chao alikuwa ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba.
Akiandika katika mitandao mbalimbali ya kijamii, Mwigulu alieleza kwamba kilichomkuta Zitto na Kitila ni matunda ya kuwemo katika chama ambacho hakiendani na kaliba yao kwa sasa.
"Kwenye CHADEMA, wale wote wenye akili wako nje ya uzio wa chemichemi ya mawazo. Mfano ni bungeni, wana CHADEMA waliowahi kufundisha vyuoni hawapewi hata unaibu waziri kivuli kwa kuwa wanatumia zaidi akili badala ya nguvu.
"Lakini, walioishia kidato cha kwanza, pili, tatu na sifuri ndiyo majembe ya chama wanaopewa fursa zote kwa kuwa wao badala ya kutumia akili wanatumia nguvu na mabavu.
"Nawafahamu Zitto na Kitila tangu nikiwa Chuo Kikuu na nawajua kama watu mahiri wanaoweza kutoa mchango popote," aliandika Mwigulu.
Hata hivyo, kauli hiyo ya Mwigulu ni tofauti kwa kiasi kikubwa na michango yake bungeni kila anapokosoa hotuba ya bajeti kutoka kwa Wizara (kivuli) ya Fedha inayoongozwa na Zitto, akiamini imekuwa ikifanywa bila umahiri wa kutosha.
Katika mazungumzo na gazeti hili wiki hii, Mwigulu alisema "Sisi hatuna tatizo na Zitto. CCM ni chama cha Watanzania wote kisichobagua watu kwa kutumia dhana za ukanda, udini wala ukabila.
Akitaka kuja, anakaribishwa kwa mikono miwili," alisema Mwigulu.
Kwa upande wa CUF, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Julius Mtatiro, alisema wanafuatilia kwa karibu kila kinachoendelea ndani ya CHADEMA kwa vile ni chama mwenza katika upinzani na lolote linalotokea litakuwa na athari katika ulingo wa kisiasa hapa nchini.
"Sitakuwa nasema ukweli kama nikisema CUF haimuhitaji Zitto, Kitila au mwanasiasa yeyote mahiri kutoka chama chochote cha siasa hapa nchini.
Hata hivyo, si vizuri pia kwangu kusema tunamtaka mwanachama wa chama kingine maana hilo linaweza kumaanisha tunachochea machafuko," alisema Mtatiro.
Hata hivyo, Raia Mwema linafahamu kwamba baadhi ya viongozi wa juu wa CUF walikuwa miongoni mwa watu wa mwanzo kutafuta mawasiliano na Zitto mara baada ya kuvuja kwa taarifa za mwanasiasa huyo kuvuliwa madaraka.
Mmoja wa viongozi wa juu wa CUF aliyezungumza na gazeti hili kwa masharti ya kutotajwa jina, alisema kama Zitto atahamia katika chama chao, watakuwa wamepata kitu kimoja tu ambacho walikuwa wakikikosa kwa muda mwingi.
"Unajua CUF Zanzibar wana Maalim Seif. Watu wanapenda sana chama chao lakini pia wana mtu ambaye wanampenda na anakiwakilisha vizuri. Mwenyekiti (Profesa Ibrahim Lipumba), amefanya kazi nzuri lakini haonekani kama anaweza kuongeza idadi ya wanachama na wapenzi wa CUF. Hana ule mvuto kama wa Maalim au alionao Zitto.
"Tunachohitaji ni mtu mmoja ambaye anaweza kuleta wanachama wapya na msukumo mpya kwenye chama.
"Bila shaka, Zitto anaweza kuleta hilo na ndiyo maana atakaribishwa kwa mikono miwili. Hata kama atatoa masharti ya kupewa cheo fulani, hilo litawezekana pia," alisema kiongozi huyo.
Akizungumzia suala la Zitto, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, alisema binafsi hawezi kuwa na tatizo iwapo mwanasiasa huyo ataamua kuhamia kwenye chama chake ingawa alisema hajafanya mazungumzo na mbunge mwenzake huyo kuhusu kuhamia chama chake.
Mimi kama James, sijazungumza na Zitto kumshawishi ahamie NCCR. Hata hivyo, NCCR si James Mbatia, ni taasisi ambayo ina watu wengi. Kama umesikia kuwa chama changu kinamtaka basi inawezekana juhudi hizo akawa amefanya mtu mwingine lakini si mimi," alisema.
Kama ilivyo CHADEMA kwa sasa, NCCR kiliwahi kuwa chama kikuu cha upinzani hapa nchini lakini kikakumbwa na migogoro iliyosababisha kushuka umaarufu wake ingawa sasa Mbatia anakijenga upya.
Mbatia alizungumzia pia mgogoro wa CHADEMA na kusema kutokana na uzoefu wa NCCR, anaamini kwamba namna pekee ya kushughulika na migogoro ni kuzungumzia kuhusu hoja na si watu binafsi na badala ya kutumia sana Katiba na sheria, viongozi watumie zaidi hekima na busara.
"Migogoro inaweza ikakijenga chama kama watu wataichukulia kwa njia chanya. Kama unapokea vibaya kutofautiana, lazima kutakuwa na matatizo. Jambo la msingi kwa CHADEMA kwa sasa ni kujibu hoja zilizotolewa na Zitto na si kumshughulikia yeye na mwenzake," alisema Mbatia.
Hoja ya Zitto kuhamia NCCR inachochewa pia na ukweli kwamba ndiyo chama chenye nguvu zaidi mkoani Kigoma anakotoka kwa sasa na tayari baadhi ya maswahiba wake wa kisiasa kama Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, wamehamia huko wakitokea CHADEMA.
Kamati Kuu CHADEMA
Taarifa za ndani ya kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA zimedai kwamba kambi ya Zitto na Kitila ilimtuhumu mke wa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbrod Slaa, Josephine, kuwa ndiye aliyesambaza ulioitwa Waraka wa Siri –ambao pamoja na mambo mengine ulidai kuwa mbunge huyo anapokea fedha kutoka Idara ya Usalama wa Taifa na kuzihifadhi katika akaunti zake za nje ya nchi.
Raia Mwema limeelezwa kwamba Zitto ndiye aliyetoa madai hayo kuhusu Josephine ambaye katika siku za karibuni amekuwa miongoni mwa wachangiaji maarufu wa masuala ya CHADEMA katika mitandao ya kijamii.
Mpaka sasa haijulikani ni nani haswa aliyeusambaza waraka huo uliosababisha Zitto aende kushitaki polisi, lakini inajulikana kuwa Slaa ni miongoni mwa waliovutiwa na maudhui yake kiasi cha ku-like waraka huo mtandaoni.
CHADEMA kimekana kuhusika na waraka huo lakini malalamiko ya Zitto yalikuwa kuhusu hatua ya bosi wake (Slaa) ‘kuupenda' waraka huo wakati ulikuwa ukimkashifu na kumvunjia heshima mmoja wa viongozi wa juu kabisa wa chama chao.
Gazeti hili linaarifiwa katika kikao hicho, Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu pamoja Mwenyekiti wa chama hicho katika mikoa ya Kanda ya Kusini, Matare Matiko, ndiyo walioongoza mashambulizi dhidi ya Zitto kwenye kikao hicho huku Msafiri Mtemelwa, akiongoza katika watetezi wa Zitto.
Ni Lissu ambaye baada ya Zitto na Kitila kutoa hoja ya kujiuzulu nyadhifa zao ndani ya chama – aliibua hoja ya kutaka wasikubaliwe kujivua wenyewe bali wavuliwe na chama na watakiwe kujieleza kwa nini wasifukuzwe chamani.
Hoja hii ya Lissu ndiyo iliyopitishwa na kamati kuu ya chama hicho.
- See more at: Raia Mwema - CHADEMA sikio la kufa?
You are just a pig unahangaika mno na issue ya Zitto ,Tafuta pesa ya familia yako ule .
 
Mingoi

Mingoi

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2012
Messages
10,984
Likes
2,832
Points
280
Mingoi

Mingoi

JF-Expert Member
Joined Jul 21, 2012
10,984 2,832 280
Sitoshangaa kuwa Josephine kuwa sehemu ya wasambazaji wa waraka
 
A

assadsyria3

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2013
Messages
6,733
Likes
2,303
Points
280
Age
38
A

assadsyria3

JF-Expert Member
Joined Apr 9, 2013
6,733 2,303 280
dk kweli anachuki na zito kapiga like :smile-big:
 
T2015CCM

T2015CCM

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2012
Messages
7,936
Likes
382
Points
180
Age
86
T2015CCM

T2015CCM

JF-Expert Member
Joined Sep 13, 2012
7,936 382 180
Chadema arusha vipande vipande...

Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Monduli asimamishwa uongozi mara moja
TAARIFA KWA UMMA

Kwa niaba ya baraza la uongozi la mkoa wa Arusha, napenda kuujulisha umma wote kwa ujumla kuwa mwenyekiti wa wilaya ya monduli Mchungaji Amani Silanga Mollel amekoma/amesimamishwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya monduli kuanzia tarehe 29 Novemba 2013 kufuatia tuhuma nzito za uvunjifu wa kanuni za maadili ya chama.
Hatua hii imefikiwa baada ya kuthibitika na yeyé mwenyewe kukiri mbele ya kikao cha kamati tendaji ya wilaya ya monduli kilichoketi tarehe 29 Novemba 2913 saa NNE asubuhi kuwa alitoa tamko batili akitumia wadhifa wa mwenyekiti wa wilaya bila ridhaa ya kamati tendaji na huku akidanganya kuwa ni tamko kwa niaba ya wilaya ya monduli.
Katika tamko lake ametoa tuhuma dhidi ya wajumbe wa kamati kuu na viongozi wakuu wa kitaifa kwa maamuzi halali ya kikao cha kamati kuu huku akijua kuwa anavunja kanuni za chama kwa mujibu wa katiba ya chama toleo la mwaka 2006 ya Kanuni za uendeshaji kazi za chama, sura ya KUMI, ibara ya 10 (X) "Kiongozi asitoe tuhuma zozote juu ya viongozi wenzake pasipo kupitia vikao halali na kuzingatia taratibu na ngazi zilizoelezwa kwenye kanuni za chama".
Sambamba na hilo, Mchungaji Amani Silanga ametoa tuhuma za uzushi, uongo na upotoshaji na kutaka kuaminisha jamii kuwa chadema ina makundi ya CHADEMA Asili na CHADEMA Family kitu ambacho ni upotoshaji mkubwa na wa hatari kwa ustawi na umoja wa chama na kinyume na kanuni za uendeshaji kazi za chama, sura ya KUMI, ibara ya 10 (VII), "Kiongozi anatakiwa kuwa mkweli na muwazi wakati wote hususani katika vikao halali na aachane na vikundi vya majungu, wadanganyifu (Rumour Mongers). Ni mwiko kwa kiongozi kujihusisha na upotoshaji wa maamuzi wa vikao halali". Kamati tendaji ya wilaya ilipomtaka aonyeshe CHADEMA asili ni kina nani na CHADEMA family ni kina nani alishindwa kutoa maelezo yoyote ya maana na kufikia hatua ya kutaka kuvuruga kikao kwa kuleta vijana wahuni wapatao 17 ndani ya kikao ambao wengi walijulikana kuwa sio WANACHADEMA. Katika utambulisho wake wa majigambo Mchungaji Amani SIlanga kwa kiburi na kejeli amejitambulisha na kukiri kuwa yeye yupo kambi ya Zito Kabwe na hakuna wa kumfanya kitu maana ni mjumbe wa baraza kuu la chama. Maneno yake yalidhihirisha kuwa Mchungaji Amani Silanga anashiriki mpango wa kuunda makundi yasiyo na tija ndani ya chama na hivyo kuwa kinyume na sura hiyo hiyo ya kumi ya kanuni za uendeshaji kazi za chama ibara ya 10 (IX), "Kiongozi asijihusishe au kushiriki na vikundi au vitendo vya kuchonganisha au kuzua migogoro ndani ya uongozi wa chama au wanachama wake".

AZIMIO LA BARAZA LA UONGOZI LA MKOA WA ARUSHA:
Baraza la uongozi la mkoa lililoketi tarehe 29 Novemba 2013, limepokea mapendekezo ya kamati tendaji ya wilaya na kuzingatia hofu kubwa iliyoainishwa na kamati tendaji kufuatia matendo mengi yanayotia shaka ya uadilifu na uwezo wa kiuongozi wa Mchungaji Amani Silanga na hivyo baraza la uongozi la mkoa limeridhia kuwa amevunja kanuni za maadili ya chama sura ya KUMI ibara ya (VII) hadi (XII) na hivyo kupelekea ukomo wa yeye kuwa Mwenyekiti wa wilaya kuanzia tarehe 29 Novemba 2013. Baraza la mkoa likiwa mamlaka ya nidhamu kwa mujibu wa katiba ibara ya 6.3.6 (a) (iv) limemjulisha tuhuma zake na hatua hii stahiki iliyochukuliwa. Kwa vile Mchungaji Amani Silanga alikiri kosa hili mbele ya kamati tendaji ya wilaya bila kulijutia au kuomba msamaha, baraza la mkoa limechukua hatua hii stahiki kwa maslahi ya chama na kuwa uchunguzi zaidi utafanyika ili kufikia maamuzi makubwa zaidi ya tuhuma nyingi kwa mujibu wa kanuni za hatua za kinidhamu.
Baraza la uongozi la mkoa wa Arusha, linatoa onyo kwa wote ambao wapo katika mtandao huu mchafu, ama watoke wenyewe mapema maana hawatavumiliwa kamwe. Baraza la uongozi wa mkoa liliona kuwa Mchungaji Silanga amepotoka na hivyo yeyé kuendelea kuwepo ndani ya chama wakati wa uchunguzi wa tuhuma hizi nzito dhidi yake ni hatari zaidi kwa ustawi wa chama na hivyo baraza likaridhia kwa kuzingatia tafsiri ya katiba ya chama ibara ya 6.3.4 (c) wa yeyé kukoma uongozi na hivyo akae nje kwa muda na waliopotoka wenzake.

Amani Golugwa
Katibu wa CHADEMA – Mkoa wa Arusha.
(Kwa niaba ya Baraza la Uongozi la Mkoa wa Arusha)
Tarehe 30 Novemba 2013

============================== ====================
Omba kazi usiombe pesa
chezea pesa usichee Kazi
 
T2015CCM

T2015CCM

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2012
Messages
7,936
Likes
382
Points
180
Age
86
T2015CCM

T2015CCM

JF-Expert Member
Joined Sep 13, 2012
7,936 382 180
Kifo cha chadema hakiepukiki.
 
T2015CCM

T2015CCM

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2012
Messages
7,936
Likes
382
Points
180
Age
86
T2015CCM

T2015CCM

JF-Expert Member
Joined Sep 13, 2012
7,936 382 180
Asante mungu kuichukua roho na mwili wa haya mauwaji watu kwa tindikali na sumu
 
A

assadsyria3

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2013
Messages
6,733
Likes
2,303
Points
280
Age
38
A

assadsyria3

JF-Expert Member
Joined Apr 9, 2013
6,733 2,303 280
Dk slaa ni janga la kitaifa
 
M

Mindi

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2008
Messages
2,009
Likes
2,041
Points
280
M

Mindi

JF-Expert Member
Joined Apr 5, 2008
2,009 2,041 280
Hii makala imeandikwa kiushabiki zaidi bila kuwa na "professionalism" ndani yake. katika gazeti hili la Raia Mwema toleo la 327 Jumatano wiki hii, nimeona pia maoni ya mhariri yako "biased" kuilaumu CHADEMA kwa maamuzi yake. pia makala ya Ahmed Rajab, inataja mambo mengi ambayo ni hisia tu za mwandishi na zinamshushia hadhi kwa sababu ni mwandishi mkongwe aliyebobea. mfano anasema Ahmed Rajab katika makala yake "Laana iliyopiga CHADEMA":

"Kinachowasikitisha wapenzi wa Chadema ni kusikia shutuma za udugu na udini au kama zile zilizotolewa na Kabwe dhidi ya wakuu wa chama. yeye hakuutaja udugu wala udini lakini aliyoyaelezea yanaonesha kwamba wakuu wenzake wa Chadema hawaelewi nini hasa maana ya Demokrasia na kama wanaielewa basi wanaikiuka misingi yake kwa makusudi. ikiwa shutuma zote hizo ni za kweli basi wakuu na wafuasi wa chadema wana kazi kubwa. na kazi yenyewe ni ya kuimarisha demokrasia ndani ya chama chao. uimarishaji huo hauwezi kutokea kwa mkupuo mmoja"

Yaani uandishi wa ajabu kabisa! kwa sentensi moja tu tayari ameshaihukumu CHADEMA kwamba ina makosa ya 1)udini, 2)udugu, na 3)kutozingatia misingi ya demokrasia. amechukua "shutuma" zinazotolewa hata na wapiga propaganda kuwa ndio ukweli wenyewe, na amechukua maelezo ya zitto kuwa ndio ukweli wenyewe na "akajenga hoja"!!

Hawa wote wa Raia Mwema wangefaidika sana kama wangesikiliza kipindi cha leo asubuhi cha "Tuongee Magazeti" cha Star TV. pale watu walionesha ukomavu kabisa katika uchambuzi. kwamba suala hapa siyo Zitto kuvuliwa vyeo vyake, bali chanzo cha yote hayo ni nini?

Mhariri wa Raia Mwema ndio kabisaa, analia machozi: "HATUTAUNGA MKONO UDHAIFU WA VYAMA". yaani hapo tayari ameona kuna udhaifu chadema kwa hatua zilizochukuliwa na kamati kuu! wala hatoi uchambuzi wowote kuonesha ni kwa lipi hasa Chadema wameonesha udhaifu. Historia itaihukumu Chadema, kama ilichofanya ni kuonesha uimara wake au ni kuonesha udhaifu wake. lakini ni vema wale wanaoshughulika kutuhabarisha wakazama katika kuchambua. mfano, iliongelewa katika kipindi cha Star TV kwamba Zitto hakutakiwa kufika katika kikao kikubwa kama kile akiwa amechelewa, hata kama alikuwa na "majukumu ya kitaifa". ukweli ni kwamba yeye ni mwenyekiti wa ile kamati ya Bunge kwa sababu ya hadhi yake ya Ubunge. na ni mbunge kwa sababu yuko CHADEMA. sasa yeye kama naibu katibu Mkuu alitakiwa ndio mmoja ya watu muhimu katika kuandaa kikao kile. na kama kingeamua kumvua uanachama, hata huo uenyekiti wa PAC ungeyeyuka pia, labda abebwe na mahakama. kwa hiyo madhaifu kama hayo kwa upande wa Zitto yanatakiwa pia yaanikwe. na mengine mengi tu.

Aliyenifurahisha katika toleo hili la Raia Mwema ni Ezekiel Kamwaga, aliyeandika makala nzuri sana na yenye balance: "Utatu wa tofauti kati ya Mbowe, Zitto na Slaa". hii ni makala iliyojaa weledi, utafiti, na tafakuri ya kina. inataja strengths and weaknesses za kila mmoja katika hao. hii unaweza kuijadili. pia kuna makala ya Lula wa Ndali Mwananzela, aliyeandika makala: "Mazuri, mabaya, ya kuudhi, kusikitisha na kuchekesha". hapa pia utaona Tafakuri Jadidi. unaewza ukaijadili makala kama hii. iko balanced. sio uchuro wa Ahmed Rajabu anayeelekea kuzeeka vibaya, na mhariri wa Raia Mwema ambaye anaonekana ana chuki binafsi na CHADEMA, au hawezi kuficha mapenzi yake kwa Zitto. nawashauri hawa wawili, kwa maneno ya Mwalimu Nyerere, kama wanampenda Zitto namna hiyo, wamkaribishe wanywe naye kahawa!!
 
Simiyu Yetu

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2013
Messages
18,936
Likes
1,600
Points
280
Simiyu Yetu

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2013
18,936 1,600 280
Chama cha maruhani kinaendeshwa kimagumashi.
 
Simiyu Yetu

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2013
Messages
18,936
Likes
1,600
Points
280
Simiyu Yetu

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2013
18,936 1,600 280
Chadema ili ibadilike labda imwagiwe tindikali ndipo itaweza kubadilika lakini kwa ushauri tu kimeshindikana.
 
A

assadsyria3

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2013
Messages
6,733
Likes
2,303
Points
280
Age
38
A

assadsyria3

JF-Expert Member
Joined Apr 9, 2013
6,733 2,303 280
Dk slaa ataiua chadema na huyu mshumbuz kihereherea
 
Forum statistics

Threads 1,251,958
Members 481,948
Posts 29,791,579