Kuungana na yeyote ni kiini macho Mkuu, tumeshuhudia kejeli za wabunge wachadema, dhidi ya wabunge wa CUF, tumeshuhudia jinsi walivyo kuwa wakijisifu na kujigamba wao ndio wenye idadi kubwa ya wabunge hivyo hawahitaji kuungana na chamachochote na wakafanya hivyo, tumeshuhudia matusi kutoka kwa, Mchungaji Msingwa dhidiya CUF, tumeshuhudia matusi ya Mh. Wenje dhidi ya upinzani, tumemshuhudia mwanadada machachari wa chadema Halima Mdee nae akiwakejeli wapinzani ndani yabunge, achilia mbali kejeli na dharau zaMh. Mkurugenzi wa sheria sijui Tundu Lisu dhidi ya CUF na upinzani wote.
Sasa Baada yakupoteza nguvu ya ushawishi na mvuto kwa wananchi, iliwalazimu Chadema kurudinyuma na kula matapishi yao wenyewe. Hapa inaonyesha Chama hiki hakipo kwamaslahi ya umoja wao huo ulioundwa kwa mgongo wa katiba mpya, laiti kamawangalikua na uwezo wa kusimama wenyewe wasingeli mkaribisha mtu yeyote Yule.
Tunasubiri kwa hamu kubwa kuona kama watakubali ProfesaLipumba awe mgombea wa UKAWA, hapa sasa zitaanza kutolewa sababu kibao ilituwajitenge.