CHADEMA naomba mfanye hili! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA naomba mfanye hili!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mwanamayu, Sep 21, 2010.

 1. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #1
  Sep 21, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,938
  Likes Received: 2,087
  Trophy Points: 280
  Inasemekana CCM wanajulikana sana vijijini kwani wako huko toka katika mfumo wa chama kimoja cha siasa. Kama ni kweli, je Chadema mtafanya kampeni kila kijiji? Kama hapana, sasa mtawafikiaje hawa wapiga kura? Nionavyo mimi ni vizuri kubandika picha za wagombea wenu hasa wa urais kwenye kila kijiji sehemu za public kama sokoni au gulioni ili wananchi kule wajue kuna chama kingine na mgombea urais mwingine - ile picha na neno CHADEMA (kwa wanaojua kusoma) yakiikiingia kwenye akili zao wanaweza kuiwekea tick picha ya Dr. Slaa siku ya uchaguzi watakapo kutana nayo - this is scientific. Kama hii ni ngumu, basi vetengenezwe vipicha vidogo kama A5 size ambavyo vitagawiwa kwenye mabasi yote yanayofanya safari nchini - ya mikoa, wilaya na vijiji na kumwomba kondakta baada ya kupewa token/ dispatch payment kudondosha idadi fulani ya vipepelushi hivyo kwenye stendi na wanakijiji kuokota na kupata ujumbe na picha ya Dr. Slaa ambako haijafika au haitafika kwa njia nyingine ile. Nasema hili kutokana na uzoefu wangu jinsi barua zinavyotumwa vijijini ambako hakuna posta - barua hudondoshwa kwenye stendi ya basi na wanakijiji uikota na kumpelekea mhusika, pia mara basi linapofika stendi wanakijiji ujazana ili kuokota barua, kupata taarifa za mdomo, sehemu ya kiburudisho na kadhalika.

  Wazo hili ni copyrighted na ninawapa Chadema permission ya kulitumia na mwingine hasijedai right hii!!
   
 2. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #2
  Sep 21, 2010
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Inaweza saidia lakini cha muhimu ni kuwafikia hukohuko vijijini na kumwaga sera
   
 3. Naloli

  Naloli JF-Expert Member

  #3
  Sep 21, 2010
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 416
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mwanamayu nimekupata na kukubaliana na mawazo yako lakini kwangu naona njia ya kwanza ni nzuri zaidi ya kusambaza picha vjijiji vyote ili mgombea wa CHADEMA na anayeungwa mkono na sisi Wanaharakati wa ukombozi wa nchi hii afahamike na iwe rais kumkumbuka tarehe 31 oct. Lakini ni vyema tukakumbuka mambo yote hayo yanaitaji fedha na je CHADEMA inajiweza kiuchumi?Je kwa kutegemea karuzuku kiduchu inachopata toka Serikalini itaweza kufanikisha kampeni kwa wagombea URAIS,UBUNGE na UDIWANI nchi nzima. Si chadema, Cuf wala Nccr na vyama vingine vyenye uwezo wa kujimudu kikampeni kulinganisha na CCM.Kwa kuongezea maoni yako mwanamayu nashauri yafuatayo:-

  Wapenda mabadiliko na wachukia ufisadi bila kujali itikadi za vyama, tuwe wazalendo na wapenda nchi yetu tuchangie vyama vyenye uelekeo wa kuleta mabadiliko ili BUNGE lijalo liwe Bunge la watanzania. Changia mgombea UBUNGEA na UDIWANI mwenye uchungu na watanzania na mwenye muelekeo wa kutetea rasilimali za nchi yetu, mchukia ufisadi toka moyoni bila kujali anatoka chama gani (chagua mtu usichague chama) . Kuhusu RAIS Chagua SLAA kwa maendeleo yako,chagua SLAA kwa usalama wa maliasili za Taifa, chagua SLAA kwa kutokomeza ufisaida, chagua SLAA kwa elimu kwa watanzania wote wenye nacho na wasiokuwa nacho, chagua SLAA kwa afya bora. chagua SLAA kwa amani na utulivu bila kunyanyaswa na viongozi, chagua SLAA kwa usalama wa nchi yako. ILI SLAA aweze kuingia IKULU unaitajika mchango wa hali na mali unaitajika. Ili wabunge wapiganaji waweze kuingia BUNGENI mchango wako unaitajika.

  WATANZANIA CHADEMA wametoa AKAUNTI ZAO, maelezo ya kuchangia kwa simu nk CUF nao wametoa jinsi gani ya kuwachangia angalia wapi kwa kuchangia ili kuiokoa TANZANIA. Muungeni mkono SABODO japokuwa ni mwana CCM amechangia TSH, MILLION 100 kwa CHADEMA. TUUNGENI MKONO SISI WANAHARAKATI kwa KUCHANGIA kiongozi sahihi kwa watanzania kwa sasa DK SLAA. changia SLAA changia MAENDELEO tokomeza Ufisadi kwa KUMCHAGUA SLAA
   
 4. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #4
  Sep 21, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160

  tatizo letu watanzania ni kiutaka mafanikio pasipo kujitoa, ndio maana ccm wakabuni mbinbu za kifisadi kufanikisha malengo yao. Kinachotakiwa ni sisi wapiganaji kujitoa zaidi kifedha kuwezesha chadema kuchapisha hizo picha. Je hilo tumefanya? Kila mmoja wetu katiamiza wajibu wake katika hili?
   
 5. PlanckScale

  PlanckScale JF-Expert Member

  #5
  Sep 25, 2010
  Joined: Sep 28, 2008
  Messages: 510
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35

  Jee CCM wanaonaje kitendo cha SABODO kuichangia CHADEMA?
  Jee SABODO bado yuko CCM?

  Angekuwa SABODO hana chama ningeelewa. Lakini kama bado yuko CCM, basi hizo pesa zina utata, no mater how you look at it.

  Alafu pia, kukubali mchango mkubwa kutoka kwa mtu mmoja kuna hatarisha demokrasia...ndiomana wenzetu Marekani wana limit michango kama hiyo...

  The FEC and the Federal Campaign Finance Law Brochure

  Tuna safari ndefu
   
Loading...