Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,347
- 26,153
Hakika mkuu wabunge wa chadema wote hovyo kabisa.Chadema uchaguzi mwakani hawatapata mbunge hata mmoja, wabunge wote wa chadema hakuna kitu wamefanya kwenye majimbo yao zaidi ya vurugu na maandamano..
Hakika mkuu wabunge wa chadema wote hovyo kabisa.
Nilikuwa Arusha kuhudhuria Kongamano na Mkutano wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS). Vyote vilifanyika kwa siku moja,yaani Jumamosi ya tarehe 16/8/2014 AICC. Pale Arusha,kulikuwa ni mahali pa kukutana na Mawakili Wasomi mbalimbali waliotawanyika nchini na kubadilishana mawazo.
Moja ya mazungumzo ilikuwa ni hali ya kisiasa hapa nchini.Mazungumzo haya yalifanyika wakati wa mapumziko ya chai au chakula cha mchana. Wakili Msomi mmoja akatoa hoja kuwa unapofanyika uchaguzi hapa nchini,wagombea wa upinzani hasa CHADEMA hupambana na wapinzani wa aina tatu. Kwanza, vyombo vya dola.Mgombea itampasa kupambana na changamoto na mikwaruzo mbalimbali kutoka vyombo vya usalama na kuvishinda kwa kulindwa na mapenzi ya wananchi juu yake.
Pili,mgombea atapambana na mgombea mwenzake wa chama tawala au kinginecho. Yampasa kujenga hoja ili akubalike zaidi ya mwenzake. Na tatu,Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Mgombea husika lazima apambane na Tume kwa namna kama ya 'kulazimisha' matokeo kutangazwa. Pia,kupambana kuepuka kuibiwa kwa kura zake na kutangazwa mwingine badala yake.
Wakili Msomi huyo akamaliza kwa kusema kuwa Wabunge wote wa Majimbo wa CHADEMA wamepambana na 'wapinzani' hao na kuwashinda. Hivyo,si jambo dogo kuwaona Bungeni. Wamefanya kazi kwelikweli. Ni mashujaa. Hivyobasi,ni watu wapambanaji,shupavu na wa kupigiwa mfano. Ni chaguo hasa la wananchi. Akamaliza kwa kusema,mwaka 2015 itakuwa kazi pevu kuwapoka Ubunge wabunge wa aina hii.
Mjadala ulikuwa mkali kwa kila Wakili Msomi aliyekuwepo hapo mazungumzuni kuwa na mtazamo wake. Nami,nikabaki kujifunza jambo tu. Nilikuwa Junior Counsel kuliko wote kwahiyo nikabaki kuwa msikilizaji.
Waungwana,kuna ukweli wowote hapa?
Chadema bonge la
chama, mageti yote hutangaza chadema, ccm wote hutangaza chadrma, tv
zote hutangaza chadema, radio zote hutanga chadema! Mtaitangaza chadema
kwanjia zote bila hata nyiwe wenyewe kujua kama mnaitangaza. Well done
chadema.
Nilikuwa Arusha kuhudhuria Kongamano na Mkutano wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS). Vyote vilifanyika kwa siku moja,yaani Jumamosi ya tarehe 16/8/2014 AICC. Pale Arusha,kulikuwa ni mahali pa kukutana na Mawakili Wasomi mbalimbali waliotawanyika nchini na kubadilishana mawazo.
Moja ya mazungumzo ilikuwa ni hali ya kisiasa hapa nchini.Mazungumzo haya yalifanyika wakati wa mapumziko ya chai au chakula cha mchana. Wakili Msomi mmoja akatoa hoja kuwa unapofanyika uchaguzi hapa nchini,wagombea wa upinzani hasa CHADEMA hupambana na wapinzani wa aina tatu. Kwanza, vyombo vya dola.Mgombea itampasa kupambana na changamoto na mikwaruzo mbalimbali kutoka vyombo vya usalama na kuvishinda kwa kulindwa na mapenzi ya wananchi juu yake.
Pili,mgombea atapambana na mgombea mwenzake wa chama tawala au kinginecho. Yampasa kujenga hoja ili akubalike zaidi ya mwenzake. Na tatu,Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Mgombea husika lazima apambane na Tume kwa namna kama ya 'kulazimisha' matokeo kutangazwa. Pia,kupambana kuepuka kuibiwa kwa kura zake na kutangazwa mwingine badala yake.
Wakili Msomi huyo akamaliza kwa kusema kuwa Wabunge wote wa Majimbo wa CHADEMA wamepambana na 'wapinzani' hao na kuwashinda. Hivyo,si jambo dogo kuwaona Bungeni. Wamefanya kazi kwelikweli. Ni mashujaa. Hivyobasi,ni watu wapambanaji,shupavu na wa kupigiwa mfano. Ni chaguo hasa la wananchi. Akamaliza kwa kusema,mwaka 2015 itakuwa kazi pevu kuwapoka Ubunge wabunge wa aina hii.
Mjadala ulikuwa mkali kwa kila Wakili Msomi aliyekuwepo hapo mazungumzuni kuwa na mtazamo wake. Nami,nikabaki kujifunza jambo tu. Nilikuwa Junior Counsel kuliko wote kwahiyo nikabaki kuwa msikilizaji.
Waungwana,kuna ukweli wowote hapa?
Mkuu MSALANI,tafadhali elewa.Hivi mtu akiitaja Uingereza anageuka kuwa Mwingereza. Nakuheshimu sana. Sipendi malumbano nawe.Ukitaka niwe CHADEMA,niletee kadi
Umeanzisha mjadala mzuri lakini umeshapokwa na mijitu ya Lumumba akina Msalani, laki si pesa, inakuwa vigumu kwa watu makini kuchangia. Lakini asante kwa kutupa angalizo hili.Mkuu MSALANI,tafadhali elewa.Hivi mtu akiitaja Uingereza anageuka kuwa Mwingereza. Nakuheshimu sana. Sipendi malumbano nawe.Ukitaka niwe CHADEMA,niletee kadi