Nilufer
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 9,568
- 13,543
WAPINZANI WAMEKOSA AGENDA ZA KUJENGA VYAMA VYAO
Wapinzani wa Tanzania wamekosa agenda za kisiasa ndio maana wameamua kubeba agenda za kinafiki
Leo hii wanasubiIia agenda kutoka mitandaoni ndio ziwe agenda za chama tena kwa habari za majungu na unafiki uliotukuka
Leo hii kiongozi wa agenda zao ni Gwajima na yule dada wa ughaibuni
Miaka ya nyuma walipiga sana kelele tena kwa muda wa miaka nane.Walipita kila wilaya na kila mkoa ndani ya Tanzania bara na visiwani kutuaminisha watanzania kuwa chama cha mapinduzi kina lea mafisadi wakubwa na mapapa
Kwa kukosa agenda kabisa wakaamua kuandaa operation waliyoibatiza jina la OPERATION SANGARA na wakapita kila mkoa kwenda kufanya mikutano ya kuitangaza hii operation yao na kila mkoa walipopita walitaja hadharani kuwa Edward Lowasa ni fisadi papa na wakatuaminisha kuwa ushahid wanao
Katika mkutano wao walioufanya katika viwanja vya mwembe yanga viongozi wa chadema taifa wakiongozwa na katibu mkuu wao Dr Slaa walikuja na majina ya mafisadi papa kama wao walivyoyabatiza na wakaibatiza pia hiyo list ya mafisadi kuwa LIST OF SHAME
Katika list of shame Edward Lowasa alikuwemo kama fisadi papa na fisadi nyangumi
Katibu mkuu wa chadema alitangaza kabisa kuwa ushahidi wa lowasa kuwa fisadi wanao na hata John Mnyika alisema kuwa ushahid wa ufisadi wa lowasa anao
Kitu ambacho kilikuwa kinasubiliwa kwa hamu kubwa ni hawa wenye ushahid wa ufisadi wa lowasa kwenda mahakamani kupeleka ushahidi wao ili sheria za nchi zifuatwe na lowasa achukuliwe hatua
Hakuna kiongozi yeyote yule kutoka chadema pamoja na wale wote waliokuwa wanasema wana ushahidi wa ufisadi wa lowasa aliyejitokeza kwenda mahakamani yaani wote waliishia kupiga fujo kwenye majukwaa tu na kutaka sifa zisizo na uhalali
Kwa mujibu wa sheria za nchi yetu chombo chenye mamlaka ya kutangaza kuwa huyu mtu ni mwizi au ni fisadi ni mahakama tu tena wanafanya hivyo baada ya kuwa na ushahidi uliotukuka
Baada ya miaka nane chadema hawa hawa waliokuwa wanatangaza kuwa lowasa ni fisadi na ushahidi wanao walimpokea tena kwa kumpigia magoti ili ajiunge na chama chao
Mshenga mkubwa wa huu mchezo alikuwa ni askofu wa kanisa la ufufuo na uzima ndugu Gwajima ambaye huyu huyu anayejiita askofu alivunja ndoa ya mtumishi wake
Lowasa akakubali kuwa mwanachama wa chadema na akapewa nafasi ya ujumbe wa kamati kuu ya chadema na pia kuwa mgombea wa urais kupitia chadema na vyama vinavyounda ukawa
Sasa mimi najiuliza ufisadi wa lowasa uliisha lini? Lowasa ni wapi alisafishwa na mahakama kuwa sio fisadi tena? Ule ushahidi waliokuwa wanasema wanao kuhusu ufisadi wa huyu mzee ulipotelea wapi.? Kaka yangu John Mnyika ushahid wako uliosema wa ufisadi wa lowasa uliliwa na panya?
Baada tena ya muda kupita wameibuka tena na tuhuma za kufoji cheti kwa mkuu wa mkoa wa Dsm lakini njia wanayoutumia ni ile ile waliyoitumia kwa lowasa
Hivi chadema na washabiki wenu mnapajua Necta? Necta walitoa tangazo kuwa mwenye kujua au mwenye taharifa za mtu anayetumia cheti cha mtu apeleke ushahidi, Sasa kwanini mnashindwa kupeleka huo ushahidi na mnakalia habari za vijiweni tu.?
Kama Gwajima anao ushahidi kuhusu hivyo vyeti kwanini anashindwa kwenda Necta kupeleka huo ushahidi?
Kwanini Gwajima asiende mahakamani kufungua kesi ili mahakama imuite muhusika na huyo Gwajima apeleke huo ushahidi?
Kwa lowasa mlipiga fujo hivi hivi na baadae mkampigia magoti na mmekaa na yeye meza moja mnakula nae na kunywa nae mmeshasahau kuwa ni fisadi sasa hivi
Mimi naona mmekosa agenda za kuvibeba vyama vyenu na hata agenda yenu ya ufisadi kwa sasa huwezi kuisikia kwa kiongozi yeyote yule wa chadema maana mafisadi sasa wapo chadema
Mnyika siku hizi yupo kimya hana la kusema, Zile kelele zake zote zimekwisha amekuwa kama kuku aliyekoswa na mwewe tu
Mara ya mwisho kusikia mbowe akisema chama chake kinapambana na ufisadi nadhani ilikuwa 2014
Mimi binafsi nawashauri kama mnavyosema kuwa ushahidi wa vyeti mnao sasa ni bora muende mahakamani sasa kuliko kupiga fujo mitandaoni maana Makonda binafsi hawezi kujibu habari za mitandaoni
Chadema acheni siasa za kitoto badilikeni
Kidumu chama cha mapinduzi
NDIMI
RAPHAEL LUKINDO