Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,280
- 25,859
Hakuna shaka kuwa,pamoja na uwepo wa UKAWA,CHADEMA ndicho chama kikuu cha upinzani Tanzania kwasasa. Pamoja na kunawiri na kupanda kwa idadi ya Wabunge,Madiwani na Wenyeviti wa mitaa,vijiji na vitongoji kwenye chaguzi,CHADEMA imebaki na suala moja ambalo hukitia aibu chama hicho kikuu cha upinzani nchini hasa wakati wa uchaguzi.
Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1992,CHADEMA wamekuwa hawana ofisi za kueleweka za mikoa,wilaya,kanda na hata mitaa achilia mbali mashina. Ni aibu,kwa maoni yangu,chama kama hiki kupanga mafremu na kuyafanya ofisi zake. Ni aibu,naamini,kwa miaka yote tangu kuanzishwa CHADEMA kukosa mipango mikakati ya kupata ardhi na kujenga ofisi zake.
Ifike mahali CHADEMA iwe pia na vitega uchumi vyao. Kimsingi,kama chama kilichokomaa,kinachoaminika na kukubalika kinapaswa kuwa na ofisi zao kwenye ardhi yao pamoja na kuwa na vitega uchumi vyake vya kueleweka.