Ulichoongea ni sahihi kabisa. Hawa watu wangeachwa wazunguke wanavyotaka, waongee wanavyotaka mwisho wasingepata attention yoyote!
Mbowe baada ya msiba wa Magufuri amezunguka karibu kanda zote! Ameyasema yote ya moyoni yaliyokuwa yanamsibu, leo si maisha yanasonga tu! Wa kwanza kuchoka ni hao hao wafuasi wake
CHADEMA wanashindwa sehemu ndogo sana! Hawana subira! Wahenga walisema subira ya vuta heri na mvumilivu hula mbivu
Rais ameapishwa tu kushika madaraka huku Taifa likiwa kwenye maombolezo, wao kesho yake washaandika barua ya kuomba mwaliko! Sio kwa haraka zile
Mpaka Sasa ni miezi minne tu tangu achukue madaraka lakini wao lawama zimeshakuwa nyingi
Ndani ya miezi hii minne walitaka wawe wameshaonana na Rais, katiba mpya iwe imeshapatikana, nk.....Kukaa na wapinzani ni jambo jema kabisa lakini mtu mzima halazimishwi kutekeleza jambo
Kwa hali ilivyo Sasa, hata mwaliko walioomba ulishakosa umaalumu tena maana ni Kama imekuwa lazima