Sir John Roberts
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 12,426
- 22,902
Tundu Antiphas Lissu
Mbunge kutoka Jimbo la Singida mashariki.ameonesha uwezo usio na Mashaka katika siasa za Kupambana na Utawala uliojaa Chuki, Visasi, Dharau, kejeli na ubabe wa Rais aliyeko madarakani.
Nathubutu kusema huyu bwana ameamua kujitoa nafsi katika kutetea utawala wa haki na sheria katika nchi hii.
Nitaeleza baadhi ya hoja za msingi ambazo amezisimamia binafsi kwa manufaa ya Nchi hii.
1. Uhuru wa kujieleza
Rais baada ya kuingia madarakani alitangaza rasmi kupiga marufuku Uhuru wa mikutano ya kisiasa ,watu au vikundi vya watu kuandamana na kukusanyika kueleza fikra zao. Ni Tundu Lissu aliyepinga hadharani suala hili na kukamatwa kwa makosa ya uchochezi.
2. Kutetea utawala wa sheria ,haki na wajibu wa serikali kwa Wananchi
Nakumbuka baada ya maafa ya tetemeko la Ardhi mkoani kagera Serikali kupitia kwa Rais ilitangaza kwamba hakutakua na msaada kwa yeyote aliyepata madhara na kwamba watu wafanye kazi kwakua tetemeko halikuletwa na serikali. Ni huyu Tundu Lissu alisimama akaeleza kwamba Serikali ina wajibu wa kuwasaidia watu wake kwa kuwa wanalipa kodi na mojawapo ya matumizi ya kodi zao ni kusaidia majanga kama hayo licha ya msaada lukuki iliyotolewa na watanzania na Wahisani walioguswa na Janga hilo.
3. Tundu Lissu kutangaza hadharani kuwania nafasi ya Urais wa chama cha Wana sheria nchini ( Tanganyika Law Society)
Hapa ni kama Tundu Lissu aliichikoza Serikali ambayo tayari Rais alishatoa warning kwa chama hiki kwamba anasikia kuna mtu kutoka chama cha Upinzani anataka kuwania urais na akasema wazi kuwa Never and Never hilo halitawezekana. Kama mnakumbuka Tundu Lissu aliamua kuchukua fomu ya kuwania urais wa TLS baada ya kusikia kauli ya Rais Magufuli katika siku ya kuadhimisha wana sheria. Kwangu huu ulikuwa ni ujasiri uliopotiliza kiwango
Kwa uchache Tundu Lissu ameonesha ujasiri wa Kupambana na Bwana John Magufuli. Nawaasa chadema hakuna Mwanaume anaeweza kuisumbua hii serikali ya ccm kwa sasa kama Tundu Lissu. Simfahamu wala sijawahi kumuona lakini nadiriki kuwa yeye ndio yeye.
Tayari ccm wamethibitisha kuwa 2020 ni John Magufuli na kiboko yake ni Tundu Lissu ana hoja za msingi na akisimama wananchi wenye vyeti ( Akili) tunamuelewa.
Chadema kama mnamasikio mnisikie mimi huwa siandiki mara kwa mara hapa Jamii Forum lakini kwa hili nimesukumwa niwaeleze.
Mwangalieni atawaokoa.
Karibuni.